“
Sina jinsi. Nguzo ya maisha yangu ni historia ya maisha yangu. Historia ya maisha yangu ni urithi wa watu waliojifunza kusema hapana kwa ndiyo nyingi – waliojitolea vitu vingi katika maisha yao kunifikisha hapa nilipo leo – walionifundisha falsafa ya kushindwa si hiari. Siri ya mafanikio yangu ni kujitahidi kwa kadiri ya uwezo wangu wote. Hiyo wote katika herufi kubwa.
Wote katika herufi kubwa (WOTE) si neno la kawaida falau katika nukuu hii ya mafanikio. Linamaanisha kujitahidi kwa kadiri ya uwezo wako wote uliopewa na Mwenyezi Mungu. Watu wengi hujitahidi kwa kadiri ya uwezo wao. Usijitahidi kwa kadiri ya uwezo wako. Jitahidi kwa kadiri ya uwezo wako WOTE.
”
”