Upole Quotes

We've searched our database for all the quotes and captions related to Upole. Here they are! All 3 of them:

Kuwa na utulivu na upole haimaanishi wewe ni dhaifu. Watu kama hao wanaonyesha kina, nguvu za ndani zilizo chini ya udhibiti. Ni kujua wakati wa kuzungumza na wakati wa kusikiliza; wakati wa kuchukua hatua na wakati wa kusubiri. Usiwadharau watu hao. Wanatembea duniani kwa nguvu kubwa zaidi!
David Shamala
Siku moja, jambo baya litatokea. Labda babu yako au mnyama wako kipenzi atafariki au shangazi yako atagundulika na kansa. Labda utafukuzwa kazi au utaachika kwa mumeo au mkeo mliyependana sana. Labda rafiki yako kipenzi atapata ajali mbaya ya gari na utatakiwa kupeleka taarifa kwa ndugu na marafiki zake. Kutoa taarifa ya jambo baya kwa mtu ni kazi ngumu sawa na kupokea taarifa ya jambo baya kutoka kwa mtu. Kama umeteuliwa kupeleka taarifa ya kifo au ya jambo lolote baya kwa mtu fanya hivyo kwa makini. Toa taarifa ya msiba au ya jambo lolote baya kwa hekima na busara kama Ibrahimu alivyofanya kwa Sara kuhusiana na kafara ya Isaka, si kama Mbenyamini alivyofanya kwa Eli kuhusiana na kutwaliwa kwa sanduku la agano na kuuwawa kwa watoto wake wawili. Jidhibiti kwanza wewe mwenyewe kama umeteuliwa kupeleka taarifa ya kifo au ya jambo lolote baya. Angalia kama wewe ni mtu sahihi wa kupeleka taarifa hiyo. Pangilia mawazo ya kile unachotaka kwenda kukisema au unachotaka kwenda kukiandika. Mwangalie machoni, si usoni, yule unayempelekea taarifa kisha mwambie kwa sauti ya upole nini kimetokea.
Enock Maregesi
Nabii wa kweli lazima awe na upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, na kiasi. Kuonyesha usungura wa manabii wa injili ya woga ni jukumu la kila Mkristo wa kweli, kuokoa roho za watu wengi kwa kadiri tutakavyoweza.
Enock Maregesi