Mwanamke Quotes

We've searched our database for all the quotes and captions related to Mwanamke. Here they are! All 25 of them:

β€œ
Ukikosana na mwanamke usimpige mchana. Mpige usiku. Ukimpiga mchana watu watasema umemwonea. Ukimpiga usiku watu watasema huenda alikuwa na makosa. Wanawake hawatakiwi kupigwa.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Ukitaka kumjua mwanamke jua historia yake.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Tabia ya mwanamke mwema inapaswa kufichwa ndani ya Kristo ili mwanamume anayemtaka huyo mwanamke amtafute ndani Kristo kwanza, ili kukutana naye.
”
”
Wilson M. Mukama
β€œ
Mwaka mmoja na nusu unatosha kumjua mwanamke kabla ya ndoa. Miezi sita itakufanya ujue kama mwanamke anaweza kuwa mchumba. Mwaka mmoja na nusu utakufanya ujue kama mwanamke anaweza kuwa mke.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Mungu alikupa maisha akakupa akili ili utambue jema na baya na akakupa amri zake ili uishi kwa amani na upendo. Kama Mungu hayupo mwanamume na mwanamke walitoka wapi? Wazazi wako walitoka wapi? Wazazi wao walitoka wapi? Wazazi wao walitoka wapi?
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Kama unataka kuijua vizuri historia ya mwanamke hasa mwanamke unayetaka kuoana naye, usifanye naye mapenzi kwa miezi sita angalau. Ukifanya naye mapenzi kwa miezi sita au zaidi, au ndani ya miezi sita, halafu akakuchanganya kimapenzi, hutakuwa na uwezo mkubwa wa kuwasikiliza watu kuhusiana na historia yake.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Lakini damu na maji vina maana kubwa katika maisha yetu. Biblia inaeleza kuwa wakati Yesu Kristo akiwa msalabani alichomwa ubavu wake kwa mkuki, ikatoka damu na maji, ndipo zilipozaliwa sakramenti za kanisa. Aidha, tukio la askari wa Kirumi kumchoma Yesu na damu na maji kutoka lina maana nyingine kubwa katika maisha yetu. Hapo ndipo Ukristo ulipozaliwa; na ni kwa sababu hiyo mwanamke anapojifungua hutoa damu na maji kutokana na kupasuka kwa utando wa mfuko wa uzazi. Kutokana na hayo, Wakristo wanapoabudu msalaba wanaeleza umuhimu wa matukio na mafundisho waliyopata kupitia mateso aliyopata kiongozi wao na kuwa, msalaba ni chombo cha ukombozi.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Ikiwa huna pesa na una mke na watoto kwa mfano, mke wako (wanawake walio wengi) hatakuona wa maana kwa sababu ya ustawi wa maisha ya familia yake. Ikiwa una mwanamke asiyekuwa na busara au hekima ya kutosha, au mwanamke ambaye akili zake zimefyatuka kidogo, atakusaliti kutafuta bwana au mtu mwenye maana. Kama huna pesa huna maana kwa mwanamke.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Hakuna mtu mwenye akili timamu anayetaka mabaya katika maisha yake. Mwanamume atake mwanamke mwenye matendo mema. Mwanamke atake mwanamume mwenye matendo mema. Misingi ya hasanati ni misingi ya utu. Tukiishi katika misingi ya utu, misingi ya matendo mema, tutaishi sawasawa na mapenzi ya Mungu. Kila mtu anapaswa kuishi na mke au mume aliye mwema.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Jina langu ni Enock Maregesi na ningependa kukwambia kisa kidogo kuhusiana na bibi yangu, Martha Maregesi. Mwanamke huyu alikuwa mke mwenye upendo usiokuwa na masharti yoyote. Alikuwa mama na bibi aliyefundisha familia yake umuhimu wa kujitolea na umuhimu wa uvumilivu. Ijapokuwa hakupendelea sana kujizungumzia mwenyewe, ningependa kukusimulia kisa kidogo kuhusiana na hadithi ya maisha ya mwanamke huyu wa ajabu katika maisha yangu. Bibi yangu alizaliwa katika Kitongoji cha Butimba, Kijiji cha Kome, Kata ya Bwasi, Tarafa ya Nyanja (Majita), Wilaya ya Musoma Vijijini, Mkoa wa Mara, katika familia ya watoto kumi, mwaka 1930. Alisoma katika Shule ya Msingi ya Kome ambako alipata elimu ya awali na msingi na pia elimu ya kiroho kwani shule yao ilikuwa ya madhehebu ya Kisabato. Aliolewa na Bwana Maregesi Musyangi Sabi mwaka 1946, na kufanikiwa kupata watoto watatu; wa kiume wakiwa wawili na wa kike mmoja. Matatizo hasa ya bibi yalianza mwaka 2005, alipougua kiharusi akiwa nyumbani kwake huko Musoma. Hata hivyo alitibiwa hapo Musoma na Dar es Salaam akapona na kuwa mwenye afya ya kawaida. Lakini tarehe 19/10/2014 alipatwa tena na kiharusi na kulazwa tena katika Hospitali ya Mkoa ya Musoma, ila akajisikia nafuu na kuruhusiwa kurudi nyumbani – lakini kwa maagizo ya daktari ya kuendelea na dawa akiwa nje ya hospitali. Tarehe 29/10/2014 alirudi tena Hospitali ya Mkoa ya Musoma kwa tiba zaidi, lakini tarehe 4/11/2014 saa 7:55 usiku akafariki dunia; akiwa amezungukwa na familia yake. Dunia ina watu wachache sana wenye matumaini na misimamo ya kutegemea mazuri, na wachache zaidi ambao wako tayari kugawa matumaini na misimamo hiyo kwa watu wengine. Nitajisikia furaha siku zote kwamba miongoni mwa watu hao wachache, hata bibi yangu alikuwemo. Msalaba uliwekwa wakfu na Mwenyezi Mungu baada ya mwili wa Yesu Kristo kuning’inizwa juu yake. Kwa kuwa bibi yangu ametanguliwa na msalaba, msalaba utamwongoza mahali pa kwenda.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Nusu dakika baada ya kuondoa gari, Murphy aliona kiwiliwili cha mtu kikimwendea mbio kutokea katika nyumba ya magaidi! Hapohapo alisimamisha gari na kuacha taa zikiwaka, halafu akashika bunduki na kushuka – akiwa ameangalia mbele kwa tahadhari kubwa. Alikuwa mwanamke. Debbie! Murphy alipojua ni Debbie, alitupa bunduki na kuchomoka mbio mpaka wakakutana na kukumbatiana kwa nguvu! Murphy alimbeba Debbie na kumbusu kila sehemu, halafu akamfuta machozi na kumbembeleza.
”
”
Enock Maregesi (Kolonia Santita)
β€œ
Badilisha tabia. Badilisha mazingira ya maisha yako. Haijalishi una umri kiasi gani au wewe ni mwanamke au mwanamume, bado hujachelewa kubadili maisha yako kutoka duni kuwa bora – kuwa na amani, furaha na kuridhika. Kama desturi yako ni kuamka saa 12:00 asubuhi kila siku ili ufike kazini saa 2:00 asubuhi ambao ni muda wa serikali wa kuanza kazi, amka saa 11:30 asubuhi ili ufike kazini saa 1:30 asubuhi – nusu saa kabla ya kuanza kazi. Kama unafanya kazi ya taaluma uliyosomea lakini maisha hayaendi, fikiria kubadili mwelekeo wa maisha ikiwemo taaluma kufikia malengo uliyojiwekea.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Mwanamume kutokana na asili yake atampenda mwanamke hata kama hataonyesha hisia zake kwake. Ukiwaweka pamoja, mwanamume na mwanamke, mwanamume hatafikiri sawasawa.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Mwanamume hataweza kumwelewa mwanamke na mwanamke hataweza kumwelewa mwanamume. Kwa sababu asili zetu ni tofauti.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Wakati Yuda ikiongozwa na kiongozi mzuri na mwenye haki kama Yosia, taifa lilistawi. Lakini ilipokuwa chini ya mwovu Manase, taifa lilisambaratika. Katika karne hii, Uingereza ilipata msukosuko mkubwa mwaka 1936 juu ya uamuzi wa Edward VIII kuoa mwanamke wa Kimarekani aliyekuwa mtalaka Wallis Simpson. Uamuzi huo ulisababisha matatizo makubwa ya kikatiba, na nusura serikali ya Uingereza ijiuzuru. Hata hivyo, kaka yake mdogo, George VI, kwa mapenzi makubwa na nchi yake, huku akikataa katakata kuondoka London wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia, aliliongoza taifa hilo katika kipindi kigumu zaidi kuliko vyote katika historia ya Uingereza. Kanuni hii ya uongozi ina ukweli katika jambo lolote kubwa na hata dogo la ujasiri.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Mwanamke mwenye umri wa miaka arobaini na mbili na kuendelea anafaa kuolewa kama ni mjane na ataweza kuwapenda watoto wako kama mama yao alishafariki. Yule ambaye hajawahi kuolewa au aliyewahi kuolewa lakini akaachika bado ni kubahatisha, kwa sababu hujui kwa nini hajaolewa au kwa nini aliachika, hata kama ana watoto.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Tupo watu takriban bilioni saba katika dunia hii. Kila mtu ni wa kipekee. Mathalani, wewe ni tofauti na baba yako au mama yako au mtu mwingine yoyote yule. Kila mtu aliumbwa kivyake na Mwenyezi Mungu. Kila mtu ana nafasi ya kwake mwenyewe aliyopangiwa na Mungu hapa duniani. Haijalishi wewe ni mwanamke au mwanamume, mweupe au mweusi, mfupi au mrefu, mzuri au mbaya, una nafasi katika nchi na dunia hii. Unachotakiwa kufanya ni kuamka, kufumbua macho na kuujua ukweli. Tafuta maarifa katika Biblia kama wewe ni Mkristo. Tafuta maarifa katika Kurani kama wewe ni Mwislamu. Tafuta maarifa katika Yoga kama wewe haumwamini Mungu. Ukishaamka na kuujua ukweli, ukishapata nafasi katika nchi yako, kuwa kiongozi na mkarimu kwa wenzako. Jifunze kutoka kwa wengine ndani na nje ya tasnia yako. Usiwe mchoyo wa maarifa. Kuwa mwadilifu. Ukifanya hivyo utafanikiwa zaidi, utaipa heshima tasnia yako, na utaacha alama katika dunia baada ya kuondoka. Kuacha alama katika dunia si lazima upate nafasi katika dunia. Kuacha alama katika dunia acha alama katika nchi yako.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Kwa mwanamke wa kuoa natafuta hasanati. Akiwa mbaya atakuwa mzuri. Akiwa maskini atakuwa tajiri. Akiwa gumbaru atakuwa msomi. Akiwa mshamba atakuwa mjanja. Akiwa mjinga atapata maarifa. Nitampenda zaidi kwa mazuri kuliko mabaya.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Sina nyemi na mwanamke mwenye sura nzuri na tabia mbaya. Nina nyemi na mwanamke mwenye sura mbaya na tabia nzuri, au mwanamke mwenye sura nzuri na tabia nzuri. Mwanamke wa kuoa sitampenda nitampendelea.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Natafuta mwanamke mwenye utu, wema, uaminifu na tabia njema – sifa ambazo ataendelea kuwa nazo hata uzeeni. Sifa hizi zinaweza kubadilika kwa sababu ya maisha au kwa sababu ya mapenzi ya Mungu, lakini mabadiliko haya hayatakuwepo kwa haraka. Sura haidumu. Tabia hudumu.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Stress za mwanamke kuingia kwenye ndoa ni kubwa kuliko mwanaume ndo sababu hata Vitabu vinaonesha mwanaume ni kiongozi lakini mjini kiongozi ni hela
”
”
Chrisper Malamsha
β€œ
Murphy alichanganyikiwa. Hakujua nini kilitokea na kwa nini. Ila, ghafla, alipotupa macho kushoto aliona kitu. Joka kubwa lilitambaa, ingawa kwa shida, kwa sababu ya sakafu, na kumfuata kummaliza. Murphy alijua joka hata angefanya vipi, hakuwa na uwezo wa kujikinga. Alipotaka kupiga kelele ili walinzi wa nje waje, Murphy alishindwa. Nyuma ya joka – katika mkia – kuna kitu kiling’aa, kikamshangaza! Muujiza ulimtokea Murphy lakini kitu kikamwambia aite walinzi wa nje ili waje wamuue yule nyoka. Lakini kabla hajapiga kelele, alisikia sauti; si ya mwanamume. Ya mwanamke!
”
”
Enock Maregesi (Kolonia Santita)
β€œ
Wachawi hivi ndivyo wanavyoapishwa na kuikana imani ya Kikristo: Mwanafunzi hupelekwa kilingeni katika siku maalumu kuonana na Shetani, pamoja na jopo la wachawi. Shetani hutokea katika mwili wa hewa, mwili uliochanganyikana na hewa na mvuke mzito, wa mwanamume na kuwasihi waishikilie imani yao kwake kwa mioyo yao yote, huku akiwaahidi utajiri na maisha marefu kama hawatamkana. Kisha wachawi wanampendekeza mwanafunzi kwa Shetani. Shetani humuuliza mwanafunzi kama yuko tayari kuikana imani yake, kuachana na Ukristo na kutokumwabudu Mwanamke Aliyebarikiwa Kuliko Wanawake Wote Duniani Maria Magdalena, na kutoziheshimu sakaramenti za aina zote. Mwanafunzi atakapokubaliana na masharti hayo, Shetani atanyoosha mkono wake na kumsihi mwanafunzi anyooshe wa kwake. Kwa mkono wake mwenyewe, mwanafunzi ataapa na kuweka agano na Shetani mbele ya jopo la wachawi. Baada ya hapo bila kuchelewa Shetani ataendelea na kusema kuwa hicho kiapo hakitoshi. Lakini mwanafunzi atakapouliza afanye kitu gani cha ziada, Shetani atahitaji kiapo kifuatacho kwa heshima yake na kwa heshima ya mashetani wote: Mwanafunzi ajikabidhi kwa Shetani kwa mwili na kwa roho yake yote daima dawamu, na afanye kila awezalo kuleta wanafunzi wengine wa kike na wa kiume katika ufalme wake. Kama hiyo haitoshi Shetani ataongeza kuwa lazima mwanafunzi atengeneze mafuta fulani kutokana na mifupa na viungo vya miili ya watoto, hasa watoto waliobatizwa, kwani kwa kufanya hivyo atamtimizia kila kitu atakachokitaka hapa duniani. Hiyo ni njia mojawapo ya kiapo. Njia nyingine ya kiapo ni kwa wale ambao hawajiamini au wana hofu ya kuonana na Shetani uso kwa uso kilingeni, akiwa na mwili wa kimazingaombwe na sauti ya kutisha kwani Shetani hana mapafu wala hana ulimi. Badala ya kilingeni mwanafunzi hupelekwa kanisani na jopo la wachawi ambapo mbele ya jopo atalazimishwa kuikana imani yake, kumkana Yesu Kristo, kuukana ubatizo na kulikana kanisa zima kwa ujumla wake. Mwanafunzi baada ya hapo atalazimishwa kutoa heshima kuu kwa Mfalme Mdogo, kwani hivyo ndivyo wanavyomwita Shetani ili kumwondolea mwanafunzi hofu, kisha atalazimishwa kunywa supu ya mtoto mchanga waliyemuua akazikwa kisha wakamfukua na kupika viungo vya mwili wake; na dakika hiyo mwanafunzi atapata maarifa, maarifa ya kichawi, kama walimu wake na watarudi nyumbani.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Mwanamke akikuomba pesa, mpe!
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Mwanamke anapenda mazoea!
”
”
Enock Maregesi