Mapenzi Quotes

We've searched our database for all the quotes and captions related to Mapenzi. Here they are! All 23 of them:

Mapenzi ni kiburudisho kikubwa kuliko vyote katika maisha.
Enock Maregesi
Wanaume hujiua kwa sababu ya fedha. Wanawake hujiua kwa sababu ya mapenzi.
Enock Maregesi
Mapenzi ni wazimu, kama si wazimu si mapenzi.
Enock Maregesi
Wanaume wanaojiua kwa sababu ya mapenzi ni wanawake; wanawake wanaojiua kwa sababu ya fedha ni wanaume.
Panthera Tigrisi
John Murphy alifanya mapenzi na Debbie kwa faida ya Tume ya Dunia.
Enock Maregesi
Ukipata matatizo kumbuka kwamba Yesu alipata matatizo pia, na kutokana na matatizo hayo mimi na wewe tulipata uhuru. Soma Biblia. Soma nyimbo katika kitabu cha Zaburi zinazomsifu Mungu katika kipindi cha matatizo. Funga na kuomba ukiamini kwamba mapenzi ya Mungu kwetu ni huru, yasiyokuwa na masharti yoyote. Toa msamaha kwa waliokukosea. Ni kitu cha muhimu kujilimbikizia imani katika kipindi cha amani, ili matatizo yakitokea usiweze kuyumba.
Enock Maregesi
Kama unataka kuijua vizuri historia ya mwanamke hasa mwanamke unayetaka kuoana naye, usifanye naye mapenzi kwa miezi sita angalau. Ukifanya naye mapenzi kwa miezi sita au zaidi, au ndani ya miezi sita, halafu akakuchanganya kimapenzi, hutakuwa na uwezo mkubwa wa kuwasikiliza watu kuhusiana na historia yake.
Enock Maregesi
Hakuna mtu mwenye akili timamu anayetaka mabaya katika maisha yake. Mwanamume atake mwanamke mwenye matendo mema. Mwanamke atake mwanamume mwenye matendo mema. Misingi ya hasanati ni misingi ya utu. Tukiishi katika misingi ya utu, misingi ya matendo mema, tutaishi sawasawa na mapenzi ya Mungu. Kila mtu anapaswa kuishi na mke au mume aliye mwema.
Enock Maregesi
Kinachotokea katika dunia hii si kitu kizuri cha kuzoea au hata kufikiria. Hivyo tuna haki ya kuwa na mawazo, hasira na wanyonge kuhusiana na suala zima la maisha yetu hapa duniani. Hata hivyo hali hii itabaki kuwa hivyo kwa sababu Mungu ametaka iwe hivyo kwa sasa. Kwa maana hiyo, hekima ni kukubaliana na mapenzi ya Mungu. Lazima tukubaliane na kisichoweza kufikirika kuweza kubadilika.
Enock Maregesi
Mbegu tunazopanda leo ni mazao ya msimu ujao. Ukipanda mbegu mbaya utavuna mabaya. Ukipanda mbegu nzuri utavuna mazuri. Ukitenda mabaya leo kesho yako itakuwa mbaya. Ukitenda mazuri leo kesho yako itakuwa nzuri. Okoa kesho leo kwa kupanda mbegu nzuri na kuzimwagilia kwa imani na upendo kwa watu. Mungu ataleta mvua, jua na ustawi wa mazao yako. Panda mbegu ya msamaha kwa maadui zako, uvumilivu kwa wapinzani wako, tabasamu kwa marafiki zako, mfano bora kwa watoto wako, uchapakazi kwa kazi zako, uadilifu kwa waajiri wako na kwa wafanyakazi wako pia kama unao, ndoto kwa malengo yako, na uaminifu kwa marafiki zako wa ukweli. Kila mbegu irutubishwe kwa mapenzi huru yasiyokuwa na masharti yoyote, au mapenzi huru yasiyokuwa na unafiki wa aina yoyote ile. Usifiche vipaji vyako. Ukiwa kimya utasahaulika. Usipopiga hatua utarudi nyuma. Usiwe na hasira, wivu au ubinafsi.
Enock Maregesi
Taabini hii ni ngumu sana kwangu kuandika pamoja na kwamba ni miaka mitatu kamili toka giza liingie. Mwaka 2014, Novemba 4, nilimpoteza bibi yangu mpendwa, Martha Maregesi, aliyefariki dunia kutokana na ukongo wa kiharusi, na tutamkumbuka daima. Alikuwa na roho ya kipekee; na kifo chake kiliwagusa wengi, pamoja na kwamba aliishi maisha kamili, zaidi ya siku 25550, siku 5110 zaidi, ambazo ndizo tulizopangiwa na Mungu. Mapenzi ya mtu kwa bibi yake ni mapenzi ya kipekee. Nadhani Mungu aliwapa mabibi wote uwezo maalumu wa kuwapenda wajukuu zao, na kufanya maisha yao yatimie, kuwafanya wawe binadamu wazuri na wenye maadili mema. Alichangia pakubwa katika malezi yangu ya utotoni; na aghalabu naweza kukumbuka nikiwa naye jikoni akipika, huku mimi nikifanya kazi nyingine, lakini wakati huohuo akinifundisha mambo kadha wa kadha ya kunikomaza kimaisha. Bibi hakuwa tu bibi. Alikuwa mlezi, rafiki na mtu aliyenihamasisha sana katika maisha. Kifo kinaleta huzuni lakini kinaleta tumaini. Naamini bibi yangu atakwenda mbinguni, kwa sababu naamini alitubu dhambi zake akisaidiwa na wachungaji. Wachungaji hao walimtembelea kila siku, nyumbani au hospitalini, akiwa kitandani kwake akiugua. Bibi yangu alitimiza wajibu wake. Alizaliwa, aliishi, na alikufa katika toba. Siku nitakapokufa ningependa kuzikwa jirani na alipozikwa bibi yangu, ili Yesu atakaporudi tufufuke pamoja.
Enock Maregesi
Mapenzi, kama ilivyo kwa vitu vyote hapa ulimwenguni, hayawezi kuwepo bila kujumuishwa na fizikia na kemia yake! Bila kemia hakuna mapenzi ya kudumu. Tamaa ya ngono kimsingi huanza pindi unapokutana na mtu. Tamaa hiyo huweza kukua na kuwa kitu kingine kadiri muda unavyokwenda lakini chanzo kinakuwepo toka siku ya kwanza mlipokutana. Kemikali inayosababisha tamaa ya ngono na hata kuikuza tamaa hiyo ni 'phenyl ethylamine' ('fino itholamine') au PEA ambayo ni kemikali ya mapenzi ndani ya ubongo. Husisimua watu na huongeza nguvu za kimwili (fizikia) na kihisia (kemia). Tamaa husababisha mtu azalishe PEA nyingi zaidi, kitu kinachosababisha kujisikia kizunguzungu (cha hisia za kimapenzi) na dalili zingine kama magoti kutetemeka, jasho kutoka viganjani na kutokutulia. Kemikali hii inapozalishwa kwa kiwango kikubwa, hutuma alamu ('signals') kutoka kwenye ubongo mpaka kwenye viungo vingine vya mwili na kutumika kama 'dopamine' au 'amphetamine' ambazo ni kemikali za ulevi ndani ya ubongo. Iwapo unajiuliza kwa nini wewe au mtu mwingine unavutiwa na mtu ambaye hamwendani kimapenzi, inaweza kuwa ni kwa sababu una kiwango kikubwa cha kemikali hizo kuliko mwenzako, kitu ambacho huzidi uwezo wa kutumia kichwa na kutoa maamuzi bora kulingana na akili ya kuzaliwa. Kwa jumla, mapenzi yote ya kweli uhitaji angalau kiwango kidogo cha PEA kwa wale wanaopendana. Cha msingi kukumbuka ni kwamba kemikali hizi huja kwa vituo, nikiwa simaanishi kwamba tamaa ya ngono hupotea pale mtu anapoelekea kwenye uhusiano wa kudumu. Lakini mambo hubadilika. Hatuwezi kuvumilia zile hisia kali kadiri tunavyozidi kusafiri kuelekea kwenye uhusiano wa kudumu na kwenye maisha ya pamoja yenye furaha. Katika uhusiano wenye afya hata hivyo matatizo hutokea hapa na pale. Chanzo cha Murphy na Debbie kupendana kilikuwa kemia zaidi kuliko fizikia. Kama hakuna kemia hakuna mapenzi.
Enock Maregesi
Tunazaliwa, kuteseka na kufa kwa sababu ya dhambi ya asili ya wazazi wetu wa kwanza (Adamu na Hawa). Kama Hawa asingekubali kudanganywa na Shetani, tungezaliwa bila uchungu, tungeishi bila kuteseka na tusingekufa milele. Lakini haya ndiyo mawazo yangu: Mungu Ahusiki na dhambi, Ahusiki na mwili, Anahusika na roho. Hivyo, mtu anapofariki mwili unabaki duniani lakini roho inarudi kwa Mungu; kwani Yeye ndiye aliyeitengeneza na kuiweka katika moyo wa mtu. Mimi na wewe ni viumbe vyenye thamani kubwa sana mbele za Mwenyezi Mungu; mapenzi Yake kwetu hayana masharti yoyote. Hainiingii akilini (hata kidogo) kumtesa mtu unayempenda kiasi hicho milele, wakati uwezo wa kumwokoa unao.
Enock Maregesi
Natafuta mwanamke mwenye utu, wema, uaminifu na tabia njema – sifa ambazo ataendelea kuwa nazo hata uzeeni. Sifa hizi zinaweza kubadilika kwa sababu ya maisha au kwa sababu ya mapenzi ya Mungu, lakini mabadiliko haya hayatakuwepo kwa haraka. Sura haidumu. Tabia hudumu.
Enock Maregesi
Lengo la kuabudu ni kumtukuza, kumheshimu, kumsifia, kumfurahia, na kumpendeza Mungu. Ibada yetu lazima ionyeshe mapenzi ya kweli na uaminifu mkubwa kwa Mungu kwa ajili ya wema na rehema ambavyo ametupa kupitia Mwanaye wa Pekee aliyekufa msalabani, ili kutuokoa kutoka ubinafsini.
Enock Maregesi
Kuna siri ambayo wanaume hawaijui kuhusu wanawake. Wanawake wenye umri wa miaka kumi na nane hadi ishirini na mbili wana mapenzi ya kweli. Ishirini na mbili hadi ishirini na nne wana mawenge. Ishirini na nne hadi ishirini na saba wanajitambua. Ishirini na saba hadi thelathini wana hofu na mashaka mengi. Thelathini hadi thelathini na tano wana msongo wa mawazo. Thelathini na tano hadi arobaini na mbili ndoa nyingi huvunjika. Kwa hiyo, kuwa makini na wanawake na wanaume hasa wanawake na wanaume wa kundi la sita. Wanawake na wanaume hasa wanawake na wanaume wa kundi la sita, wengi wao wana DNA ya wapenzi wao wa zamani.
Enock Maregesi
Kabla ya uasi, Mungu alimpa Shetani na wasaidizi wake ambao ni mapepo mamlaka makubwa juu ya kila kitu hapa duniani; kuanzia angahewa la dunia hadi ardhi ya dunia nzima nasi wakazi wake tukijumuishwa. Abadani tusisahau kwamba, kwa kiasi kikubwa, kupambana kwetu kama Paulo anavyosema ni dhidi ya hawa mapepo na mfalme wao ambaye ni Shetani. Tunaishi katika eneo ambapo hata wao wanaishi. Hawa mapepo wabaya huwatumia maadui wa msalaba wa Yesu Kristo kutekeleza mipango yao kwa lengo la kuwaangamiza marafiki wote wa msalaba wa Yesu Kristo, wanashawishiwa kwa kiasi kikubwa na hizo mamlaka za kimapepo, na kwa sababu wamedanganywa, hawajui hata kidogo kama Shetani anawatumia! Inawezekana hawajatwaliwa na mapepo lakini wanashawishiwa na mapepo kutenda kinyume na mapenzi ya Mungu kwa wanadamu wote.
Enock Maregesi
Wakati Yuda ikiongozwa na kiongozi mzuri na mwenye haki kama Yosia, taifa lilistawi. Lakini ilipokuwa chini ya mwovu Manase, taifa lilisambaratika. Katika karne hii, Uingereza ilipata msukosuko mkubwa mwaka 1936 juu ya uamuzi wa Edward VIII kuoa mwanamke wa Kimarekani aliyekuwa mtalaka Wallis Simpson. Uamuzi huo ulisababisha matatizo makubwa ya kikatiba, na nusura serikali ya Uingereza ijiuzuru. Hata hivyo, kaka yake mdogo, George VI, kwa mapenzi makubwa na nchi yake, huku akikataa katakata kuondoka London wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia, aliliongoza taifa hilo katika kipindi kigumu zaidi kuliko vyote katika historia ya Uingereza. Kanuni hii ya uongozi ina ukweli katika jambo lolote kubwa na hata dogo la ujasiri.
Enock Maregesi
Mwanampotevu dunia ilimfundisha ndiyo maana akarudi kwa baba yake akiwa amenyooka, hakuwa na maadili mema. Yusufu dunia ilimfundisha ndiyo maana akawa waziri mkuu wa Misri, na ndiyo maana akaokoa familia yake kutokana na njaa, alikuwa na maadili mema. Heri kudharaulika kwa kutenda mema kuliko kudharaulika kwa kutenda maovu. Ukidharaulika kwa kutenda maovu hutaishi sawasawa na mapenzi ya Mungu. Ukidharaulika kwa kutenda mema Mungu atakuinua.
Enock Maregesi
Hakimu na Kuhani Mkuu wa Shilo Eli alipata matatizo makubwa wakati wa mgogoro wa Waisraeli na Wafilisti, kati ya mwaka 2871 na 2870 Kabla ya Kristo. Mara tu baada ya kupewa taarifa ya kifo cha watoto wake wawili, Hofni na Finehasi, na kutwaliwa kwa Sanduku la Agano la Bwana wa Majeshi lililohifadhi Amri Kumi za Mungu, Eli alianguka kutoka katika kiti chake na kufariki papo hapo akiwa na umri wa miaka 98. Aidha, mkwe wa Eli, mke wa Finehasi, alijifungua ghafla na kufariki alipopata taarifa ya kifo cha mkwewe na taarifa ya kuuwawa kwa mumewe na ya kutekwa nyara kwa Sanduku la Agano. Mwanajeshi kutoka Benyamini falaula angetumia hekima na busara kutoa taarifa ya kifo na ya kutwaliwa kwa Sanduku la Agano huenda Eli asingefariki, na huenda mkwewe asingejifungua mtoto njiti na huenda asingekufa siku hiyo. Kwani Sanduku la Agano lilirejeshwa nchini Israeli, na Wafilisti wenyewe, baada ya miezi saba tangu litwaliwe, na kifo cha watoto wa Eli yalikuwa mapenzi ya Mungu. Hivyo Eli asingeweza kuzuia kifo cha watoto wake, na Wafilisti wasingeweza kukaa na Sanduku la Agano milele. Lakini katika kafara ya Isaka ambapo Isaka aliamua kujitoa kafara mwenyewe kumfurahisha Mungu na baba yake kama Yesu alivyoamua kujitoa kafara mwenyewe kumfurahisha Mungu na baba yake wa mbinguni, Sara angekufa kama Ibrahimu hangetumia hekima alipomwambia anakwenda kumtolea Bwana kafara ya mwanakondoo wakati akijua anakwenda kumtoa Isaka mtoto wa pekee wa Sara. Hekima inatoka moyoni, busara inatoka mdomoni. Kwa vile suala la kutoa taarifa mbaya kwa mtu ni gumu kwa yule anayetoa na kwa yule anayepokea, hekima na busara havina budi kutumika.
Enock Maregesi
Damu, mto wa maisha unaotiririsha maji yake mwilini kwa kusukumwa na pampu za moyo na kuchujwa na fizi za mapafu, inaundwa na seli na maji yaitwayo utegili au maji ya damu, ambayo kazi yake ni kusafirisha oksijeni na virutubisho katika kila sehemu ya mwili, ndani yake kuna roho. Mungu alitoa kafara ya damu kwa ajili ya Adamu na Hawa katika Bustani ya Edeni. Ibrahimu alitoa kafara ya damu kwa ajili ya Israeli ijapokuwa mapenzi ya Mungu kwa Israeli yalikwisha baada ya kusulubiwa kwa Yesu Kristo. Wana wa Israeli walitoa kafara za damu kwa ajili ya wokovu wa watoto wao wa kwanza na watoto wa kwanza wa wanyama wao nchini Misri. Mungu alitoa kafara ya damu ya Yesu Kristo nchini Israeli kwa ajili ya wanadamu wote duniani. Damu ya mwanakondoo ina nguvu kuliko maombi, imetiwa wakfu na Mwenyezi Mungu na ina uhusiano mkubwa na ulimwengu wa roho. Ukifunikwa na damu ya mwanakondoo Shetani hatakuona. Shetani asipokuona, utafanikiwa.
Enock Maregesi
Mapenzi ni kiburudisho kisichojulikana ladha yake. Huwezi kuyazuia.
Simon Mashalla
Licha ya matatizo yanayotokea tunapaswa kujua kwa imani kwamba Mungu asiyeonekana na mwenye nguvu bado yuko kwenye kiti chake cha enzi, akisimamia kila kitu kinachoendelea, huku akijua bayana kwamba mapenzi yake lazima yatimie, bila kujali watu wasiomwamini wenye upofu wa rohoni.
Enock Maregesi