β
Usiwe na wasiwasi, Peter. Hizo ni hisia zangu tu. Huwezi kuwa mpelelezi. Lakini, kusema ule ukweli, ningependa sana kuonana na John Murphy. Kuna kazi binafsi ningependa kumpa. Wewe unatoka Afrika, hujawahi kumwona?β Debbie alizidi kumshtua Murphy.
βNani?β Murphy aliuliza huku akitabasamu.
βJohn Murphy wa Afrika.β
βSijawahi kumwona. Mbona unamuulizia hivyo?β
Debbie alitulia. Kisha akarusha nywele ili aone vizuri.
βNampenda sana!β
βKwa nini?β
βSimpendi kwa mahaba, lakini.β
βNdiyo. Kwa nini?β
βOK. Nampenda kwa kipaji chake. Alichopewa na Mungu, cha ujasusi. Kusaidia watu.β
βAhaa!β Murphy alidakia, sasa akifikiri sana.
βMurphy ana mashabiki wengi hapa Meksiko bila yeye mwenyewe kujua, kwa sababu ya kupambana na wahalifu wa madawa ya kulevya β hasa wa huku Latino. Tatizo lake haonekani. Wengi hudhani ni hadithi tu, kwamba hakuna mtu kama huyo hapa duniani.β
βHapana! Murphy yupo! Ni mfanyabiashara maarufu huko Tanzania. Lakini ndiyo hivyo kama unavyosema ... Haonekani!
β
β