Hii Quotes

We've searched our database for all the quotes and captions related to Hii. Here they are! All 67 of them:

β€œ
Ikiwa hakuna kitu kinafanyika katika maisha yako usijali. Kuna kitu kinafanyika – kuingia na kutoka kwa hii pumzi.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Gari hii ni nzuri kuendesha.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
hii
”
”
Testy McTesterson (The Saga of Greguin)
β€œ
Mungu anatupenda sana, ndiyo maana akamleta Mwanawe wa pekee ili afe kwa ajili yetu, lakini haupendi mfumo wa maisha wa dunia hii.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Tunaishi katika urazini wa kuwili mwenzangu, kujijua kupitia macho ya wengine; tunaishi pembezoni. Hii ndiyo tanzia ya rangi!
”
”
K.W. Wamitila (Bina-Adamu!)
β€œ
he sobs, this fearless man who buried hiis parents and crossed oceans, who fell in love with a woman he barely knew and built a life with her in a desolate place i miss her, abu whispers. she knew all my secrets
”
”
Sabaa Tahir (All My Rage)
β€œ
Familia yako haikusaidii chochote katika mipango ya takdiri yako. Hii inasikitisha sana. Unajitahidi kila siku kuwafurahisha watu unaowapenda na watu wako wa karibu. Kila ukijitahidi kupata kibali cha watu unaishia kudharaulika na kuonekana mjinga asiyekuwa na maana. Sikiliza mazungumzo ya ndani ya moyo wako. Wapendwa wako watakukubali kama mtu hodari asiyekata tamaa, na tena watakuheshimu kutokana na tabia zako hizo. Mabadiliko haya ya kifikra hayatatokea haraka kama unavyofikiria. Yatachukua muda. Hivyo, kuwa mvumilivu. Wakati huohuo, endelea kucheza ngoma uliyoianzisha mwenyewe, endelea na mipango yako kama akili yako inavyokutuma.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Kinachotokea katika dunia hii si kitu kizuri cha kuzoea au hata kufikiria. Hivyo tuna haki ya kuwa na mawazo, hasira na wanyonge kuhusiana na suala zima la maisha yetu hapa duniani. Hata hivyo hali hii itabaki kuwa hivyo kwa sababu Mungu ametaka iwe hivyo kwa sasa. Kwa maana hiyo, hekima ni kukubaliana na mapenzi ya Mungu. Lazima tukubaliane na kisichoweza kufikirika kuweza kubadilika.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Ningependa kujitokeza leo kutoa salamu zangu za rambirambi kwa Watu wa Musoma; kutokana na ajali mbaya ya mabasi ya J4 Express, Mwanza Coach, na gari ndogo aina Nissan Terrano, iliyotokea Ijumaa tarehe 5/9/2014 katika eneo la Sabasaba mjini Musoma. Kulingana na vyombo vya habari, watu 39 wamefariki dunia. Wengine wengi wamejeruhiwa vibaya. Mali za mamilioni ya fedha zimeteketea kabisa. Hii ni ajali mbaya na ya kusikitisha mno kwa maana halisi ya maneno mabaya na ya kusikitisha. Maneno hayataweza kuelezea kikamilifu huzuni niliyonayo juu ya ajali hii ya kutisha, lakini Mungu awasaidie wale wote waliofiwa au walioguswa na ajali hiyo kwa namna yoyote ile, na awasamehe marehemu wote dhambi zao na awapumzishe mahali pema peponi. Wale wote waliofariki hawataweza kurudi huku, lakini sisi tutakwenda huko.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Mwili wako una uwezo wa kujua kabla yako kitakachotokea baadaye. Kama una njaa kwa mfano, mwili wako utakwambia. Kama una kiu, mwili wako utakwambia. Kama unaumwa, mwili wako utakwambia. Kama kuna kitu kibaya kinatarajia kutokea katika maisha yako au katika maisha ya mtu mwingine, mwili wako utakwambia. Kuwa makini na alamu zinazotoka ndani ya mwili wako, kwani hizo ni ishara za Roho Mtakatifu kukuepusha na matatizo ya dunia hii.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Kutokana na utafiti wa kisayansi wa kionairolojia ambayo ni sayansi ya ndoto; wakati tumelala, sehemu yetu ya akili isiyotambua huamka na kuanza kazi; kwa kupangilia mawazo, kuanzia mawazo ya siku iliyopita, na kuimarisha mahusiano baina ya mawazo hayo na matukio ya wakati ujao, huku ikiondoa mawazo yasiyokuwa na maana, kunusuru ubongo usielemewe na msongo. Kazi hiyo hutambuliwa haraka na akili inayotambua, kwa njia ya alamu, lakini akili inayotambua inapagawa kwa sababu haijui akili isiyotambua inamaanisha nini kutuma alamu kama hizo. Kwa hiyo inajaribu kwa kadiri inavyoweza kutunga hadithi kuhusiana na vitu mbalimbali, ambayo baadaye hutafsiriwa kama ndoto. Hii ndiyo sababu tunaota ndoto za ajabu ambazo aghalabu hazina maana yoyote, na hazina maana yoyote kwa sababu hazitakiwi kuwa na maana yoyote, na hazina ujumbe wowote halisi kutoka akilini mwetu. Hayo ni matokeo ya akili kujaribu kusanisi sauti, kutoka katika akili isiyotambua.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Taabini hii ni ngumu sana kwangu kuandika pamoja na kwamba ni miaka mitatu kamili toka giza liingie. Mwaka 2014, Novemba 4, nilimpoteza bibi yangu mpendwa, Martha Maregesi, aliyefariki dunia kutokana na ukongo wa kiharusi, na tutamkumbuka daima. Alikuwa na roho ya kipekee; na kifo chake kiliwagusa wengi, pamoja na kwamba aliishi maisha kamili, zaidi ya siku 25550, siku 5110 zaidi, ambazo ndizo tulizopangiwa na Mungu. Mapenzi ya mtu kwa bibi yake ni mapenzi ya kipekee. Nadhani Mungu aliwapa mabibi wote uwezo maalumu wa kuwapenda wajukuu zao, na kufanya maisha yao yatimie, kuwafanya wawe binadamu wazuri na wenye maadili mema. Alichangia pakubwa katika malezi yangu ya utotoni; na aghalabu naweza kukumbuka nikiwa naye jikoni akipika, huku mimi nikifanya kazi nyingine, lakini wakati huohuo akinifundisha mambo kadha wa kadha ya kunikomaza kimaisha. Bibi hakuwa tu bibi. Alikuwa mlezi, rafiki na mtu aliyenihamasisha sana katika maisha. Kifo kinaleta huzuni lakini kinaleta tumaini. Naamini bibi yangu atakwenda mbinguni, kwa sababu naamini alitubu dhambi zake akisaidiwa na wachungaji. Wachungaji hao walimtembelea kila siku, nyumbani au hospitalini, akiwa kitandani kwake akiugua. Bibi yangu alitimiza wajibu wake. Alizaliwa, aliishi, na alikufa katika toba. Siku nitakapokufa ningependa kuzikwa jirani na alipozikwa bibi yangu, ili Yesu atakaporudi tufufuke pamoja.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Kamishna … karibu," alisema Nafi huku akisimama na kutupa gazeti mezani na kuchukua karatasi ya faksi, iliyotumwa. "Ahsante. Kuna nini …" "Kamishna, imekuja faksi kutoka Oslo kama nilivyokueleza – katika simu. Inakutaka haraka, kesho, lazima kesho, kuwahi kikao Alhamisi mjini Copenhagen," alisema Nafi huku akimpa kamishna karatasi ya faksi. "Mjini Copenhagen!" alisema kamishna kwa kutoamini. "Ndiyo, kamishna … Sidhani kama kuna jambo la hatari lakini." "Nafi, nini kimetokea!" "Kamishna … sijui. Kwa kweli sijui. Ilipofika, hii faksi, kitu cha kwanza niliongea na watu wa WIS kupata uthibitisho wao. Nao hawajui. Huenda ni mauaji ya jana ya Meksiko. Hii ni siri kubwa ya tume kamishna, na ndiyo maana Oslo wakaingilia kati." "Ndiyo. Kila mtu ameyasikia mauaji ya Meksiko. Ni mabaya. Kinachonishangaza ni kwamba, jana niliongea na makamu … kuhusu mabadiliko ya katiba ya WODEA. Hakunambia chochote kuhusu mkutano wa kesho!" "Kamishna, nakusihi kuwa makini. Dalili zinaonyesha hali si nzuri hata kidogo. Hawa ni wadhalimu tu … wa madawa ya kulevya." "Vyema!" alijibu kamishna kwa jeuri na hasira. Halafu akaendelea, "Kuna cha ziada?" "Ijumaa, kama tulivyoongea wiki iliyopita, nasafiri kwenda Afrika Kusini." "Kikao kinafanyika Alhamisi, Nafi, huwezi kusafiri Ijumaa …" "Binti yangu atafukuzwa shule, kam …" "Nafi, ongea na chuo … wambie umepata dharura utaondoka Jumatatu; utawaona Jumanne … Fuata maadili ya kazi tafadhali. Safari yako si muhimu hivyo kulinganisha na tume!" "Sawa! Profesa. Niwie radhi, nimekuelewa, samahani sana. Samahani sana.
”
”
Enock Maregesi (Kolonia Santita)
β€œ
Biblia pamoja na historia vinatwambia kuwa mitume kumi na wawili wa Yesu Kristo waliamua kufa kinyama kama mfalme wao alivyokufa, kwa sababu walikataa kukana imani yao juu ya Yesu Kristo. Mathayo alikufa kwa ajili ya Ukristo nchini Ethiopia kwa jeraha lililotokana na kisu kikali, Marko akavutwa na farasi katika mitaa ya Alexandria nchini Misri mpaka akafa, kwa sababu alikataa kukana jina la Yesu Kristo. Luka alinyongwa nchini Ugiriki kwa sababu ya kuhubiri Injili ya Yesu Kristo katika nchi ambapo watu hawakumtambua Yesu. Yohana alichemshwa katika pipa la mafuta ya moto katika kipindi cha mateso makubwa ya Wakristo nchini Roma, lakini kimiujiza akaponea chupuchupu, kabla ya kufungwa katika gereza la kisiwa cha Patmo (Ugiriki) ambapo ndipo alipoandika kitabu cha Ufunuo. Mtume Yohana baadaye aliachiwa huru na kurudi Uturuki, ambapo alimtumikia Bwana kama Askofu wa Edessa. Alikufa kwa uzee, akiwa mtume pekee aliyekufa kwa amani. Petro alisulubiwa kichwa chini miguu juu katika msalaba wa umbo la X kulingana na desturi za kikanisa za kipindi hicho, kwa sababu aliwaambia maadui zake ya kuwa alijisikia vibaya kufa kama alivyokufa mfalme wake Yesu Kristo. Yakobo ndugu yake na Yesu (Yakobo Mkubwa), kiongozi wa kanisa mjini Yerusalemu, alirushwa kutoka juu ya mnara wa kusini-mashariki wa hekalu aliloliongoza la Hekalu Takatifu (zaidi ya futi mia moja kwenda chini) na baadaye kupigwa kwa virungu mpaka akafa, alipokataa kukana imani yake juu ya Yesu Kristo. Yakobo mwana wa Zebedayo (Yakobo Mdogo) alikuwa mvuvi kabla Yesu Kristo hajamwita kuwa mchungaji wa Injili yake. Kama kiongozi wa kanisa hatimaye, Yakobo aliuwawa kwa kukatwa kichwa mjini Yerusalemu. Afisa wa Kirumi aliyemlinda Yakobo alishangaa sana jinsi Yakobo alivyolinda imani yake siku kesi yake iliposomwa. Baadaye afisa huyo alimsogelea Yakobo katika eneo la mauti. Nafsi yake ilipomsuta, alijitoa hatiani mbele ya hakimu kwa kumkubali Yesu Kristo kama kiongozi wa maisha yake; halafu akapiga magoti pembeni kwa Yakobo, ili na yeye akatwe kichwa kama mfuasi wa Yesu Kristo. Bartholomayo, ambaye pia alijulikana kama Nathanali, alikuwa mmisionari huko Asia. Alimshuhudia Yesu mfalme wa wafalme katika Uturuki ya leo. Bartholomayo aliteswa kwa sababu ya mahubiri yake huko Armenia, ambako inasemekana aliuwawa kwa kuchapwa bakora mbele ya halaiki ya watu iliyomdhihaki. Andrea alisulubiwa katika msalaba wa X huko Patras nchini Ugiriki. Baada ya kuchapwa bakora kinyama na walinzi saba, alifungwa mwili mzima kwenye msalaba ili ateseke zaidi. Wafuasi wake waliokuwepo katika eneo la tukio waliripoti ya kuwa, alipokuwa akipelekwa msalabani, Andrea aliusalimia msalaba huo kwa maneno yafuatayo: "Nimekuwa nikitamani sana na nimekuwa nikiitegemea sana saa hii ya furaha. Msalaba uliwekwa wakfu na Mwenyezi Mungu baada ya mwili wa Yesu Kristo kuning’inizwa juu yake." Aliendelea kuwahubiria maadui zake kwa siku mbili zaidi, akiwa msalabani, mpaka akaishiwa na nguvu na kuaga dunia. Tomaso alichomwa mkuki nchini India katika mojawapo ya safari zake za kimisionari akiwa na lengo la kuanzisha kanisa la Yesu Kristo katika bara la India. Mathiya alichaguliwa na mitume kuchukua nafasi ya Yuda Iskarioti, baada ya kifo cha Yuda katika dimbwi la damu nchini India. Taarifa kuhusiana na maisha na kifo cha Mathiya zinachanganya na hazijulikani sawasawa. Lakini ipo imani kwamba Mathiya alipigwa mawe na Wayahudi huko Yerusalemu, kisha akauwawa kwa kukatwa kichwa. Yuda Tadei, ndugu yake na Yesu, aliuwawa kwa mishale alipokataa kukana imani yake juu ya Yesu Kristo. Mitume walikuwa na imani kubwa kwa sababu walishuhudia ufufuo wa Yesu Kristo, na miujiza mingine. Biblia ni kiwanda cha imani. Tunapaswa kuiamini Biblia kama mitume walivyomwamini Yesu Kristo, kwa sababu Biblia iliandikwa na mitume.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Sigara zilizidi kuvutwa, ndani ya nyumba, na magaidi wale wawili, wakati Murphy akisinzia kudanganyia kama kweli nguvu zilishamwisha. Alimfikiria tena mpenzi wake Sophia, safari hii sana. Alimkumbuka Debbie; hakujua alikuwa wapi na hakujua mama yake angefanya nini kama Debbie angekufa, na Murphy ndiye aliyetoka naye. Debbie alimuuma zaidi. Alimkataza kufa kwa ajili ya mchumba wake. Sasa alikufa kwa ajili ya mtu ambaye hakumjua. Murphy alijilaumu kumtongoza na kumchukua kwao na kulala naye na kula chakula chake cha kifalme. Wazazi wake wangejisikiaje kama angekufa, tena katika mazingira ya kutatanisha kama yale. Kufa alijua angekufa; lakini Mungu angemsaidia, awaage watu wake.
”
”
Enock Maregesi (Kolonia Santita)
β€œ
John Murphy amefariki dunia. Ndege aliyotoka nayo hapa, Dar es Salaam, ndiyo aliyotoka nayo Paris na ndiyo hiyo iliyoanguka katika mazingira ya kutatanisha. Watu waliobahatika kuing’amua fununu hii ni wachache na ambao hivi sasa hawajiwezi kabisa, akiwemo kamishna wetu wa kanda Profesa Mafuru. Profesa yuko mahututi. Ameshtuka baada ya kusikia taarifa hizo katika redio ya hapa. Yuko chini ya uangalizi mkali wa madaktari. Mungu aiweke roho ya John Murphy, shujaa wa karne, mahali pema peponi. Bwana alitoa na Bwana ametwaa. Jina la Bwana lihimidiwe.
”
”
Enock Maregesi (Kolonia Santita)
β€œ
Kujua nini kitatokea kesho, au kesho kutwa, au kujua jinsi usaili wako wa kazi utakavyokuwa, au ni maswali gani utakayoulizwa kwenye mtihani kwa mfano, kutarahisisha sana maisha yetu. 'Madirisha' madogo katika kipindi cha saa za usoni hufunguka mara kwa mara katika maisha yetu, kimiujiza na bila kutegemea. Hudokeza kidogo jinsi tukio fulani, au hali fulani, au kitu fulani kitakavyotokea katika kipindi cha wakati ujao bila sisi wenyewe kujua. Hali hii hujulikana kama jakamoyo. Jakamoyo ni sanaa ya kubashiri vitu visivyojulikana. Kazi yake ni kutuhadharisha na kutusaidia! Kujua mapema hatari iliyoko mbele yako inamaanisha kuwa na uwezo wa kujilinda kutokana na hatari hiyo, na kuwa na uwezo wa kuepuka mitego. Jakamoyo huweza kumtokea mtu katika hali ya 'maono', au 'mwako wa mwanga' (yaani kufumba na kufumbua). Mara nyingi huonekana kama ndoto. Hutokea wakati mtu amelala usingizi. Ikitokea wakati mtu yuko macho, wakati mwingine huendana na misisimko ya mwili kabla ya mwako, ikiwa na maana ya kumfanya mtu awe makini na kitu chochote kinachotarajia kutokea. Ndiyo maana baadhi ya watu utakuta wakisema wanaumwa tumbo, kifua au kichwa cha ghafla katika kipindi ambacho taswira ya tukio fulani inakuwa ikitokea akilini mwao, ikiwaambia waende mahali fulani bila kukosa kwa mfano, na kadhalika. Hakuna mtu anaweza kufanya jakamoyo imtokee. Hutokea yenyewe muda wowote kuleta ujumbe, kuhusiana na matukio ya wakati ujao. Kamwe usipuuze wito wa moyo wako.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Hii ni sheria ya akili yangu: Akili yangu ni muhimu kuliko familia yangu. Nisipoitunza vizuri akili yangu, sitaitunza vizuri familia yangu.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Mapenzi, kama ilivyo kwa vitu vyote hapa ulimwenguni, hayawezi kuwepo bila kujumuishwa na fizikia na kemia yake! Bila kemia hakuna mapenzi ya kudumu. Tamaa ya ngono kimsingi huanza pindi unapokutana na mtu. Tamaa hiyo huweza kukua na kuwa kitu kingine kadiri muda unavyokwenda lakini chanzo kinakuwepo toka siku ya kwanza mlipokutana. Kemikali inayosababisha tamaa ya ngono na hata kuikuza tamaa hiyo ni 'phenyl ethylamine' ('fino itholamine') au PEA ambayo ni kemikali ya mapenzi ndani ya ubongo. Husisimua watu na huongeza nguvu za kimwili (fizikia) na kihisia (kemia). Tamaa husababisha mtu azalishe PEA nyingi zaidi, kitu kinachosababisha kujisikia kizunguzungu (cha hisia za kimapenzi) na dalili zingine kama magoti kutetemeka, jasho kutoka viganjani na kutokutulia. Kemikali hii inapozalishwa kwa kiwango kikubwa, hutuma alamu ('signals') kutoka kwenye ubongo mpaka kwenye viungo vingine vya mwili na kutumika kama 'dopamine' au 'amphetamine' ambazo ni kemikali za ulevi ndani ya ubongo. Iwapo unajiuliza kwa nini wewe au mtu mwingine unavutiwa na mtu ambaye hamwendani kimapenzi, inaweza kuwa ni kwa sababu una kiwango kikubwa cha kemikali hizo kuliko mwenzako, kitu ambacho huzidi uwezo wa kutumia kichwa na kutoa maamuzi bora kulingana na akili ya kuzaliwa. Kwa jumla, mapenzi yote ya kweli uhitaji angalau kiwango kidogo cha PEA kwa wale wanaopendana. Cha msingi kukumbuka ni kwamba kemikali hizi huja kwa vituo, nikiwa simaanishi kwamba tamaa ya ngono hupotea pale mtu anapoelekea kwenye uhusiano wa kudumu. Lakini mambo hubadilika. Hatuwezi kuvumilia zile hisia kali kadiri tunavyozidi kusafiri kuelekea kwenye uhusiano wa kudumu na kwenye maisha ya pamoja yenye furaha. Katika uhusiano wenye afya hata hivyo matatizo hutokea hapa na pale. Chanzo cha Murphy na Debbie kupendana kilikuwa kemia zaidi kuliko fizikia. Kama hakuna kemia hakuna mapenzi.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Wakati mwingine inaweza kuonekana kuwa kadiri unavyozidi kujitolea kwa ajili ya watu wengine ndivyo unavyozidi kuwa maskini, lakini hii si kweli. Huduma kwa ajili ya watu wengine huleta maana fulani na ukamilifu katika maisha yetu kwa namna ambayo utajiri, madaraka na mali haviwezi kushindana nao. Mungu hababaishwi na kiasi gani unatoa. Anababaishwa na imani uliyonayo wakati unatoa. Ukitoa kidogo inatosha. Ukitoa kingi inatosha pia.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Kila mtu kabla ya kuzaliwa alipewa na Mwenyezi Mungu unabii na nyota ya ufalme. Una bahari ya fursa ya kuwa kitu chochote unachotaka kuwa katika dunia hii. Kama unataka furaha, furaha iko ndani yako. Kama unataka utajiri, utajiri uko ndani yako. Kama unataka amani, amani iko ndani yako. Kama wewe ni tone na fursa ni bahari, wewe ni bahari ndani ya tone.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Utajiri wa mbinguni ni wa milele na mungu wake ni Yehova. Utajiri wa duniani ni wa muda na mungu wake ni Mammon. Mammon, ambaye hata Yesu alimtaja katika Injili ya Mathayo 6 na katika Injili ya Luka 16, ni mungu wa uchoyo na utajiri wa dunia hii. Mammon kazi yake ni kufanya watu waliokufa kifedha na walio hai kifedha kuwa maskini wa milele ahera. Yesu Kristo alikuwa maskini, ili tuwe matajiri kupitia umaskini wake, lakini kwa sababu alikuwa na imani ya Mungu katika moyo wake alikuwa tajiri. Hivyo unaweza kuwa na utajiri wa mbinguni hapa duniani, ukiikaribisha amani ya Mungu katika moyo wako.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Hufanani na yoyote katika dunia hii. Unafanana na wewe mwenyewe. Usimdharau mtu, humjui!
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Tupo watu takriban bilioni saba katika dunia hii. Kila mtu ni wa kipekee. Mathalani, wewe ni tofauti na baba yako au mama yako au mtu mwingine yoyote yule. Kila mtu aliumbwa kivyake na Mwenyezi Mungu. Kila mtu ana nafasi ya kwake mwenyewe aliyopangiwa na Mungu hapa duniani. Haijalishi wewe ni mwanamke au mwanamume, mweupe au mweusi, mfupi au mrefu, mzuri au mbaya, una nafasi katika nchi na dunia hii. Unachotakiwa kufanya ni kuamka, kufumbua macho na kuujua ukweli. Tafuta maarifa katika Biblia kama wewe ni Mkristo. Tafuta maarifa katika Kurani kama wewe ni Mwislamu. Tafuta maarifa katika Yoga kama wewe haumwamini Mungu. Ukishaamka na kuujua ukweli, ukishapata nafasi katika nchi yako, kuwa kiongozi na mkarimu kwa wenzako. Jifunze kutoka kwa wengine ndani na nje ya tasnia yako. Usiwe mchoyo wa maarifa. Kuwa mwadilifu. Ukifanya hivyo utafanikiwa zaidi, utaipa heshima tasnia yako, na utaacha alama katika dunia baada ya kuondoka. Kuacha alama katika dunia si lazima upate nafasi katika dunia. Kuacha alama katika dunia acha alama katika nchi yako.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Katika dunia hii tunatakiwa kumwabudu Mungu peke yake. Si mtu au kitu kingine, chochote kile.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Watu wa zamani katika Agano la Kale walikuwa wakiabudu miungu iliyotengenezwa kwa mawe na vinyago. Miungu hiyo haikuwa na chochote ndani mbali na kutengenezwa kwa akili na fikira za kibinadamu. Hii ilikuwa ni kinyume cha ukweli wa Kibiblia kwamba Mungu alimuumba mtu kwa mfano wake, lakini si mtu aliyejaa dhambi kumtengeneza Mungu kwa mfano wake. Kuabudu miungu mingine ni dhambi kubwa. Tii Amri Kumi za Mungu; hasa ya kwanza, ya pili na ya tatu.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Siri ya utajiri ni mawazo ya mtu. Maisha unayoishi uliyataka mwenyewe. Amka uishi. Hii ndiyo siri kubwa ya utajiri kuliko zote ulimwenguni. Ukifikiria chanya maisha yako yatakuwa chanya, ukifikiria hasi maisha yako yatakuwa hasi. Unachofikiria ndicho unachokuwa. Siri ya mafanikio yako ni jumla ya mambo unayoyawaza.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Hii ndiyo kanuni ya nguvu ya uvutano: Kuamini = kujua! Haijalishi unamwamini Mungu au haumwamini. Kugeuza kuamini kuwa kujua si kazi rahisi hata kidogo, lakini ukigeuza kuamini kuwa kujua utafanikiwa.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Vita ya Shetani na Mungu inatuathiri zaidi sisi wanadamu – na hapo baadaye itamuathiri Shetani pia. Vita hii haiwezi kuisha hadi siku ya mwisho, Yesu Kristo atakaporudi kuwachukua wateule wake. Pambana kwa njia ya maombi hadi siku ya mwisho kwa sababu adui tunayepambana naye hana muda wa kupumzika. Pambana kujiombea na kuwaombea wengine waliohai, na hata wale ambao bado hawajazaliwa, kabla mafuta ya dunia hii hayajalipuka. Usiishi kama adui wa msalaba wa Yesu Kristo, badala yake, ishi kama rafiki wa msalaba wa Yesu Kristo. Kuishi kama rafiki wa msalaba wa Yesu Kristo ni kupinga majivuno yote ya Shetani kwa upendo uliotukuka wa kujishusha au kujidharirisha, kutokutetereka hata kidogo na tamaa za ulimwengu huu kwa upendo mkubwa wa umaskini, na kutokuyumba wakati wa matatizo kwa sababu wakati wa amani ulijilimbikizia imani.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Jambo ambalo Mungu anataka tulitambue ni kwamba hatuko wenyewe katika bahari hii ya hewa. Hata nyangumi na wazira waovu wanapozunguka huko na huko baharini, ambao pia ni mapepo, wanaochukuliwa kama viumbe wabaya na wachafu na wala mizoga, wanaishi katika bahari hii ya hewa pamoja na sisi. Ni muhimu, kwa ajili ya ustawi wetu wa kiroho, kusikia onyo la Paulo katika Waefeso 6:10-12 kwamba vita yetu si dhidi ya hawa viumbe, na wanapambana usiku na mchana kutetea kile ambacho wanaamini ni cha kwao kwa sababu ya haki ya kuwepo hapa kwanza kabla yetu. Dunia, Biblia inatwambia, ilikuwa makazi yao ya kwanza (Yuda 1:6, KJV). Wanatuchukia kwa sababu taratibu tunakuwa Baba na Mwana, na kwa sababu wanajua hii dunia, urithi wetu, itachukuliwa kutoka mikononi mwao na kukabidhiwa kwa wale ambao ni watoto wa Mungu, wale ambao ni marafiki wa msalaba wa Yesu Kristo.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Usipoangalia kwa undani sana, mapepo wanatutawala kwa sababu hatuna uwezo wa kuwaona. Aidha, wanaweza, bila hata sisi kujua, kuwasiliana nasi kimawazo na kitabia kupitia hewa hiihii inayotusaidia katika kuishi. Watu wengi katika dunia hii hawajui kama wanadanganywa au walishadanganywa tayari. Shetani na mapepo wake hawataki tujue kama wanatudanganya au wameshatudanganya tayari, na hawataki tujue kama wako hapa kwa ajili ya kutudanganya sisi. Tunajua tu kwa sababu Neno la Mungu hudhihirisha ukweli huu kupitia Roho Mtakatifu na malaika wema, na tunauamini. Licha ya hili jambo kutokea katika maisha yetu, Shetani bado anaweza kutudanganya hadi pale tutakapoerevuka kwa kiasi cha kutosha kuhakikisha kwamba udanganyifu huo hautatokea tena.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Lakini ukweli ni upi? Ukweli ni kwamba utajiri una changamoto nyingi kuupata na kuudumisha pia kuliko usomi na kwamba ukweli ni amani ya Mungu katika moyo wa mwanadamu. Heri msomi kuliko tajiri – Heri yule aliyesoma kuliko tajiri asiyesoma au yule aliyesoma kuliko vile alivyosoma tajiri au tajiri asiyesoma au aliyesoma lakini asiyekuwa na tamaa kabisa na dunia hii ambaye kukosa kwake tamaa na dunia hii kunamfanya msomi. Ndivyo Kristo anavyomaanisha. Si kwamba tajiri hawezi kuuona ufalme wa mbinguni. Ibrahimu, Isaka, Yakobo, Yusufu, Daudi, Sulemani, Yehoshafati, Hezekia, Zakayo, Yoana, Susana, na Lidia watauona ufalme wa mbinguni na walikuwa matajiri. Mali zao zilivyozidi hawakuangalia moyoni, hawakuwa na tamaa kabisa na dunia hii, bali walimtumaini Mungu kwa kila kitu walichokuwa nacho. Anaweza. Lakini asiipende dunia bali ayapende mambo ya ufalme wa Mungu kwa moyo wake wote.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Mungu anataka tujifunike kwa ngao yake. Yaani, tuwe na imani iliyokomaa katika Bwana na yeye atatufunika. Maana ya kauli hiyo ni kwamba kila kiungo cha miili yetu kuanzia unyayo hadi kichwa lazima kifunikwe kwa silaha ya Mungu, ambayo Mungu anaiita panoplia. Panoplia haimo katika kamusi ya Kiswahili au Kiingereza, lakini maana yake ni β€˜ngao kamili ya Mungu’. Hii si tu silaha ya Mungu. Ni silaha kamili ya Mungu tunayotakiwa kujifunika kwayo.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Shetani anajua kwamba sisi ni warithi wa wokovu na kwamba dunia hii ni kitu kilichoahidiwa kwa Ibrahimu na watoto wake. Sisi wote ni watoto wa Ibrahimu. Anajua kabisa kwamba baadaye sisi ndiyo tutakaokuwa watawala halisi wa dunia hii. Hivyo, anajitahidi kwa kadiri ya uwezo wake wote ili hilo lisitokee. Shetani na malaika wake ni wengi sana, na wanatumia kila silaha waliyokuwa nayo kutawala dunia.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Israeli, kama adhabu kwa uozo wake wa kiroho na kimaadili, ilivamiwa na Ashuru katika mwaka wa 721 BC na kuangushwa vibaya katika vita hiyo kubwa. Waisraeli waliosalia walitekwa na kupelekwa uhamishoni ambako inaonekana walitoweka kabisa katika uso wa dunia hii. Hili lilikuwa ni jibu la Mungu kwa dhambi na uasi wao.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Wakati Yuda ikiongozwa na kiongozi mzuri na mwenye haki kama Yosia, taifa lilistawi. Lakini ilipokuwa chini ya mwovu Manase, taifa lilisambaratika. Katika karne hii, Uingereza ilipata msukosuko mkubwa mwaka 1936 juu ya uamuzi wa Edward VIII kuoa mwanamke wa Kimarekani aliyekuwa mtalaka Wallis Simpson. Uamuzi huo ulisababisha matatizo makubwa ya kikatiba, na nusura serikali ya Uingereza ijiuzuru. Hata hivyo, kaka yake mdogo, George VI, kwa mapenzi makubwa na nchi yake, huku akikataa katakata kuondoka London wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia, aliliongoza taifa hilo katika kipindi kigumu zaidi kuliko vyote katika historia ya Uingereza. Kanuni hii ya uongozi ina ukweli katika jambo lolote kubwa na hata dogo la ujasiri.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Dunia hii ipo mahali tusipodhani ipo!
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Hata hivyo, toka mwaka 1995 watu wengi walianza kuamka kiroho dunia nzima; na mwaka 2012 waliamka zaidi, pale ulimwengu ulipoanza kuhama kutoka kwenye masafa ya ngazi ya nne ya ufahamu wa binadamu (β€˜4th dimension’) kwenda kwenye masafa ya ngazi ya tano ya ufahamu wa binadamu (β€˜5th dimension’) inayohusika zaidi na ulimwengu wa roho na ambayo bado inaendelea kuhama mpaka dakika hii. Ndiyo maana watu wengi zaidi wanamjua Mungu kipindi hiki kuliko kipindi kingine chochote kile katika historia ya dunia yetu. Kwa sababu hiyo, Shetani hatashinda.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Katika karne hii watu watawapenda zaidi marafiki kuliko ndugu.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Too Owen, wow hat's alot ov boocs how doo yu reed so meny Quot K4
”
”
Tara McMahon
β€œ
Bibi Martha Maregesi aliishi maisha mazuri sana hapa duniani. Alibarikiwa na Mungu. Aliishi miaka 84 – siku 30660 badala ya siku 25550 tulizopangiwa na Mungu. Katika uhai wake wote, kwa wale wote aliowalea, hakuna mtoto wake hata mmoja aliyefariki kabla yake. Hakuna mjukuu wake hata mmoja aliyefariki kabla yake. Hakuna kitukuu chake hata kimoja kilichofariki kabla yake. Bibi yangu ametimiza mwaka mmoja kamili leo hii, tangu amefariki dunia Novemba 4 mwaka 2014 mjini Musoma. Tunamkumbuka leo akiwa amefariki kama tulivyomkumbuka jana akiwa hai. Nguvu ya sala zetu imfanye Mwenyezi Mungu aendelee kumsamehe dhambi zake zote, na amweke mahali anapostahili, Amina.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Nguvu za hasi ni mawazo mabaya, na nguvu za chanya ni mawazo mazuri. Nguvu za hasi ni Shetani, kwa vile Shetani ndiye anayeleta mabaya. Nguvu za chanya ni Mungu, kwa vile Mungu ndiye anayeleta mazuri. Katika dunia hii utapambana na Shetani lakini hutamshinda, kwani hapa ndipo anapotawala. Pambana na Shetani katika dunia ya kiroho, kwa maana ya maombi na utiifu kamili kwa Mwenyezi Mungu, kama unataka kuzishinda nguvu zake.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Shetani ni mungu wa dunia hii kwa wale wasiomwamini Mungu. Kwa wale wanaomwamini Mungu, Mungu ndiye Mungu wa dunia hii.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Hakuna maana yoyote kupambana na Shetani katika dunia hii ambapo yeye ndiye mtawala. Pambana na Shetani katika dunia ya kiroho ambapo Shetani hana nguvu yoyote dhidi ya Yesu Kristo.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Kutakuwepo na nguvu za hasi na chanya katika maisha yako kadiri utakavyoishi hapa duniani. Ukiruhusu mwili wako utawaliwe na hasi utakuwa hasi. Ukiruhusu mwili wako utawaliwe na chanya utakuwa chanya. Shetani hawezi kuona ndani ya moyo wako hadi wewe wenyewe umwonyeshe. Ukionyesha tamaa ya uzinzi atakupa uzinzi. Ukionyesha tamaa ya ulevi atakupa ulevi. Ukionyesha tamaa ya wizi atakupa wizi, na kadhalika. Kadiri utavyojitahidi kuwa chanya ndivyo utakavyozidi kuwa chanya; na kadiri utavyojitahidi kuwa hasi ndivyo utakavyozidi kuwa hasi. Usipambane na Shetani katika dunia hii ambapo yeye ndiye mtawala. Pambana na Shetani katika dunia ya kiroho ambapo Shetani hana nguvu yoyote dhidi ya Yesu Kristo.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
XM29 OICW ni bunduki iliyowasaidia Vijana wa Tume kubomoa jengo la utawala la Kolonia Santita katika Kiwanda cha Dongyang Pharmaceuticals jijini Mexico City, iliyowasaidia kukamata baadhi ya wakurugenzi wa Kolonia Santita kabla hawajatoroshwa na walinzi wao makomandoo. Bunduki hii inayotumia teknolojia ya OICW ('Objective Individual Combat Weapon') iliyotengenezwa na Kiwanda cha Heckler & Koch cha Ujerumani, ina uwezo wa kufyatua makombora ya HEAB ('High Explosive Air Bursting') yenye ukubwa wa milimeta 20; ambayo hulipuka hewani kabla ya kugonga shabaha, kwa lengo la kusambaza vyuma vya moto katika eneo lote walipojificha maadui. Bunduki hizi hazitumiki tena. Zilitumika mara ya mwisho mwaka 2004.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Kuwepo kwa Mti wa Uzima wa Milele katika Bustani ya Edeni (pamoja) na Mti wa Maarifa ya Mema na Mabaya inamaanisha, Adamu na Hawa walikuwa hai kiroho mpaka walipokula tunda la mti wa katikati ambapo hali yao ya maisha ilibadilika. Adamu na Hawa walikufa lakini hawakufa – walikufa baadaye kabisa. Hii inamaanisha kwamba (haya ni mawazo yangu tu) mtu anapokufa anakuwa amekula tunda la mti wa katikati, litakalomwezesha kuendelea kuishi katika hali nyingine ya maisha ambayo sisi hatuijui.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Wanasayansi wanaamini kuwa Yesu atarudi tarehe 29 Julai 2016. Tarehe hiyo kitu kikubwa sana kitatokea katika dunia yetu kitakachosababisha tetemeko kubwa la ardhi, litakalosababishwa na kubadilika kwa ncha za dunia, tendo litakalosababisha mionzi ya gama kutoka kwenye jua ifike duniani na kuua kila kitu kinachoonekana katika uso wa dunia hii. Watakatifu watafufuka na kumlaki Kristo mawinguni, ambaye anakuja kuwachukua wateule na kumweka Shetani kifungoni kwa miaka 1000. Hayo yote, wanasema, yatatokea ndani ya siku 11 kuanzia leo. Yaani, kusini mwa dunia kutakuwa kaskazini mwa dunia, kaskazini mwa dunia kutakuwa kusini mwa dunia. Kitendo hicho kitafanya dunia ikose kinga ya sumaku iitwayo β€˜magnetosphere’ ambayo hukinga dunia dhidi ya mionzi ya gama kutoka kwenye jua. Mionzi hiyo hugonga ukuta wa β€˜magnetosphere’ kila baada ya dakika 8 kwa mwendokasi wa kilometa milioni 1080 kwa saa; na kusambazwa katika ncha za dunia ambapo aghalabu huchanganyikana na oksijeni na kutengeneza kitu kinaitwa β€˜aurora’, au mwanga wa ncha, ambacho ni maajabu mengine ya angani. Mwaka 2012 wanasayansi walisema ncha za dunia zingebadilika lakini hazikubadilika. Je, muda umefika sasa wa kuwaamini wanasayansi? Biblia ni chuo cha Mungu. Soma Biblia kupata maarifa.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Kabla ya kukata roho mapigo ya kasi ya moyo aliyoyapata Yesu kutokana na mshtuko wa hipovolimia, pia yalisababisha maji kujikusanya katika vifuko vya maji au ute kandokando ya moyo na kandokando ya mapafu. Mkusanyiko huu wa maji kandokando ya moyo hujulikana kama β€˜pericardial effusion’ na mkusanyiko wa maji kandokando ya mapafu hujulikana kama β€˜pleural effusion’. Hii ndiyo maana baada ya Yesu kukata roho, na askari wa Kirumi kurusha mkuki katika ubavu wake, baada ya kutoboa mapafu na moyo, damu na maji vilitoka katika mbavu za Yesu kama Yohana alivyorekodi katika Injili yake. Mapafu ya Yesu na tumbo la Yesu vilijaa damu na maji. Mkuki ulivyotupwa maji yalitoka katika mapafu ya Yesu na katika tumbo la Yesu, na katika utando unaozunguka moyo wa Yesu, kutokana na kupasuka kwa moyo.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Kilio kikuu cha Yesu, β€œEloi, Eloi, lama sabakthani?”, yaani, β€œMungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?”, na β€œImekwisha”, vilitabiriwa katika Zaburi 22 ili watu waliompinga Kristo waamini kama Yesu alikuwa Masihi. Zaburi 22 ulikuwa wimbo maarufu katika kipindi cha karne ya kwanza, kipindi ambacho Yesu alizaliwa na kufa, uliotungwa na mfalme Daudi, ulioitwa β€˜zaburi ya mateso na matumaini ya mwadilifu’. Kwa hiyo Yesu aliposema maneno hayo yaliwaingia watu akilini, na kuanzia hapo imani hasa ya Ukristo ikachukua kasi hadi leo hii. Zaburi 22 inaanza na β€œMungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?” na inaisha na β€œImekwisha”, miongoni mwa maneno saba aliyoyasema Yesu pale msalabani Golgotha. Kwa hiyo, Zaburi 22 ni utabiri wa kifo cha Yesu.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Hii ni muhimu sana kwa Pasaka. Si tu kwamba Pasaka ni tamasha linalojitegemea, lakini kadhalika linatumika kama siku ya maandalizi kwa ajili ya siku takatifu, siku ya kwanza ya Sikukuu ya Mkate Usiotiwa Chachu. Kwa mujibu wa hesabu za kalenda ya Kihebrania, Pasaka inaweza kuangukia siku ya Jumatatu, Jumatano, Ijumaa au Sabato.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Kamwe usikubali kuwa mvivu, wala usikubali kuwa mlaodikia. Usikubali starehe za dunia hii kuwa kikwazo cha maendeleo yako ya kiroho ya kadari ya maisha yako. Palilia bustani yako ya kiroho, kuondoa magugu ambayo ni raha za dunia hii.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Mbegu zilizopandwa kwenye udongo wenye rutuba ni rahisi sana kuvamiwa na magugu iwapo mwenye bustani hataipalilia bustani yake kila siku. Kila siku tunapaswa kupalilia bustani zetu za kiroho, kuondoa magugu ambayo ni raha za dunia hii.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Mlaodikia ni mtu anayejua kwamba bustani yake ina magugu lakini anaona uvivu kwenda kuipalilia. Kinachofanya aone uvivu kwenda kuipalilia ni raha za dunia hii. Usiwe vuguvugu. Kama umeamua kuwa moto kuwa moto. Kama umeamua kuwa baridi kuwa baridi.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Maisha ni kitu cha ajabu kuliko vyote ulimwenguni kilichowashangaza hata wanasayansi wa dunia hii. Amka na uujue ukweli.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Watoto wadogo wanakufa. Watu wazima wasiokuwa na hatia wanakufa vitani na katika majanga mengine ya asili. Kwa nini? Watoto wadogo wanaokufa walikuja duniani kufanya nini? Kwa nini watu wasiokuwa na hatia wanakufa ilhali Mungu yupo na asiwaepushe na matatizo ya dunia hii? Kama aliweza kuzuia binadamu wasiishi majini kwa sababu watakufa kwa nini asizuie matatizo yasiwapate watoto na watu wazima wasiokuwa na hatia? Sisi ni wadogo sana na Mungu ni mkubwa mno. Jibu hatutaweza kulielewa pamoja na kwamba tumepewa. Hata hivyo, Mungu hababaishwi na mwili. Anababaishwa na roho.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Adamu na Hawa walipotenda dhambi waligundua kuwa kumbe walikuwa na miili, walipogundua kuwa walikuwa uchi, kisha Mungu akawalaani. Miili yao ikakosa thamani mbele ya Mungu, sisi wote tukalaaniwa pamoja nao. Kwa Mungu hii miili haina thamani hata kidogo. Chenye thamani ni roho.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Mungu angekuwa anababaishwa na mwili asingeruhusu Shetani autese mwili wa Ayubu kiasi chote kile isipokuwa roho yake, wala tusingekuwa tunateseka, wala watoto wadogo wasingekuwa wanakufa, wala watu wasiokuwa na hatia wasingekuwa wanakufa vitani au katika majanga mengine yoyote yale katika dunia hii.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Sina jinsi. Nguzo ya maisha yangu ni historia ya maisha yangu. Historia ya maisha yangu ni urithi wa watu waliojifunza kusema hapana kwa ndiyo nyingi – waliojitolea vitu vingi katika maisha yao kunifikisha hapa nilipo leo – walionifundisha falsafa ya kushindwa si hiari. Siri ya mafanikio yangu ni kujitahidi kwa kadiri ya uwezo wangu wote. Hiyo wote katika herufi kubwa. Wote katika herufi kubwa (WOTE) si neno la kawaida falau katika nukuu hii ya mafanikio. Linamaanisha kujitahidi kwa kadiri ya uwezo wako wote uliopewa na Mwenyezi Mungu. Watu wengi hujitahidi kwa kadiri ya uwezo wao. Usijitahidi kwa kadiri ya uwezo wako. Jitahidi kwa kadiri ya uwezo wako WOTE.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Umri sahihi wa kuoa au kuolewa kulingana na kanuni ya ndoa iitwayo β€˜optimal stopping’ ni miaka 26. Kanuni hii ya hesabu hujulikana kama kanuni ya asilimia 37, welekeo wa 0.37 wa kumpata mwenza bora zaidi katika maisha yako kuliko wengine wote.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Lakini kanuni hii (β€˜optimal stopping’) ina walakini. Kwa mfano utajuaje watu au wapenzi utakaotembea nao au kuachana nao katika kipindi chote cha maisha yako? Au itakuaje kama mpenzi wako wa kwanza uliyemwacha ndiye yule ambaye Mungu alikupangia kuwa naye maishani?
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Yesu Kristo wa Nazarethi ni mtu mashuhuri zaidi kuliko wote kuwahi kukanyaga ardhi ya dunia hii. Alikufa majira ya saa 9 kamili za mchana, siku ya Jumatano, katika kipindi cha demani cha AD 31. Saa chache baadaye, jua lilipokuwa likizama, alilazwa katika kaburi jipya la Yusufu wa Arimathaya. Katika siku ya kawaida ya Sabato, Jumamosi, siku tatu kamili baada ya mazishi yake, Mungu Baba alimfufua Mtoto Wake kwa ajili ya uzima wa milele.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Dunia hii ina watu ambao Mungu anataka kuwaokoa, lakini inafanya wawe wagumu kwelikweli.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Kwa sababu ya kutofautiana kati ya Mungu na ulimwengu huu, dunia hii haiwezi kuwa dunia ambayo Mungu alijitolea Mwanawe wa pekee.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Nimeishi na watu kutoka katika mabara yote ya dunia hii. Wanaume wana asili yao na wanawake wana asili yao. Ndiyo maana katika upendo wa PHILADELPHIA, upendo wa wanachama wa mashirika ya siri, wanaume na wanawake hawachangamani.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Hakuna maana yoyote kupambana na Shetani katika dunia hii ambapo yeye ndiye mtawala. Pambana na Shetani katika dunia ya kiroho ambapo Shetani hana nguvu yoyote mbele ya Yesu Kristo.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Unaruhusiwa kutokubaliana na wengine, sema maoni yako kwa heshima lakini usiwe na kimwili au vurugu. Mbinu hii inatufanya tofauti na wanyama! Kwa hiyo ustaarabu, sikiliza kile wengine wanachosema lakini uepuka athari za magoti. Ingekuokoa kutoka kwa majuto mengi!
”
”
David Shamala