Woga Quotes

We've searched our database for all the quotes and captions related to Woga. Here they are! All 15 of them:

Tumaini lina nguvu kuliko woga… Usisimame. Endelea kutembea.
Enock Maregesi
Maskini na tajiri wana mawazo tofauti. Maskini hudhani utajiri ni chanzo cha matatizo. Tajiri hudhani umaskini ni chanzo cha matatizo. Maskini hudhani ubinafsi ni kitu kibaya. Tajiri hudhani ubinafsi ni kitu kizuri. Maskini ana mawazo ya kupata pesa bila kufanya kazi. Tajiri ana mawazo ya kupata pesa kwa kufanya kazi. Maskini hudhani tajiri ana tabia ya kuringa. Tajiri hupenda kuzungukwa na watu sahihi wenye mawazo sawa na ya kwake. Maskini hutengeneza pesa kwa kufanya kazi asizozipenda. Tajiri hutengeneza pesa kwa kufanya kazi anazozipenda. Maskini hudhani kuwa tajiri lazima usome sana. Tajiri hudhani kuwa tajiri si lazima usome sana. Maskini hutamani mambo mazuri ya wakati uliyopita. Tajiri hutamani mambo mazuri ya wakati unaokuja. Maskini huamini ili uwe tajiri lazima ufanye kitu fulani. Tajiri huamini ili uwe tajiri lazima uwe kitu fulani. Maskini hupenda kuburudishwa kuliko kuelimishwa. Tajiri hupenda kuelimishwa kuliko kuburudishwa. Maskini ana woga. Tajiri hana woga. Maskini hufundisha watoto wake jinsi ya kupambana na maisha. Tajiri hufundisha watoto wake jinsi ya kuwa matajiri. Maskini hana nidhamu ya mapato na matumizi. Tajiri ana nidhamu ya mapato na matumizi. Maskini hufanya kazi kwa bidii kupata pesa. Tajiri hutumia pesa kupata pesa. Maskini ni mdogo kuliko matatizo yake. Tajiri ni mkubwa kuliko matatizo yake. Maskini huamini unahitaji pesa kupata pesa. Tajiri huamini utapata pesa kwa kutumia pesa za wengine. Maskini ana wivu wa chuki. Tajiri ana wivu wa maendeleo. Fikiri kama anavyofikiri tajiri. Ukifikiri tofauti na anavyofikiri tajiri, utakufa maskini.
Enock Maregesi
Nyoka ni mnyama mdogo lakini anayeogopwa hata na majambazi wakubwa. Adui wa dirishani alipogeuka kumwangalia Murphy, alimwangalia pia mwenzake na kucheka bila Murphy kujua kilichofanya wafurahi. Ghafla, kuna kitu kilitokea! Nyoka mkubwa aina ya swila aliruka toka dirishani na kuanguka katika mabega ya yule adui. Adui aliruka kwa woga na kuanguka chini … halafu yakatokea maajabu! Bunduki ilifyatuka kutoka nje, ikaripuka kwa sauti ya juu, walinzi wote wa Murphy wakaruka na kuanguka chini shaghalabaghala, na kufa papo kwa papo!
Enock Maregesi (Kolonia Santita)
Watu wanaoogopa kufa huogopa pia kuishi.
Enock Maregesi
Ukiogopa kushindwa hutashinda.
Enock Maregesi
Heri kushindwa kuliko kuogopa.
Enock Maregesi
Maarifa hupunguza woga.
Enock Maregesi
Wafuasi wa Yesu Kristo watapata taabu kubwa ambayo haijawahi kutokea. Yeyote atakayempinga Mpinga Kristo, yeyote atakayepinga utawala wa Mpinga Kristo, atakiona cha mtema kuni. Watu wengi watauwawa kwa sababu ya ufuasi wao kwa Masihi. Wale watakaokuwa na talanta ya kuhubiri watauwawa kinyama, hadharani, ili liwe fundisho kwa wafuasi wengine wa Yesu Kristo. Miongoni mwa wale watakaokuwa wanahubiri injili ya kweli ya ufalme wa Mungu bila woga wa aina yoyote ile, atakuwemo Eliya na Enock. Eliya na Enock Mungu aliwachukua bila kuonja mauti, kama akiba, kwa sababu ya kipindi hicho cha Taabu ya Yakobo. Eliya na Enock wataibuka ghafla jijini Yerusalemu na kuanza kuhubiri injili ya kumpinga Mpinga Kristo. Kwa vile hawataogopa chochote, wala hawatamwogopa yeyote, serikali ya Israeli itawakamata na kuwatesa lakini hawatanyamaza.
Enock Maregesi
Musa alipokuwa mlimani kupokea Amri Kumi za Mungu kwa ajili ya Wana wa Israeli alikawia sana kurudi, kiasi cha watu kukata tamaa na kujiona wapweke wakiwa njiani kuelekea katika Nchi ya Ahadi. Kutokana na woga usio na kifani na kukata huko kwa tamaa waliamua kutosubiri tena kusikia neno kutoka kwa Mungu, au kuiona sura halisi ya Mungu kama Musa alivyokuwa amewaahidi, hivyo wakamlazimisha Haruni awatengenezee mungu kutokana na taswira ambayo tayari walishakuwa nayo vichwani mwao kuhusu mungu waliyemtaka; yaani ndama wa dhahabu, au mungu mpya ambaye angewapa chochote walichotaka muda wowote waliotaka.
Enock Maregesi
Maskini ana woga. Tajiri hana woga.
Enock Maregesi
Mungu anapokupa kipaji anategemea ukitumie vizuri kwa ajili ya wengine. Usipokitumia vizuri kwa ajili ya wengine, ama kwa uvivu au kwa woga, atawapa wengine wakitumia kwa ajili yako. Ukitumia vipaji vyako vizuri, Mungu atakuongezea maradufu. Yaani, ukitumia muda wako vizuri atakuongezea muda. Ukitumia nguvu zako vizuri atakuongea nguvu. Ukitumia pesa yako vizuri atakuongezea pesa. Ukitumia ukarimu wako vizuri atakuongezea ukarimu. Ukitumia maarifa yako vizuri atakuongezea maarifa.
Enock Maregesi
Wananchi wakiamua kufanya kitu katika nchi yao kwa asilimia 100 serikali, na taasisi zake zote, haitaweza kuwazuia. Kwa sababu, mamlaka ya wananchi hushinda ya serikali.
Enock Maregesi
Wananchi wataendelea kuwepo hata kama serikali haitakuwepo. Serikali haiwezi kuwashinda wananchi. Sauti ya umma ni sauti ya Mungu. Serikali haiwezi kumshinda Mungu.
Enock Maregesi
Kitalifa ni utiifu kamili, woga, umbali (kwa maana ya kuwa mbali na biashara ya mamafia wengine mpaka kwa makubaliano maalumu) na nidhamu ya kutoshirikiana na mamlaka zote za serikali. Ukishtakiwa kwa kosa la madawa au ujambazi ambalo hukufanya, utatumikia kifungo mpaka mwisho bila kushirikiana na polisi (kwa maana ya kutaja aliyehusika au waliohusika na uhalifu huo) hata kama aliyehusika au waliohusika hana au hawana uhusiano wowote na Kolonia Santita. Falsafa ya Kitalifa ni Sheria ya Kitalifa ya Kiapo cha Swastika cha Kolonia Santita. Na adhabu ya kuvunja sheria hiyo ni kifo.
Enock Maregesi
Nabii wa kweli lazima awe na upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, na kiasi. Kuonyesha usungura wa manabii wa injili ya woga ni jukumu la kila Mkristo wa kweli, kuokoa roho za watu wengi kwa kadiri tutakavyoweza.
Enock Maregesi