Mimi Siku Quotes

We've searched our database for all the quotes and captions related to Mimi Siku. Here they are! All 3 of them:

Adam Kuambiana umerudi nyumbani ulikotoka, ukiongozwa na imani na mwanga wa wale uliowapenda na kuwapoteza. Hatuwezi kukumbuka kwamba umetutoka bila kukumbuka kwamba uliishi, na kwamba maisha yako yalitupa kumbukumbu nzuri tusizoweza kuzisahau haraka. Jumanne, siku ya kuuaga mwili uliokuwa ukitumiwa na wewe, wengine watasema Kwa heri lakini mimi nitasema Asante! Asante kwa sababu ya kipaji chako. Asante kwa sababu ya kujitahidi kwa kadiri ya uwezo wako wote, kutoa sauti kwa wale wote waliokuwa hawawezi kusikika. Asante kwa sababu ya kuacha dunia katika hali nzuri kuliko ulivyoikuta wakati ukiingia, na Asante kwa sababu ya maisha yako. Tukiendelea kuomboleza kifo cha Adam Kuambiana hapa duniani, wengine wanasherehekea kukutana naye huko mbinguni. Mchungaji wa uhai wa wote Mungu wa mbinguni ailaze roho yake mahali pema peponi: Yeye ni mwandishi wa hadithi ya maisha yetu na ndiye aliyeandika ukurasa wa mwisho wa hadithi ya Adam.
Enock Maregesi
Taabini hii ni ngumu sana kwangu kuandika pamoja na kwamba ni miaka mitatu kamili toka giza liingie. Mwaka 2014, Novemba 4, nilimpoteza bibi yangu mpendwa, Martha Maregesi, aliyefariki dunia kutokana na ukongo wa kiharusi, na tutamkumbuka daima. Alikuwa na roho ya kipekee; na kifo chake kiliwagusa wengi, pamoja na kwamba aliishi maisha kamili, zaidi ya siku 25550, siku 5110 zaidi, ambazo ndizo tulizopangiwa na Mungu. Mapenzi ya mtu kwa bibi yake ni mapenzi ya kipekee. Nadhani Mungu aliwapa mabibi wote uwezo maalumu wa kuwapenda wajukuu zao, na kufanya maisha yao yatimie, kuwafanya wawe binadamu wazuri na wenye maadili mema. Alichangia pakubwa katika malezi yangu ya utotoni; na aghalabu naweza kukumbuka nikiwa naye jikoni akipika, huku mimi nikifanya kazi nyingine, lakini wakati huohuo akinifundisha mambo kadha wa kadha ya kunikomaza kimaisha. Bibi hakuwa tu bibi. Alikuwa mlezi, rafiki na mtu aliyenihamasisha sana katika maisha. Kifo kinaleta huzuni lakini kinaleta tumaini. Naamini bibi yangu atakwenda mbinguni, kwa sababu naamini alitubu dhambi zake akisaidiwa na wachungaji. Wachungaji hao walimtembelea kila siku, nyumbani au hospitalini, akiwa kitandani kwake akiugua. Bibi yangu alitimiza wajibu wake. Alizaliwa, aliishi, na alikufa katika toba. Siku nitakapokufa ningependa kuzikwa jirani na alipozikwa bibi yangu, ili Yesu atakaporudi tufufuke pamoja.
Enock Maregesi
Biblia inatuambia kuwa tuombe bila kukoma. Lakini tutaombaje bila kukoma? Njia mojawapo ya kufanya hivyo ni kutumia ‘maombi ya pumzi’ kila siku kama ambavyo Wakristo wengi wamekuwa wakifanya kwa karne nyingi. Unachagua sentensi fupi au maneno rahisi kuhusu Yesu unayoweza kuyasema na kuyarudia kimoyomoyo kila siku katika kila pumzi inayoingia na kutoka ndani ya mapafu yako! Kwa mfano: “Asante Yesu.” “U pamoja nami.” “Nataka kukujua.” “Napokea neema yako.” “Nakutegemea wewe.” “Mimi ni wako.” “Nisaidie nikuamini.” “U Mungu wangu.” “Naishi kwa ajili yako.” “Nisamehe dhambi zangu zote.” Fundisha akili yako kumkumbuka Mungu kila wakati.
Enock Maregesi