Mchumba Quotes

We've searched our database for all the quotes and captions related to Mchumba. Here they are! All 4 of them:

Mwaka mmoja na nusu unatosha kumjua mwanamke kabla ya ndoa. Miezi sita itakufanya ujue kama mwanamke anaweza kuwa mchumba. Mwaka mmoja na nusu utakufanya ujue kama mwanamke anaweza kuwa mke.
Enock Maregesi
Kama unataka kuijua vizuri historia ya mwanamke hasa mwanamke unayetaka kuoana naye, usifanye naye mapenzi kwa miezi sita angalau. Ukifanya naye mapenzi kwa miezi sita au zaidi, au ndani ya miezi sita, halafu akakuchanganya kimapenzi, hutakuwa na uwezo mkubwa wa kuwasikiliza watu kuhusiana na historia yake.
Enock Maregesi
Radia Hosni, mhitimu wa mikanda miwili myeusi ya sanaa za mapigano za kareti na kung’fu katika ngazi ya dani mbili za kung’fu na dani moja ya kareti, mwanajeshi wa Tunisia aliyepata mafunzo ya kawaida ya kijeshi nchini Ufaransa na mafunzo ya kikomandoo nchini Uingereza kabla ya kujiunga na Tume ya Dunia, alikuwa mshindi wa tuzo ya shujaa wa taifa la Tunisia. Hussein Kashoggi alipokuwa akiwasili Tunis kutokea Copenhagen, Radia alikuwa katika Uwanja wa Mpira wa El Menzah akiangalia mechi kati ya Stade Tunisien na Espérance ST – timu ambayo mchumba wake Fathi Meoki alikuwa kocha msaidizi. Fujo zilipozuka, baada ya Stade Tunisien kufungwa bao moja kwa sifuri na Espérance ST, Radia alipanda Quadrifoglio na kuondoka kuelekea Uwanja wa Ndege wa Tunis-Carthage; ambapo alimpokea Hussein Kashoggi na jambazi wa Kolonia Santita, Delfina Moore.
Enock Maregesi
Sigara zilizidi kuvutwa, ndani ya nyumba, na magaidi wale wawili, wakati Murphy akisinzia kudanganyia kama kweli nguvu zilishamwisha. Alimfikiria tena mpenzi wake Sophia, safari hii sana. Alimkumbuka Debbie; hakujua alikuwa wapi na hakujua mama yake angefanya nini kama Debbie angekufa, na Murphy ndiye aliyetoka naye. Debbie alimuuma zaidi. Alimkataza kufa kwa ajili ya mchumba wake. Sasa alikufa kwa ajili ya mtu ambaye hakumjua. Murphy alijilaumu kumtongoza na kumchukua kwao na kulala naye na kula chakula chake cha kifalme. Wazazi wake wangejisikiaje kama angekufa, tena katika mazingira ya kutatanisha kama yale. Kufa alijua angekufa; lakini Mungu angemsaidia, awaage watu wake.
Enock Maregesi (Kolonia Santita)