Uzalendo Quotes

We've searched our database for all the quotes and captions related to Uzalendo. Here they are! All 6 of them:

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa baba kwa familia yake. Kwa Tanzania alikuwa mlezi; wa ndoto ya haki, amani, uzalendo, ujamaa, na uhuru.
Enock Maregesi
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa bendera ya taifa letu! Alikuwa alama ya amani, haki, uhuru, ujamaa, uzalendo, na Tanzania.
Enock Maregesi
Kama huijui historia ya Zanzibar kwa nini unajiita Mtanzania? Uzalendo ni pamoja na kuijua nchi yako.
Enock Maregesi
Tabia yako ya siri mwanao atakuwa nayo! Kama Nelson Mandela alikuwa alama ya msamaha, msamaha ni tabia yetu. Kama Kwame Nkrumah alikuwa alama ya umoja, umoja ni tabia yetu. Kama Patrice Lumumba alikuwa alama ya uzalendo, uzalendo ni tabia yetu. Kama Robert Mugabe ni alama ya udikteta, udikteta ni tabia yetu. Kama Haile Selassie alikuwa alama ya ushujaa, ushujaa ni tabia yetu. Kama Samora Machel alikuwa alama ya ujamaa, ujamaa ni tabia yetu. Kama Julius Kambarage Nyerere alikuwa alama ya haki, haki ni tabia yetu. Sisi ni watoto wa wazalendo wa Afrika! Wao ni baba wa mataifa ya Afrika! Tumerithi tabia zao za siri.
Enock Maregesi
Wananchi wakiamua kufanya kitu katika nchi yao kwa asilimia 100 serikali, na taasisi zake zote, haitaweza kuwazuia. Kwa sababu, mamlaka ya wananchi hushinda ya serikali.
Enock Maregesi
Wananchi wataendelea kuwepo hata kama serikali haitakuwepo. Serikali haiwezi kuwashinda wananchi. Sauti ya umma ni sauti ya Mungu. Serikali haiwezi kumshinda Mungu.
Enock Maregesi