Msamaha Quotes

We've searched our database for all the quotes and captions related to Msamaha. Here they are! All 23 of them:

Toa msamaha kwa waliokukosea kwa sababu dhambi zilizofanya mkosane zilitoka kwa Shetani.
Enock Maregesi
Mandela alikuwa hodari ndiyo maana akapelekwa jela. Alikuwa mvumilivu ndiyo maana akakaa jela kwa miaka ishirini na saba. Alivyotoka akawa kiongozi bora wa Afrika Kusini. Utu ukafanya awasamehe binadamu wenzake. Urithi wa Nelson Mandela kwetu ni uhodari, uvumilivu, uongozi bora, utu na msamaha kwa binadamu wenzetu. Mandela alikuwa baba kwa familia yake. Kwa Afrika Kusini alikuwa mlezi wa ndoto, ya amani na uhuru.
Enock Maregesi
Kama umefanya au umesema kitu kibaya na ukasema ukweli mbele ya mtu au ya watu, omba msamaha kupata tena kibali cha umma.
Enock Maregesi
Ukipata matatizo kumbuka kwamba Yesu alipata matatizo pia, na kutokana na matatizo hayo mimi na wewe tulipata uhuru. Soma Biblia. Soma nyimbo katika kitabu cha Zaburi zinazomsifu Mungu katika kipindi cha matatizo. Funga na kuomba ukiamini kwamba mapenzi ya Mungu kwetu ni huru, yasiyokuwa na masharti yoyote. Toa msamaha kwa waliokukosea. Ni kitu cha muhimu kujilimbikizia imani katika kipindi cha amani, ili matatizo yakitokea usiweze kuyumba.
Enock Maregesi
Wataalamu wanaosoma au kufundisha msamaha huweka wazi kwamba unapomsamehe mtu, huwezi kupotezea au kukana uzito wa kosa alilokufanyia. Kusamehe ni hali fulani inayotoka ndani ya moyo wa mtu, ikiwa na hali ya uhuru wa hiari wa mtu mwenyewe kuamua kuachilia kile kinachomuumiza, pasipo kuwepo masharti ya aina yoyote ile kwa mtu aliyemuumiza.
Enock Maregesi
Mbegu tunazopanda leo ni mazao ya msimu ujao. Ukipanda mbegu mbaya utavuna mabaya. Ukipanda mbegu nzuri utavuna mazuri. Ukitenda mabaya leo kesho yako itakuwa mbaya. Ukitenda mazuri leo kesho yako itakuwa nzuri. Okoa kesho leo kwa kupanda mbegu nzuri na kuzimwagilia kwa imani na upendo kwa watu. Mungu ataleta mvua, jua na ustawi wa mazao yako. Panda mbegu ya msamaha kwa maadui zako, uvumilivu kwa wapinzani wako, tabasamu kwa marafiki zako, mfano bora kwa watoto wako, uchapakazi kwa kazi zako, uadilifu kwa waajiri wako na kwa wafanyakazi wako pia kama unao, ndoto kwa malengo yako, na uaminifu kwa marafiki zako wa ukweli. Kila mbegu irutubishwe kwa mapenzi huru yasiyokuwa na masharti yoyote, au mapenzi huru yasiyokuwa na unafiki wa aina yoyote ile. Usifiche vipaji vyako. Ukiwa kimya utasahaulika. Usipopiga hatua utarudi nyuma. Usiwe na hasira, wivu au ubinafsi.
Enock Maregesi
Mbegu ni neno la Mungu. Mfano bora, msamaha, ndoto, tabasamu, uadilifu, uaminifu, uchapakazi na uvumilivu ni maneno ya Mungu. Kwa hiyo mfano bora, msamaha, ndoto, tabasamu, uadilifu, uaminifu, uchapakazi na uvumilivu ni mbegu. Watu ni ardhi. Panda mbegu ya mfano bora kwa watoto wako, msamaha kwa maadui zako, ndoto kwa malengo yako, tabasamu kwa marafiki zako, uadilifu kwa waajiri wako na kwa wafanyakazi wako pia kama unao, uaminifu kwa marafiki zako wa ukweli, uchapakazi kwa kazi zako na uvumilivu kwa wapinzani wako. Kila mbegu irutubishwe kwa imani na upendo kwa watu.
Enock Maregesi
Mbegu ni neno la Mungu. Mfano bora, msamaha, ndoto, tabasamu, uadilifu, uaminifu, uchapakazi na uvumilivu ni maneno ya Mungu. Kwa hiyo mfano bora, msamaha, ndoto, tabasamu, uadilifu, uaminifu, uchapakazi na uvumilivu ni mbegu. Watu ni ardhi. Panda mbegu ya mfano bora kwa watoto wako, msamaha kwa maadui zako, ndoto kwa malengo yako, tabasamu kwa marafiki zako, uadilifu kwa waajiri wako na kwa wafanyakazi wako pia kama unao, uaminifu kwa marafiki zako wa ukweli, uchapakazi kwa kazi zako na uvumilivu kwa wapinzani wako. Kila mbegu irutubishwe kwa imani na upendo kwa watu. Katika mfano huu ukuaji unawakilisha utakaso, ambao ni muundo wa taswira ya Mungu ndani yetu kwa kuishi kama anavyoishi yeye kwa nguvu ya Roho Mtakatifu. Tunachotakiwa kufanya baada ya kupanda mbegu ni kutimiza wokovu wetu sisi wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka. Kutimiza wokovu wetu sisi wenyewe ni sawa na mvua, jua, palizi, mbolea, ili mavuno yaweze kuwa ya uhakika.
Enock Maregesi
Damu ya Mwanakondoo ina nguvu kuliko maombi. Mungu hauwi, Anamtumia Shetani kama wakala wake wa kutoa adhabu kwa binadamu. Ukifunikwa na damu ya Mwanakondoo Shetani, ambaye ni wakala, hatakuona. Lakini Mungu atakuona. Bila kafara ya damu hakuna msamaha wa dhambi. Bila kafara ya damu hakuna mafanikio.
Enock Maregesi
Yesu alipokuwa msalabani watu wengi walimzunguka. Askari wa Kirumi aliyekuwa na chongo, na mkuki, alikuwa na jukumu la kumtesa Yesu hadi kufa kwa amri ya Pilato. Yesu alipolia kwa sauti kuu, “Eloi, Eloi, lama sabakthani?”, yule askari alikurupuka na kumwendea Yesu. Lakini Yesu alishakata roho. Kuthibitisha kama Yesu alishakata roho, askari alimchoma Yesu mkuki kwenye mbavu kwa nguvu zake zote. Mkuki huo ukamtoboa Yesu hadi upande wa pili, ukatoboa hata moyo wake. Askari alipochomoa mkuki, damu na maji viliruka na kupiga jicho lake bovu. Papo hapo askari akapona na kuona vizuri. Alipoona kweli amepona na kuona vizuri, askari alipiga kelele, alipiga magoti na kuomba Mungu amsamehe dhambi zake. Msamaha una nguvu kuliko dhambi. Askari huyo atakwenda mbinguni. Haijalishi umechukia watu kiasi gani. Haijalishi umetesa watu kiasi gani. Haijalishi umeua watu kiasi gani. Haijalishi umetenda dhambi kiasi gani. Mungu anachotaka kutoka kwako, tubu.
Enock Maregesi
Macho ya tai yana nguvu mara nne zaidi ya macho ya mwanadamu. Tai ana uwezo wa kuona hadi umbali wa kilometa themanini bila matatizo yoyote. Ana uwezo wa kuruka hadi futi elfu kumi, na ana uwezo wa kukimbia hadi mwendokasi wa kilometa mia moja na ishirini kwa saa. Kihekima, wale tu wanaoweza kuona mbali kama tai ndiyo watakaouweza msamaha. Lakini wale wenye mabawa ya kuku, wale ambao hawawezi kuruka wala kuona mbali, watapata taabu sana kuijua radhi. Kwa hiyo, wanapaswa kukua. Ukiwa mnyenyekevu wa moyo hutamchukia adui yako.
Enock Maregesi
Msamaha si jambo dogo. Watu wadogo, watu wenye uwezo mdogo wa kufikiri, hawawezi kupambana na changamoto za msamaha. Msamaha ni kwa ajili ya watu wenye macho kama ya tai wanaoweza kuona mbali ambao wako tayari kushindwa vita ili washinde vita. Hewa inaingia ndani ya mapafu na kutoka; chakula kinaingia ndani ya mwili na kutoka; mwanamasumbwi anapigana bila kugombana; injini ya gari haiwezi kusukuma gari mbele au nyuma bila kutoa hewa katika paipu ya ekzosi. Lakini kile kinachoingia moyoni mwako hakitoki! Maumivu yanapoingia ndani ya moyo yanapaswa kutoka nje kama yalivyoingia kwa sababu, yasipotoka yatatengeneza sumu ndani ya moyo wako na yatatengeneza sumu ndani ya roho yako pia. Sumu hiyo itahatarisha safari yako ya mbinguni na Mungu hatakusamehe tena. Badala ya yule aliyekukosea kuumia, utaumia wewe uliyekosewa. Yesu anaposema samehe saba mara sabini hatanii. Usiposamehe, hutasamehewa.
Enock Maregesi
Msamaha si kwa ajili ya watu wenye mabawa ya kuku, ni kwa ajili ya watu wenye macho ya tai. Kua kuujua msamaha.
Enock Maregesi
Toa msamaha usiokuwa na masharti yoyote kwa yeyote aliyekukosea kwa sababu, dhambi iliyofanya mkosane ilitoka kwa Shetani. Kwa mfano, usiseme umesamehe lakini hutasahau, sema umesamehe na umesahau.
Enock Maregesi
Utamsaidiaje mtu aliyekukosea? Msamehe!
Enock Maregesi
Bila dhambi hakuna msamaha.
Enock Maregesi
Tabia yako ya siri mwanao atakuwa nayo! Kama Nelson Mandela alikuwa alama ya msamaha, msamaha ni tabia yetu. Kama Kwame Nkrumah alikuwa alama ya umoja, umoja ni tabia yetu. Kama Patrice Lumumba alikuwa alama ya uzalendo, uzalendo ni tabia yetu. Kama Robert Mugabe ni alama ya udikteta, udikteta ni tabia yetu. Kama Haile Selassie alikuwa alama ya ushujaa, ushujaa ni tabia yetu. Kama Samora Machel alikuwa alama ya ujamaa, ujamaa ni tabia yetu. Kama Julius Kambarage Nyerere alikuwa alama ya haki, haki ni tabia yetu. Sisi ni watoto wa wazalendo wa Afrika! Wao ni baba wa mataifa ya Afrika! Tumerithi tabia zao za siri.
Enock Maregesi
Upendeleo na msamaha ni sumu na baraka ya usuluhishi miongoni mwa watu kwa mpangilio huo. Yaani, upendeleo ni sumu ya usuluhishi, msamaha ni baraka ya usuluhishi. Usuluhishi wenye msamaha, usiokuwa na upendeleo wowote, ni dawa ya uhusiano mwema miongoni mwa watu. Upendeleo ni sumu ya usuluhishi – Msamaha ni kiuasumu cha usuluhishi.
Enock Maregesi
Msamaha si jambo rahisi. Tunapoumizwa, au watu wetu wa karibu wanapoumizwa, tendo la kusamehe linaweza kuwa gumu kuliko matendo yote. Lakini, tambua kwamba msamaha ni mchakato wa muda mrefu unaohitaji ujasiri mkubwa kuuanza hadi kuukamilisha, ongea na watu wanaoelewa maana ya msamaha ili wakuongoze katika mchakato huo. Vilevile, tambua kwamba hata wewe umewahi kufanya makosa na unahitaji msamaha, tambua kwamba suluhisho kamili linahitaji matendo kutoka kwa aliyekosea na kwa aliyekosewa. Wengine hupendwa kwa sababu wanastahili, lakini wengine wanastahili kwa sababu hupendwa. Mungu anatupenda kwa jinsi tulivyo hata kama tunajiona hatustahili. Hivyo, jithamini.
Enock Maregesi
Msamaha ni uamuzi wa makusudi wa kuachilia hisia za chuki au kisasi juu ya mtu au kikundi cha watu ambaye amekuumiza au ambacho kimekuumiza, bila kujali kama anastahili au kinastahili msamaha wako. Wataalamu wanaosoma au kufundisha msamaha huweka bayana ya kuwa, unaposamehe, hutakiwi kusitiri au kukana uzito wa kosa ulilofanyiwa. Msamaha haumaanishi kusahau wala haumaanishi kupuuza, au kujisingizia, makosa ambayo mtu amekufanyia au kikundi cha watu kimekufanyia. Ijapokuwa msamaha unaweza kusaidia kujenga uhusiano ulioharibika, haukulazimishi kupatana na mtu aliyekukosea au kumfanya asiwajibike kisheria kwa makosa aliyokufanyia. Badala yake, msamaha humletea yule anayesamehe amani ya moyo; na humpa uhuru kutokana na hasira aliyokuwa nayo, juu ya yule aliyemkosea.
Enock Maregesi
Mtu akikuomba msamaha msamehe. Usipomsamehe hutasamehewa na aliyetusamehe.
Enock Maregesi
Msamaha ni afya.
Enock Maregesi
Jifunze kusamehe na kwa kweli usamehe!
Enock Maregesi