Kufa Quotes

We've searched our database for all the quotes and captions related to Kufa. Here they are! All 35 of them:

Kusaliti nchi, ambayo majeshi ya ulinzi na usalama yameundwa kuilinda, ni miongoni mwa makosa makubwa kabisa kuweza kufanywa na mtu! Adhabu yake ni kifungo cha maisha jela, au kunyongwa hadi kufa.
Enock Maregesi
Kitu cha kwanza kufanyika mwanadamu anapozaliwa ni kuvuta pumzi ya kwanza katika mapafu ya mwili wake. Cha mwisho kufanyika kabla ya kufa ni kutoa pumzi ya mwisho katika mapafu ya mwili wake. Pumzi iliyoingia kwanza baada ya kuzaliwa, itakuwa ya mwisho kutoka kabla ya kufa. Pumzi ni bora kuliko muda halafu pumzi ni uhai. Bila uhai watu hawataweza kusherehekea mwaka mpya au kufanya chochote. Likumbuke jina la Mwenyezi Mungu katika kila pumzi unayoingiza na kutoa.
Enock Maregesi
Mama anaweza kufa ili mwanawe aishi, anaweza kufunga na kuomba ili mwanawe Mungu amsaidie ashinde mtihani wake, anaweza kulala njaa ili mwanawe ale, anaweza kujitolea vitu vingi au mambo mengi katika maisha yake ili mwanawe aishi vizuri, anaweza kuingia dhambini ili mwanawe asamehewe.
Enock Maregesi
Ujanja wote ulimwisha Murphy. Ilimbidi kutoboa siri ili adui asizidi kumuumiza. Alilaumu mno kufa wakati alishakula ng’ombe mzima. Alifikiri Mogens na Yehuda walishauwawa kulingana na hasira nyingi za magaidi. Walihakikisha hawafanyi makosa hata kidogo. Alivyomaliza kumhoji, yule adui alizunguka nyuma katika mgongo wa Murphy na kwenda katika dirisha lililokuwa wazi – la mashariki – ambapo aliegemea na kuvuta sigara. Alichungulia kidogo nje kisha akageuka na kuendelea kupata upepo mdogo wa baridi.
Enock Maregesi (Kolonia Santita)
Akili yangu itakaponipeleka kwa mgonjwa hospitalini halafu sekunde hiyohiyo jicho langu likacheza au kiungo changu chochote cha mwili kikauma na kuacha ghafla ‘bila’ sababu yoyote, najua kile ninachokifikiria kuhusu mgonjwa huyo ama kitatokea au hakitatokea. Nikifikiria amepona, halafu ghafla kichwa kikaniuma na kuacha, kitakuwa kinyume chake. Yaani, hatapona. Nikifikiria amekufa, halafu ghafla kichwa au kiungo kingine chochote kikaniuma na kuacha, kitakuwa kinyume chake pia. Yaani, hatakufa. Hivyo, nikifikiria amepona, nikifikiria amekufa, na kichwa kikaniuma na kuacha, sekunde hiyohiyo natakiwa kumwombea mgonjwa huyo. Kama ni kupona, apone kama Mungu alivyokusudia; na kama ni kufa, afe kama Mungu alivyokusudia. Si kama Shetani alivyokusudia.
Enock Maregesi
Biblia pamoja na historia vinatwambia kuwa mitume kumi na wawili wa Yesu Kristo waliamua kufa kinyama kama mfalme wao alivyokufa, kwa sababu walikataa kukana imani yao juu ya Yesu Kristo. Mathayo alikufa kwa ajili ya Ukristo nchini Ethiopia kwa jeraha lililotokana na kisu kikali, Marko akavutwa na farasi katika mitaa ya Alexandria nchini Misri mpaka akafa, kwa sababu alikataa kukana jina la Yesu Kristo. Luka alinyongwa nchini Ugiriki kwa sababu ya kuhubiri Injili ya Yesu Kristo katika nchi ambapo watu hawakumtambua Yesu. Yohana alichemshwa katika pipa la mafuta ya moto katika kipindi cha mateso makubwa ya Wakristo nchini Roma, lakini kimiujiza akaponea chupuchupu, kabla ya kufungwa katika gereza la kisiwa cha Patmo (Ugiriki) ambapo ndipo alipoandika kitabu cha Ufunuo. Mtume Yohana baadaye aliachiwa huru na kurudi Uturuki, ambapo alimtumikia Bwana kama Askofu wa Edessa. Alikufa kwa uzee, akiwa mtume pekee aliyekufa kwa amani. Petro alisulubiwa kichwa chini miguu juu katika msalaba wa umbo la X kulingana na desturi za kikanisa za kipindi hicho, kwa sababu aliwaambia maadui zake ya kuwa alijisikia vibaya kufa kama alivyokufa mfalme wake Yesu Kristo. Yakobo ndugu yake na Yesu (Yakobo Mkubwa), kiongozi wa kanisa mjini Yerusalemu, alirushwa kutoka juu ya mnara wa kusini-mashariki wa hekalu aliloliongoza la Hekalu Takatifu (zaidi ya futi mia moja kwenda chini) na baadaye kupigwa kwa virungu mpaka akafa, alipokataa kukana imani yake juu ya Yesu Kristo. Yakobo mwana wa Zebedayo (Yakobo Mdogo) alikuwa mvuvi kabla Yesu Kristo hajamwita kuwa mchungaji wa Injili yake. Kama kiongozi wa kanisa hatimaye, Yakobo aliuwawa kwa kukatwa kichwa mjini Yerusalemu. Afisa wa Kirumi aliyemlinda Yakobo alishangaa sana jinsi Yakobo alivyolinda imani yake siku kesi yake iliposomwa. Baadaye afisa huyo alimsogelea Yakobo katika eneo la mauti. Nafsi yake ilipomsuta, alijitoa hatiani mbele ya hakimu kwa kumkubali Yesu Kristo kama kiongozi wa maisha yake; halafu akapiga magoti pembeni kwa Yakobo, ili na yeye akatwe kichwa kama mfuasi wa Yesu Kristo. Bartholomayo, ambaye pia alijulikana kama Nathanali, alikuwa mmisionari huko Asia. Alimshuhudia Yesu mfalme wa wafalme katika Uturuki ya leo. Bartholomayo aliteswa kwa sababu ya mahubiri yake huko Armenia, ambako inasemekana aliuwawa kwa kuchapwa bakora mbele ya halaiki ya watu iliyomdhihaki. Andrea alisulubiwa katika msalaba wa X huko Patras nchini Ugiriki. Baada ya kuchapwa bakora kinyama na walinzi saba, alifungwa mwili mzima kwenye msalaba ili ateseke zaidi. Wafuasi wake waliokuwepo katika eneo la tukio waliripoti ya kuwa, alipokuwa akipelekwa msalabani, Andrea aliusalimia msalaba huo kwa maneno yafuatayo: "Nimekuwa nikitamani sana na nimekuwa nikiitegemea sana saa hii ya furaha. Msalaba uliwekwa wakfu na Mwenyezi Mungu baada ya mwili wa Yesu Kristo kuning’inizwa juu yake." Aliendelea kuwahubiria maadui zake kwa siku mbili zaidi, akiwa msalabani, mpaka akaishiwa na nguvu na kuaga dunia. Tomaso alichomwa mkuki nchini India katika mojawapo ya safari zake za kimisionari akiwa na lengo la kuanzisha kanisa la Yesu Kristo katika bara la India. Mathiya alichaguliwa na mitume kuchukua nafasi ya Yuda Iskarioti, baada ya kifo cha Yuda katika dimbwi la damu nchini India. Taarifa kuhusiana na maisha na kifo cha Mathiya zinachanganya na hazijulikani sawasawa. Lakini ipo imani kwamba Mathiya alipigwa mawe na Wayahudi huko Yerusalemu, kisha akauwawa kwa kukatwa kichwa. Yuda Tadei, ndugu yake na Yesu, aliuwawa kwa mishale alipokataa kukana imani yake juu ya Yesu Kristo. Mitume walikuwa na imani kubwa kwa sababu walishuhudia ufufuo wa Yesu Kristo, na miujiza mingine. Biblia ni kiwanda cha imani. Tunapaswa kuiamini Biblia kama mitume walivyomwamini Yesu Kristo, kwa sababu Biblia iliandikwa na mitume.
Enock Maregesi
Mitume kumi na wawili wa Yesu Kristo waliamua kufa kinyama kulinda heshima ya mfalme wao Yesu Kristo, kama Biblia na historia vinavyosema. Kwa nini watu (wengine) wa kizazi hiki wanasema hakuna Mungu na kwa sababu hiyo hawamwamini Yesu? Je, uko tayari kufa kwa ajili ya mtu aliyekufa kwa ajili yako? Kwa ajili ya mtu ambaye mitume walikuwa tayari kufa kwa ajili yake? Je, wewe una akili zaidi kuliko mitume? Yesu aliamua kufa ili wewe uishi, lakini bado unakuwa mbishi. Badilika.
Enock Maregesi
Wachawi wanamwabudu Shetani. Lakini Shetani wanayemwabudu si Shetani Ibilisi aliyeumbwa na Mwenyezi Mungu kuja kuudanganya ulimwengu wote. Ni Shetani roho ya mabadiliko, mabadiliko ya kweli, ya ufahamu kamilia ulimwengu huu ambamo sisi sote tunaishi. Wachawi, kwa maneno mengine, wanaabudu miungu – kama vile Inanna wa Mesopotamia, Isis wa Misri, Asherah wa Kaanani au Belus wa Assyria ambaye ndiye mungu wa kwanza kuabuadiwa kama sanamu duniani – iliyotwaliwa na Shetani tangu misingi ya ulimwengu huu kusimikwa. Dhambi aliyotenda Shetani mbinguni ni ndogo kuliko dhambi wanazotenda wachawi duniani, ijapokuwa dhambi aliyotenda Shetani haitaweza kusamehewa na ndiyo maana Shetani hataweza kuwasamehe wanadamu. Ni jukumu letu kuwaita wachawi wote kutoka Babeli na kuwaleta katika ukweli kama kweli wanayemwabudu ni Shetani Ibilisi, Shetani Beelzebub, Shetani Asmodeus, Shetani Leviathan, Shetani Mammon, Shetani Amon au Shetani Belphegor ambao ni mabingwa wa kiburi, uroho, zinaa, wivu, fedha, hasira na uvivu duniani. Wachawi hawajui, na usipojua waweza kufa bila kujua.
Enock Maregesi
In conjunction with the development of the theology of the Occultation and the foundation of Twelver Shi’ism, another branch of Shia was also making great strides in the 9th and 10th centuries: the Ismailis.  After the death of the 6th Imam, Jafar, the Shia split between the followers of the son of his elder son Ismail (hence the term “Ismailis”) and the followers of his third son, Musa.  The followers of Musa remained based in Medina and developed an intellectual strand of Shi’ism around their clerical Imams that eventually lead to the Occultation.  The Ismailis, on the other hand, took a more political approach to their Imamate, based out of the restive Shia city of Kufa.
Jesse Harasta (The History of the Sunni and Shia Split: Understanding the Divisions within Islam)
When the major met with Kufa’s mayor, he made an odd request: Could they keep food vendors out of the plazas? Sure, the mayor said. A few weeks later, a small crowd gathered near the Masjid al-Kufa, or Great Mosque of Kufa. Throughout the afternoon, it grew in size. Some people started chanting angry slogans. Iraqi police, sensing trouble, radioed the base and asked U.S. troops to stand by. At dusk, the crowd started getting restless and hungry. People looked for the kebab sellers normally filling the plaza, but there were none to be found. The spectators left. The chanters became dispirited. By 8 P.M., everyone was gone.
Charles Duhigg (The Power of Habit: Why We Do What We Do and How to Change)
An important event during the government of Haroon was the discovery of the hidden grave of Imam Ali (AS) in Najaf. The Shia Imams knew its hidden location and had kept it as a secret. They had only revealed it to their close companions. This location was hidden from the public for about 130 years until the government of Haroon. During this long period, the holy grave of Imam Ali was protected from the vengeful actions of the Khawarij and the Umayyads, who hated Imam Ali’s justice. For example, during the government of Hajjaj in Kufa, around 3,000 graves were exhumed by his order in an attempt to find and disrespect Imam Ali’s grave. At the time of Haroon, no serious threat was facing the unveiled grave of Imam Ali. The Khawarij ideology had been weakened and their activities were limited to the boundaries of the Islamic
Mahdi Maghrebi (A Historical Research on the Lives of the 12 Shia Imams)
*Wazee wanasema, "Usijaribu kupaa kabla ya mabawa yako kuota." Ni hatari hata kwa kifaranga au ndege anayejitutumua na kuanza kuruka kabla ya mabawa na manyoya yake kuota vizuri. Kifaranga kinapaswa kiwe na subira; kikijitutumua na kuruka, huenda kikajiumiza au kuzama na kufa majini. Kila jambo na wakati wake. Tusitamani utajiri, cheo, au mamlaka kwa haraka haraka bila hata ya kupata uzoefu. Mungu aliweka matawi ya chini kwa ajili ya wale wasioweza kuruka vizuri ili hata wakianguka, wasipate kuumia sana. Na hata baada ya kufanikiwa kuruka, tambua kwamba hata ukifanikiwa kuruka juu kiasi gani, lazima utarudi chini tu kwa ajili ya kutafuta chakula.* mkia ukikatika ng'ombe hawezi kuazima kufukuzia nzi, linda heshima yako ukiipoteza hutaweza kuazima heshima ya mtu mwingine kujiheshimisha. Mchana mwema.
©️Pd. PK
Tunazaliwa, kuteseka na kufa kwa sababu ya dhambi ya asili ya wazazi wetu wa kwanza (Adamu na Hawa). Kama Hawa asingekubali kudanganywa na Shetani, tungezaliwa bila uchungu, tungeishi bila kuteseka na tusingekufa milele. Lakini haya ndiyo mawazo yangu: Mungu Ahusiki na dhambi, Ahusiki na mwili, Anahusika na roho. Hivyo, mtu anapofariki mwili unabaki duniani lakini roho inarudi kwa Mungu; kwani Yeye ndiye aliyeitengeneza na kuiweka katika moyo wa mtu. Mimi na wewe ni viumbe vyenye thamani kubwa sana mbele za Mwenyezi Mungu; mapenzi Yake kwetu hayana masharti yoyote. Hainiingii akilini (hata kidogo) kumtesa mtu unayempenda kiasi hicho milele, wakati uwezo wa kumwokoa unao.
Enock Maregesi
Watu wanaoogopa kufa huogopa pia kuishi.
Enock Maregesi
Ukitaka kuishi usiogope kufa. Kwa maneno mengine, ukitaka kufanikiwa katika maisha yako, usiogope kufa.
Enock Maregesi
Asiyeogopa kufa anaogopa kuishi.
Enock Maregesi
Yeyote anayesema haogopi kufa anajua hatakiwi kuwa jasiri kiasi hicho.
Enock Maregesi
Neno la mwisho kuongea kabla ya kufa lina nguvu kubwa kuliko la kwanza baada ya kuzaliwa.
Enock Maregesi
Mnamo mwaka 1957 Rais David Eisenhower wa Marekani (inasemekana) alipewa taarifa usiku mmoja akiwa Washington, D.C., kuhusu chombo cha ajabu kilichoanguka kwenye jangwa la Nevada huko Marekani. Ndani ya chombo kile kulikuwa na ‘aliens’ wawili, nao waliomba kuonana na Eisenhower kuhusu ujumbe waliokuja nao kutoka katika ulimwengu wao. Bila kuchelewa, Eisenhower alipanda ndege usiku huohuo mpaka Texas. Huko alichukua gari hadi kwenye eneo la kijeshi liitwalo Area 51, ambapo ndipo ule ujumbe wa ulimwengu mwingine ulipokuwa umeshikiliwa. Mkutano wa aina yake ulifanyika chini ya ardhi, kati ya Rais Eisenhower na hao viumbe wawili wa anga za mbali, chini ya tafsiri ya wanasayansi wa NASA. Walichotaka ni urafiki na dunia yetu, inayogombewa na dunia nyingi za ‘aliens’, kwa mbadala wa teknolojia kadha wa kadha ambazo sisi hatukuwa nazo. Pande zote mbili zilifikia maafikiano, wao wakitupa teknolojia, sisi tukiwapa uwezo wa kufanya majaribio ya kisayansi kwa binadamu wa dunia nzima. Hivyo kuanzia hapo ‘aliens’ wakawa na uhalali wa kuteka watu katika mazingira ya kutatanisha na kuingilia watu usiku wakiwa wamelala, katika tukio la kiulimwengu wa roho lijulikanalo kama ‘sleep paralysis’. ‘Sleep Paralysis’ ni tukio la ajabu. Mtu anapokuwa amelala mwili wake huonekana kufa ganzi, kiasi kwamba anajihisi hawezi hata kunyanyua mkono. Aghalabu hali hiyo inapotokea maana yake ni kwamba ‘aliens’ wanamchukua huyo mtu, kupitia kwenye paa la nyumba aliyolala, hadi mawinguni katika ndege yao. Ndani ya ndege wanaulaza mwili wa binadamu juu ya kitanda cha upasuaji, na kumfanyia upasuaji, ili kusoma biolojia iliyotumika kuumba wanadamu na kujua kwa nini sisi tuko tofauti na wao. Baada ya hapo wanamrudisha huyo mtu kitandani kwake, ambapo atalala usingizi wa kawaida hadi asubuhi. Atakapoamka hatajua kama alifanyiwa upasuaji. Wapo mamilioni ya watu duniani waliolalamika kutokewa na ‘aliens’, lakini serikali haziwahi kuilithibitisha hilo. Inavyosemekana, teknolojia za ‘aliens’ zinahifadhiwa na Jeshi la Marekani (Pentagon) na shirika la kijasusi la MAJI au MJ12. MJ12 ni watu 12 hatari zaidi duniani, wakiongozwa na mkurugenzi mkuu wa CIA (anayejulikana kama MJ1).
Enock Maregesi
Sigara zilizidi kuvutwa, ndani ya nyumba, na magaidi wale wawili, wakati Murphy akisinzia kudanganyia kama kweli nguvu zilishamwisha. Alimfikiria tena mpenzi wake Sophia, safari hii sana. Alimkumbuka Debbie; hakujua alikuwa wapi na hakujua mama yake angefanya nini kama Debbie angekufa, na Murphy ndiye aliyetoka naye. Debbie alimuuma zaidi. Alimkataza kufa kwa ajili ya mchumba wake. Sasa alikufa kwa ajili ya mtu ambaye hakumjua. Murphy alijilaumu kumtongoza na kumchukua kwao na kulala naye na kula chakula chake cha kifalme. Wazazi wake wangejisikiaje kama angekufa, tena katika mazingira ya kutatanisha kama yale. Kufa alijua angekufa; lakini Mungu angemsaidia, awaage watu wake.
Enock Maregesi (Kolonia Santita)
Nyoka ni mnyama mdogo lakini anayeogopwa hata na majambazi wakubwa. Adui wa dirishani alipogeuka kumwangalia Murphy, alimwangalia pia mwenzake na kucheka bila Murphy kujua kilichofanya wafurahi. Ghafla, kuna kitu kilitokea! Nyoka mkubwa aina ya swila aliruka toka dirishani na kuanguka katika mabega ya yule adui. Adui aliruka kwa woga na kuanguka chini … halafu yakatokea maajabu! Bunduki ilifyatuka kutoka nje, ikaripuka kwa sauti ya juu, walinzi wote wa Murphy wakaruka na kuanguka chini shaghalabaghala, na kufa papo kwa papo!
Enock Maregesi (Kolonia Santita)
Tunazaliwa na kufa. Lakini hatujui tunakotoka. Wala hatujui tunakokwenda. Huenda tunatoka na kwenda katika dunia nyingine, ya ulimwengu mwingine, hivyo kutufanya wageni wa dunia yetu wenyewe. Acha dunia katika hali nzuri kuliko ulivyoikuta.
Enock Maregesi
Jamais je ne m’étais plaint de l’adversité, jamais je ne m’étais troublé devant les nombreux soucis qui m’assaillaient, jusqu’au jour où je me trouvai pieds nus, sans argent pour m’acheter des babouches. Contrarié, j’entrai dans la mosquée de Kufa afin d’apaiser la douleur de mon cœur. C’est alors que je vis un homme qui n’avait pas de pieds…
Saadi Shirazi, Le Gulistan
Muda haututoshi. Tunajua mizigo hiyo ni ya nani. Tunajua nani aliua maafisa wetu wa polisi na maafisa wa polisi wa Meksiko na Marekani na wapita njia na kwa nini alifanya hivyo. Hatujui kwa hakika imefichwa wapi. Kuwakamata wahusika ni kazi nzito, ndugu wajumbe. Inahitaji ujasiri wa kupindukia … na kujitoa mhanga. Kuzuia mizigo ya CS-14, na kumkamata kiongozi wake, lazima tupigane kufa na kupona. Kwa siku kumi shehena zikamatwe na kuharibiwa, na viongozi wa Santita (wote) wakamatwe na kuwekwa chini ya sheria.
Enock Maregesi (Kolonia Santita)
Mambo mawili ya kuchagua kwa binadamu anayejitambua,Katika maisha ya kawaida kuna KUFA au KUFANIKIWA
Chrisper Malamsha
Kilio kikuu cha Yesu, “Eloi, Eloi, lama sabakthani?”, yaani, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?”, na “Imekwisha”, vilitabiriwa katika Zaburi 22 ili watu waliompinga Kristo waamini kama Yesu alikuwa Masihi. Zaburi 22 ulikuwa wimbo maarufu katika kipindi cha karne ya kwanza, kipindi ambacho Yesu alizaliwa na kufa, uliotungwa na mfalme Daudi, ulioitwa ‘zaburi ya mateso na matumaini ya mwadilifu’. Kwa hiyo Yesu aliposema maneno hayo yaliwaingia watu akilini, na kuanzia hapo imani hasa ya Ukristo ikachukua kasi hadi leo hii. Zaburi 22 inaanza na “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?” na inaisha na “Imekwisha”, miongoni mwa maneno saba aliyoyasema Yesu pale msalabani Golgotha. Kwa hiyo, Zaburi 22 ni utabiri wa kifo cha Yesu.
Enock Maregesi
Yesu alipokuwa msalabani watu wengi walimzunguka. Askari wa Kirumi aliyekuwa na chongo, na mkuki, alikuwa na jukumu la kumtesa Yesu hadi kufa kwa amri ya Pilato. Yesu alipolia kwa sauti kuu, “Eloi, Eloi, lama sabakthani?”, yule askari alikurupuka na kumwendea Yesu. Lakini Yesu alishakata roho. Kuthibitisha kama Yesu alishakata roho, askari alimchoma Yesu mkuki kwenye mbavu kwa nguvu zake zote. Mkuki huo ukamtoboa Yesu hadi upande wa pili, ukatoboa hata moyo wake. Askari alipochomoa mkuki, damu na maji viliruka na kupiga jicho lake bovu. Papo hapo askari akapona na kuona vizuri. Alipoona kweli amepona na kuona vizuri, askari alipiga kelele, alipiga magoti na kuomba Mungu amsamehe dhambi zake. Msamaha una nguvu kuliko dhambi. Askari huyo atakwenda mbinguni. Haijalishi umechukia watu kiasi gani. Haijalishi umetesa watu kiasi gani. Haijalishi umeua watu kiasi gani. Haijalishi umetenda dhambi kiasi gani. Mungu anachotaka kutoka kwako, tubu.
Enock Maregesi
Tukio la Yesu kufa, kufufuka na kupaa kwenda mbinguni bila mabawa ni tukio kubwa kuliko yote yaliyowahi kutokea katika historia ya ulimwengu huu. Naamini, Mungu yupo.
Enock Maregesi
Wanasayansi wana uwezo wa kupeleleza hadi kipindi cha karne ya kwanza ambapo Yesu aliishi, alikufa, alifufuka na alipaa kwenda mbinguni, na wana uwezo wa kujua mambo mengi kwa hakika yaliyofanyika katika kipindi hicho na hata katika kipindi cha kabla ya hapo. Kuna miujiza ambayo Yesu aliifanya ambayo haiko ndani ya Biblia. Kwa mfano, Biblia inasema Yesu alizaliwa ndani ya zizi la ng’ombe wakati sayansi inasema alizaliwa nje ya zizi la ng’ombe; na muujiza wa kwanza kuufanya ambao hauko ndani ya Biblia ni kutembea mara tu baada ya kuzaliwa, na watu na ndege wa angani kuganda kabla ya kuzaliwa Masihi na kabla ya wakunga kufika kumsaidia Maria Magdalena kujifungua. Akiwa na umri wa miaka sita, sayansi inasema, Yesu alikuwa akicheza na mtoto mwenzake juu ya paa la nyumba ya jirani na mara Yesu akamsukuma mwenzake kutoka juu hadi chini na mwenzake huyo akafariki papo hapo. Watu walipomsonga sana Yesu kwa kumtuhumu kuwa yeye ndiye aliyesababisha kifo cha mwenzake, na kwamba wangemfungulia mashtaka, Yesu alikataa katakata kuhusika na kifo hicho. Lakini walipozidi kumsonga, aliusogelea mwili wa rafiki yake kisha akamwita na kumwambia asimame. Yule mtoto alisimama! Huo ukawa muujiza mkubwa wa kwanza wa Yesu Kristo, kufufua mtu nje ya maandiko matakatifu. Kuna mifano mingi inayodhihirisha uwepo wa Mungu ambayo wanasayansi hawawezi hata kuipatia majibu. Tukio la Yoshua kusimamisha jua limewashangaza wanasayansi hadi nyakati za leo. Mwanzoni mwa miaka ya 70 wanasayansi walijaribu kurudisha muda nyuma kwa kompyuta kuona kama kweli wangekuta takribani siku moja imepotea kama ilivyorekodiwa katika Biblia. Cha kushangaza, cha kushangaza mno, walikuta saa 23 na dakika 20 zimepotea katika mazingira ambayo hawakuweza na hawataweza kuyaelewa. Walipochunguza vizuri walikuta ni kipindi cha miaka ya 1500 KK (Jumanne tarehe 22 Julai) ambacho ndicho tukio la Yoshua la kusimamisha jua na kusogeza mwezi nyuma digrii 10, ambazo ni sawa na mzunguko wa dakika 40, lilipotokea. Kwa kutumia elimu ya wendo, elimu ya kupanga miaka na matukio ya Kibiblia, dunia iliumbwa Jumapili tarehe 22 Septemba mwaka 4000 KK. Hata hivyo, mahesabu ya kalenda yanaonyesha kuwa Septemba 22 ilikuwa Jumatatu (si Jumapili) na kwamba kosa hilo labda lilisababishwa na siku ya Yoshua iliyopotea. Hayo yote ni kwa mujibu wa Profesa C. A. Totten, wa Chuo Kikuu cha Yale, katika kitabu chake cha ‘Joshua’s Long Day and the Dial of Ahaz: A Scientific Vindication and a Midnight Cry’ kilichochapishwa mwaka 1890. Kama hakuna Mungu iliwezekanaje Yoshua aombe jua lisimame na jua likasimama kweli? Iliwezekanaje Yesu aseme atakufa, atafufuka na atapaa kwenda mbinguni na kweli ikatokea kama alivyosema? Ndani ya Biblia kuna tabiri 333 zilizotabiri maisha yote ya Yesu Kristo hapa duniani na zote zilitimia – bila kupungua hata moja. Utasemaje hapo hakuna Mungu? Mungu yupo, naamini, sijui. Tukio la Yesu kufa, kufufuka na kupaa kwenda mbinguni si la vitabu vitakatifu pekee, hata sayansi inakubaliana na hilo.
Enock Maregesi
In addition to a greater understanding of secular subjects, the invention of cryptanalysis aslo depended on the growth of religious sholarship. Major theological schools were established in Basra, Kufa and Baghdad, where thelogians scrutinized the revelations of Muhammad as contained in the Koran. The theologians were interested in establishing the chronology of the revelations, which they did by counting the frequencies of words contained in each revelation. The theory was that certain words had evolved relatively recently, and hence if a revelation contained a high number of these newer words, this would indicate that it came later in the chronology. Theologians also studied the Hadith, which consists of the Prophet's daily utterances. They tried to demonstrate that each statement was indeed attributable to Muhammad. This was done by studying the etymology of words and the structure of sentences, to test whether particular texts were consistent with the linguistic patterns of the Prophet.
Simon Singh (The Code Book: The Science of Secrecy from Ancient Egypt to Quantum Cryptography)
Understanding habits is the most important thing I’ve learned in the army,” the major told me. “It’s changed everything about how I see the world. You want to fall asleep fast and wake up feeling good? Pay attention to your nighttime patterns and what you automatically do when you get up. You want to make running easy? Create triggers to make it a routine. I drill my kids on this stuff. My wife and I write out habit plans for our marriage. This is all we talk about in command meetings. Not one person in Kufa would have told me that we could influence crowds by taking away the kebab stands, but once you see everything as a bunch of habits, it’s like someone gave you a flashlight and a crowbar and you can get to work.” The major was a small man from Georgia. He was perpetually spitting either sunflower seeds or chewing tobacco into a cup. He told me that prior to entering the military, his best career option had been repairing telephone lines, or, possibly, becoming a methamphetamine entrepreneur, a path some of his high school peers had chosen to less success. Now, he oversaw eight hundred troops in one of the most sophisticated fighting organizations on earth. “I’m telling you, if a hick like me can learn this stuff, anyone can. I tell my soldiers all the time, there’s nothing you can’t do if you get the habits right.
Charles Duhigg (The Power Of Habit: Why We Do What We Do In Life And Business)
Wapo watu ukitaka kuwaua wambie wasome vitabu. Hata ukiwambia someni kitabu fulani kujikinga na kifo wako tayari kufa kuliko kusoma.
Enock Maregesi
Not one person in Kufa would have told me that we could influence crowds by taking away the kebab stands
Charles Duhigg (The Power of Habit: Why We Do What We Do in Life and Business)
Jamais je ne m’étais plaint de l’adversité, jamais je ne m’étais troublé devant les nombreux soucis qui m’assaillaient, jusqu’au jour où je me trouvai pieds nus, sans argent pour m’acheter des babouches. Contrarie, j’entrai dans la mosquée de Kufa afin d’apaiser la douleur de mon cœur. C’est alors que je vis un homme qui n’avait pas de pieds…
Saadi Shirazi, Le Gulistan
Usikate tamaa kabla ya kufa. Pambana.
Enock Maregesi