Wivu Quotes

We've searched our database for all the quotes and captions related to Wivu. Here they are! All 8 of them:

β€œ
Mbegu tunazopanda leo ni mazao ya msimu ujao. Ukipanda mbegu mbaya utavuna mabaya. Ukipanda mbegu nzuri utavuna mazuri. Ukitenda mabaya leo kesho yako itakuwa mbaya. Ukitenda mazuri leo kesho yako itakuwa nzuri. Okoa kesho leo kwa kupanda mbegu nzuri na kuzimwagilia kwa imani na upendo kwa watu. Mungu ataleta mvua, jua na ustawi wa mazao yako. Panda mbegu ya msamaha kwa maadui zako, uvumilivu kwa wapinzani wako, tabasamu kwa marafiki zako, mfano bora kwa watoto wako, uchapakazi kwa kazi zako, uadilifu kwa waajiri wako na kwa wafanyakazi wako pia kama unao, ndoto kwa malengo yako, na uaminifu kwa marafiki zako wa ukweli. Kila mbegu irutubishwe kwa mapenzi huru yasiyokuwa na masharti yoyote, au mapenzi huru yasiyokuwa na unafiki wa aina yoyote ile. Usifiche vipaji vyako. Ukiwa kimya utasahaulika. Usipopiga hatua utarudi nyuma. Usiwe na hasira, wivu au ubinafsi.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Maskini na tajiri wana mawazo tofauti. Maskini hudhani utajiri ni chanzo cha matatizo. Tajiri hudhani umaskini ni chanzo cha matatizo. Maskini hudhani ubinafsi ni kitu kibaya. Tajiri hudhani ubinafsi ni kitu kizuri. Maskini ana mawazo ya kupata pesa bila kufanya kazi. Tajiri ana mawazo ya kupata pesa kwa kufanya kazi. Maskini hudhani tajiri ana tabia ya kuringa. Tajiri hupenda kuzungukwa na watu sahihi wenye mawazo sawa na ya kwake. Maskini hutengeneza pesa kwa kufanya kazi asizozipenda. Tajiri hutengeneza pesa kwa kufanya kazi anazozipenda. Maskini hudhani kuwa tajiri lazima usome sana. Tajiri hudhani kuwa tajiri si lazima usome sana. Maskini hutamani mambo mazuri ya wakati uliyopita. Tajiri hutamani mambo mazuri ya wakati unaokuja. Maskini huamini ili uwe tajiri lazima ufanye kitu fulani. Tajiri huamini ili uwe tajiri lazima uwe kitu fulani. Maskini hupenda kuburudishwa kuliko kuelimishwa. Tajiri hupenda kuelimishwa kuliko kuburudishwa. Maskini ana woga. Tajiri hana woga. Maskini hufundisha watoto wake jinsi ya kupambana na maisha. Tajiri hufundisha watoto wake jinsi ya kuwa matajiri. Maskini hana nidhamu ya mapato na matumizi. Tajiri ana nidhamu ya mapato na matumizi. Maskini hufanya kazi kwa bidii kupata pesa. Tajiri hutumia pesa kupata pesa. Maskini ni mdogo kuliko matatizo yake. Tajiri ni mkubwa kuliko matatizo yake. Maskini huamini unahitaji pesa kupata pesa. Tajiri huamini utapata pesa kwa kutumia pesa za wengine. Maskini ana wivu wa chuki. Tajiri ana wivu wa maendeleo. Fikiri kama anavyofikiri tajiri. Ukifikiri tofauti na anavyofikiri tajiri, utakufa maskini.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Shetani alikuwa malaika aliyeumbwa na Mungu lakini baadaye akamwonea Mungu wivu, wivu wa madaraka, hivyo Mungu akamtupa duniani kwa sababu ya kupingana na utawala wake mtakatifu. Duniani Shetani akamtumia nyoka kama mdakale kumdanganya Hawa. Hawa na Adamu wakamsikiliza Shetani badala ya kumsikiliza Mungu, nao wakalaaniwa. Shetani akajidai kuwa alikuwa na uwezo wa kufanya uzao wote wa Adamu na Hawa uwe mbali na Mungu, hivyo Mungu akampa muda wa kujaribu na kuthibitisha madai yake, lakini Shetani mpaka leo bado hajafanikiwa. Wakiitawala dunia leo kwa udanganyifu wa hali ya juu, pamoja naye, ni baadhi ya malaika ambao Shetani alifanikiwa kuwalaghai huko mbinguni. Mungu akawalaani pia na kuwatupa huku duniani, ambako Shetani alipapenda zaidi.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Maskini ana wivu wa chuki. Tajiri ana wivu wa maendeleo.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Usimwabudu mungu mwingine isipokuwa Mungu. Usimwabudu mtu, mnyama, sanamu, samaki, au usiziabudu fikira zako kichwani. Usiitumikie kazi, mali, mila, anasa, siasa, wala usiyatumikie mamlaka au usiutumikie umaarufu au ufahari, kuliko Mungu. Ukiithamini kazi, mali, mila, anasa, siasa au ukiyathamini mamlaka, au ukiuthamini umaarufu au ufahari zaidi kuliko Mungu, au ukiyapa majukumu yako muda mwingi zaidi kuliko Mungu umeabudu miungu; wakati ulipaswa kumwabudu Mungu peke yake. Usiwe na vipaumbele vingine vyovyote vile katika maisha yako zaidi ya Mungu, kwani Mungu ni Mungu mwenye wivu.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Wachawi wanamwabudu Shetani. Lakini Shetani wanayemwabudu si Shetani Ibilisi aliyeumbwa na Mwenyezi Mungu kuja kuudanganya ulimwengu wote. Ni Shetani roho ya mabadiliko, mabadiliko ya kweli, ya ufahamu kamilia ulimwengu huu ambamo sisi sote tunaishi. Wachawi, kwa maneno mengine, wanaabudu miungu – kama vile Inanna wa Mesopotamia, Isis wa Misri, Asherah wa Kaanani au Belus wa Assyria ambaye ndiye mungu wa kwanza kuabuadiwa kama sanamu duniani – iliyotwaliwa na Shetani tangu misingi ya ulimwengu huu kusimikwa. Dhambi aliyotenda Shetani mbinguni ni ndogo kuliko dhambi wanazotenda wachawi duniani, ijapokuwa dhambi aliyotenda Shetani haitaweza kusamehewa na ndiyo maana Shetani hataweza kuwasamehe wanadamu. Ni jukumu letu kuwaita wachawi wote kutoka Babeli na kuwaleta katika ukweli kama kweli wanayemwabudu ni Shetani Ibilisi, Shetani Beelzebub, Shetani Asmodeus, Shetani Leviathan, Shetani Mammon, Shetani Amon au Shetani Belphegor ambao ni mabingwa wa kiburi, uroho, zinaa, wivu, fedha, hasira na uvivu duniani. Wachawi hawajui, na usipojua waweza kufa bila kujua.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Mammon ni mungu wa pesa wa kuzimu anayesimamia mambo yote ya kifedha ulimwenguni. Ni miongoni mwa mashetani saba waliotupwa na Mwenyezi Mungu hapa duniani kutokea mbinguni akiwemo Ibilisi, Beelzebub, Asmodeus, Leviathan, Amon na Belphegor. Ibilisi ni mungu wa kiburi, Beelzebub ni mungu wa uroho, Asmodeus ni mungu wa zinaa, Leviathan ni mungu wa wivu, Amon ni mungu wa hasira na Belphegor ni mungu wa uvivu. Jukumu la mashetani hawa ni kusimamia kwa uaminifu mkubwa kutokea kuzimu dhambi kubwa saba duniani ambazo ni kiburi, uroho, zinaa, wivu, hasira, uvivu na uchoyo. Dawa ya dhambi hizo ni busara, kiasi, ujasiri, imani, haki, tumaini na upendo.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Mungu si wa kudhihakiwa (Wagalatia 6:7)! Katika maneno kadhaa ya Biblia, anasema bila masihara kabisa kwamba yeye ni Mungu mwenye wivu (Kutoka 34:14; Kumbukumbu la Torati 6:4-15) – Yeye si wa kuabudiwa kama mungu mwingine yeyote yule (Kumbukumbu la Torati 12:3-4, 30-31). Alipowaagiza watu wake wateule Israeli kwa njia ya ibada yake, aliwaonya wasiongeze juu ya kile alichokuwa amewapa wala wasipunguze chochote (Kumbukumbu la Torati 4:2; 12:32; angalia pia Ufunuo 22:18-19). Kwa mfano, angalia hasira yake kuu wakati wana wa Israeli walipojaribu kumwabudu kupitia Ndama wa Dhahabu (Kutoka 32:1-9). Walitangaza kuwa ilikuwa sikukuu ya Bwana (mstali wa 5), lakini Mungu hakulithamini hilo! Alikuwa na hasira kali juu ya ibada ya sanamu za watu, kiasi kwamba alifikiria kuangamiza taifa zima na kuanza upya na familia ya Musa. Mungu huyohuyo – Yahweh, Bwana wa Agano la Kale – akawa Yesu Kristo! Je, Mwokozi wetu atakubali kuabudiwa kwa namna yoyote ambayo misingi yake imejikita kwenye uongo? Hapana! Na hili kwa vyovyote vile limezingatia mila na desturi zisizo za kibiblia (labda tunaweza kusema za β€œkipagani”) ambazo zimechukua nafasi ya maadhimisho ya kafara na ushindi wa kishindo wa Yesu Kristo.
”
”
Enock Maregesi