Msaada Quotes

We've searched our database for all the quotes and captions related to Msaada. Here they are! All 9 of them:

Ukitaka kufanikiwa katika maisha angalia watu wanataka nini halafu wape. Kama wanataka burudani wape. Kama wanataka elimu wape. Kama wanataka bidhaa wape. Kama wanataka huduma wape. Wape kwa msaada wa wataalamu.
Enock Maregesi
Toa msaada katika jamii iliyosaidia kukulea ulipokuwa mdogo.
Enock Maregesi
Wewe kuingilia mambo ya John ni sawa na kusema, ‘Mungu umeshindwa hebu ngoja na mimi nijaribu; ngoja niingilie kati kukusaidia juu ya maisha ya John Doe.’ Hiyo ni dhambi. Tena ni dhambi kubwa. Unajifananisha na Mungu; kwamba Mungu wa John Doe ameshindwa kwa hiyo mungu wewe ndiye utakayemtatulia matatizo yake. Amri kuu ya kwanza ya Mungu inasema, ‘Usiwe na miungu mingine ila mimi.’ Kuingilia mambo ya John tayari umevunja amri ya kwanza ya Mungu kwa kujifanya Mungu. Mungu ana mpango na maisha ya John, na anatumia matatizo yake kumfikisha kwenye takdiri aliyompangia. Hivyo, wewe si Mungu, acha Mungu afanye kazi yake. Mungu akikuruhusu kuingilia kati, yaani John akiamua kwa hiari yake mwenyewe kukuomba msaada wa mawazo au ushauri, maana yake ni kwamba Mungu amekuchagua wewe kuwa sehemu ya mafanikio ya John Doe.
Enock Maregesi
Hutaweza kufikia malengo yako kikamilifu bila msaada wa wataalamu – Hata kama una kipaji au ujuzi kiasi gani.
Enock Maregesi
Wakati Ford Bronco inatoka katika Kiwanda cha Dongyang Pharmaceuticals S.A de C.V. (kilichomilikiwa na mkurugenzi mkuu wa 'methamphetamine' wa Kolonia Santita mfanyabiashara wa Kichina kutoka Chaling, katika jimbo la Hunan, kusini ya kati ya China, Li Dongyang; na mkurugenzi wa usalama wa Kolonia Santita kutoka Lomas de Chapultepec, Mexico City, Gortari Manuel) Daniel Yehuda na Radia Hosni, waliokuwa wakipiga picha kila kitu kilichokuwa kikiingia na kutoka kiwandani kwa ajili ya ripoti ya upelelezi wao ya baadaye, waliiona. Lakini, hawakujua kama ilikuwa ikienda Varsovia kumuua Murphy na Sajini Mogens. Bronco ilipofika Varsovia ilisimama kwa fujo mbele ya SUV ya msafara wa Mtoto wa Rais Debbie Patrocinio Abrego, aliyekuwa ndani ya Mgahawa wa Angus akicheza muziki wa 'mariachi' na John Murphy, huku Mogens akilinda usalama wa kamanda wake na usalama wa baa nzima. Kabla majambazi wa Kolonia Santita hawajaleta madhara au fujo yoyote kwa Vijana wa Tume, polisi walifika eneo lile haraka ilivyowezekana! Kwa msaada wa walinzi wa Debbie! Wale majambazi walipekuliwa na kukutwa na bastola moja ya Akdal Ghost, bunduki mbili za AK-47, na picha nne za Vijana wa Tume ndani ya gari yao. Polisi waliwakamata na kuwapeleka katika kituo cha polisi cha Tume ya Dunia kilichopo Zona Rosa, Mexico City.
Enock Maregesi
Ukimpa msaada uliyemkosea unammaliza.
Enock Maregesi
Maana halisi ya ukarimu si kutoa vitu au mali nyingi kwa watu wanaohitaji msaada, bali ni kutoa vitu au mali hizo bila kinyongo au unafiki wowote. Ukarimu unapaswa kutolewa kwa watu sahihi, wakati sahihi, kiasi sahihi na kwa moyo mmoja bila kinyongo chochote. Ukitoa kwa lengo la kupata faida, huo ni ubinafsi na unafiki mkubwa.
Enock Maregesi
Vitibegi vya makomandoo wa Tume ya Dunia (vitibegi vya msalaba mwekundu na vitibegi vya kujiokolea) vilikuwa na vifaa maridadi vya kisasa kama vile pisto, visu, madawa ya huduma ya kwanza, kalamu za Inka, ramani za Meksiko, tochi ndogo zenye mwanga mkali za Cyba-Lite, Vioo vya TOPS, vibiriti vya Firesteel, pasi za kusafiria, pesa na vipenga vyenye viwango vya sauti vya desabo 126. Kipenga chenye kiwango cha sauti cha desabo 126 kinaweza kupasua ngoma za masikio ya adui, na kuwajulisha Vijana wa Tume mwenzao alipo hivyo kwenda haraka na kumpa msaada.
Enock Maregesi
Irani itakapoipiga Israeli, kama ambavyo imeshaahidi, Israeli itajibu mapigo. Kwa vile Israeli ina nguvu zaidi kuliko Irani, itaipiga Irani kwa silaha za kawaida. Itaipiga hata kwa silaha za kinyukilia pia. Kutunisha misuli, Irani itaomba msaada wa kijeshi kutoka katika nchi za Kiarabu; ambazo zitakubali kuingilia kati na kuisaidia Irani. Kwa silaha za kawaida, bado nchi zote za Kiarabu zitakazokubali kuisaidia Irani hazitakuwa na uwezo wa kuishinda Israeli. Kuishinda itabidi zitumie silaha za kinyukilia. Silaha za kinyukilia zitakapoanza kutumika, Marekani itaingilia kati kuisaidia Israeli. Marekani itakapoingilia kati kuisaidia Israeli, Urusi itaingilia kati kuisaidia Irani. Ufaransa, Uingereza na Ujerumani zitaingilia kati kuisaidia Israeli; huku China ikiingilia kati kuisaidia Irani. Hapo Vita Kuu ya Tatu ya Dunia itaanzishwa rasmi. Katika vita hiyo ya kinyukilia na mbaya kuliko vita zote zilizowahi kupiganwa, Israeli itashinda vita na itaanzisha utawala wa Mpinga Kristo duniani kote. Kutakuwa na dini moja. Kutakuwa na serikali moja. Kutakuwa na sarafu moja. Watu watapungua hadi kufikia milioni 500, kama ilivyokuwa mwaka 1650, asilimia 7 ya idadi ya watu wote ya leo.
Enock Maregesi