Mipango Quotes

We've searched our database for all the quotes and captions related to Mipango. Here they are! All 7 of them:

β€œ
Familia yako haikusaidii chochote katika mipango ya takdiri yako. Hii inasikitisha sana. Unajitahidi kila siku kuwafurahisha watu unaowapenda na watu wako wa karibu. Kila ukijitahidi kupata kibali cha watu unaishia kudharaulika na kuonekana mjinga asiyekuwa na maana. Sikiliza mazungumzo ya ndani ya moyo wako. Wapendwa wako watakukubali kama mtu hodari asiyekata tamaa, na tena watakuheshimu kutokana na tabia zako hizo. Mabadiliko haya ya kifikra hayatatokea haraka kama unavyofikiria. Yatachukua muda. Hivyo, kuwa mvumilivu. Wakati huohuo, endelea kucheza ngoma uliyoianzisha mwenyewe, endelea na mipango yako kama akili yako inavyokutuma.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Kabla ya uasi, Mungu alimpa Shetani na wasaidizi wake ambao ni mapepo mamlaka makubwa juu ya kila kitu hapa duniani; kuanzia angahewa la dunia hadi ardhi ya dunia nzima nasi wakazi wake tukijumuishwa. Abadani tusisahau kwamba, kwa kiasi kikubwa, kupambana kwetu kama Paulo anavyosema ni dhidi ya hawa mapepo na mfalme wao ambaye ni Shetani. Tunaishi katika eneo ambapo hata wao wanaishi. Hawa mapepo wabaya huwatumia maadui wa msalaba wa Yesu Kristo kutekeleza mipango yao kwa lengo la kuwaangamiza marafiki wote wa msalaba wa Yesu Kristo, wanashawishiwa kwa kiasi kikubwa na hizo mamlaka za kimapepo, na kwa sababu wamedanganywa, hawajui hata kidogo kama Shetani anawatumia! Inawezekana hawajatwaliwa na mapepo lakini wanashawishiwa na mapepo kutenda kinyume na mapenzi ya Mungu kwa wanadamu wote.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Kama damu haina maana kwa nini Mungu anaipenda? Kama damu haina maana kwa nini Shetani anaipenda? Mungu ni roho, Shetani ni roho, lakini damu ni kitu kinachoonekana kwa macho. Kwa nini damu ni kitu cha muhimu kiasi hicho kwa Mungu na kwa Shetani pia? Damu ni pato la ziada la ufunuo wa kiroho. Yaani, damu ni sehemu ya ulimwengu wa roho. Mungu ndiye aliyetengeneza damu kwa malengo anayoyajua yeye mwenyewe, hata Shetani hajui kwa asilimia mia umuhimu wa damu katika ulimwengu unaoonekana na katika ulimwengu usioonekana. Damu ina uwezo wa kuzuia mapepo kutoka kuzimu yasiharibu mipango ya maisha ya watu na ina uwezo wa kuondoa dhambi. Kafara ya damu inapotolewa inaimarisha uhusiano kati ya mtu na ulimwengu wa roho. Roho unayoitolea kafara inasikiliza shida zako papo hapo na kila unachoomba aghlabu kinatekelezwa. Ukitoa kafara kwa ajili ya Shetani, Shetani atasikiliza shida zako. Ukitoa kafara kwa ajili ya Mungu, Mungu atasikiliza shida zako. Tatizo kubwa la mwanadamu ni dhambi! Jibu la tatizo hilo ni damu ya Yesu Kristo.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Mungu alikuumba miaka mingi kabla hujazaliwa. Ndani ya roho yako kulikuwa na mpango mkuu wa Mungu juu ya maisha yako katika kipindi chote utakachokuwa hai, na katika kipindi chote utakachokuwa mfu. Lakini Shetani katika mji wa angani unaosemekana kuzuia majibu ya maombi ya Danieli ya siku ishirini na moja, kutoka mbinguni kuja duniani, uitwao Sadiki, wenye mashetani wenye nguvu kuliko mashetani wote katika ufalme wa giza, akaizuia roho hiyo kisha akaiwekea mpango mkuu wa Shetani juu ya maisha yako ili umtumikie yeye badala ya kumtumikia Mwenyezi Mungu. Kwa mfano, Mungu alipanga uzaliwe mkoani Arusha. Halafu akapanga mke au mume wako azaliwe mkoani Mwanza. Mkoani Arusha Mungu alipanga uwe mwinjilisti wa vitabu, wakati mkoani Mwanza alipanga mke au mume wako awe mwimbaji wa nyimbo za injili. Katika mikoa yote miwili Mungu alishatuma malaika wema wa kuwasaidia katika mipango mikuu ya maisha yenu na kuwaepusha na hila zote za adui. Lakini badala ya kuzaliwa Arusha au Mwanza Shetani ataziprogramu roho zenu upya ili wa Arusha azaliwe Dodoma au Mara au Venezuela na wa Mwanza azaliwe Lindi au Kagera au Mombasa, ambapo hakutakuwa na malaika wema wa kuwasaidia. Badala ya kuwa mwinjilisti wa vitabu, Shetani atakufanya uwe jambazi; na badala ya kuwa mwimbaji wa nyimbo za injili, Shetani atakufanya uwe mwanamuziki. Ndiyo maana wakati mwingine ni vizuri kuhama sehemu unapoishi na kwenda kuishi sehemu nyingine, ambapo kwa kusaidiana na malaika wako wa mwanzo ambaye Mungu alikupangia kabla hujazaliwa, utafanikiwa katika maisha yako, kama alivyofanya Ibrahimu. Watu wengi wanaishi maisha ambayo si ya kwao. Kukomboa kile ambacho Mungu alikipanga ndani ya roho yako kabla hujazaliwa, na kabla roho yako haijazuiwa na mashetani wa angani, kuwa karibu na Mwenyezi Mungu. Kwa Mungu hakuna siri, atakufunulia tu.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Ukitamka nadhiri waziwazi Shetani atasikia. Akisikia atavuruga. Mipango yako yote aliyosikia itakuwa matatizoni.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Akili ya mipango ni bora kuliko akili ya darasani.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Tovuti za miadi (β€˜dating sites’) hutumia β€˜optimal stopping’ kuwachagulia watu wachumba wao. Wanachofanya ni kwamba wanachagua watu 100. Wanaondoa 37% ya kwanza ya wale ambao sifa zao haziendani na sifa unazozitaka. Kisha wanakuchagulia mtu waliyeona ni bora zaidi kuliko wote waliobakia. Huyo waliyekuchagulia anaweza kuwa mke au mume bora. Lakini Mungu ana mipango yake. Unaweza kushangaa mke au mume bora akatoka kwenye 37% ya wale walioachwa.
”
”
Enock Maregesi