Mambo Jambo Quotes

We've searched our database for all the quotes and captions related to Mambo Jambo. Here they are! All 6 of them:

Kuna tofauti kati ya haki na utawala wa mabavu. Haki ni jambo ambalo mtu anastahili au kitu anachostahiki kuwa nacho. Utawala wa mabavu ni utawala wa kidikteta. Ukitenda haki lazima kuna watu watafaidi. Lazima kuna watu wataumia. Fidel Castro alikuwa kiongozi msahili. Alikuwa kiongozi aliyewezesha kutendeka kwa mambo. Kwa sababu hiyo, wachache walimpenda, wengi walimchukia. Lakini ili ufanye mazuri lazima upambane na mabaya. Shetani mwenyewe hatakuruhusu ufanye mazuri bila kukuletea mabaya.
Enock Maregesi
Mbegu ni neno la Mungu na kudondoka kwake kwenye ardhi si mwisho wa maisha yake. Mambo kadha wa kadha yanaweza kutokea yanayoweza kuathiri ukuaji wa mbegu husika. Nyingine zinaweza kuanguka karibu na njia ndege wakaja wakazila, nyingine zinaweza kuanguka penye miamba pasipokuwa na udongo mwingi wa kutosha, nyingine zinaweza kujifukia ndani kabisa ya ardhi na kupotelea huko kwa miaka mingi, mvua inaweza kunyesha na kuhamisha baadhi ya mbegu kwa kuzisomba na maji. Lakini kwa kuwa maisha yamo ndani ya mbegu, jambo fulani litatokea.
Enock Maregesi
Shahidi mwaminifu na wa kweli anayajua mambo yetu yote tangu kuumbwa hadi mwisho wa dunia yetu. Kwa hiyo, ni kweli unabii lazima utimie. Mungu anataka tuwe na amani ndani ya mioyo yetu lakini anajua si jambo rahisi kwa sababu ya hila za Shetani. Shetani asingekuwepo amani ingekuwepo; watakatifu wasingekuwepo, dunia isingekuwepo. Lakini mlango wa rehema bado haujafungwa. Bado tuna uhuru wa kuchagua mema dhidi ya mabaya.
Enock Maregesi
Mfalme Sulemani alikuwa mtu mwenye hekima kuliko wote ulimwenguni. Anatushauri, “Adui yako akiwa ana njaa, mpe chakula; Tena akiwa ana kiu, mpe maji ya kunywa; Maana utatia makaa ya moto kichwani pake; Na BWANA atakupa thawabu (Mithali 25:21-22). Yesu anasema jambo fulani linalofanana sana na hilo katika mafundisho Yake yaliyofuata (Mathayo 5:44-45). Kitendo cha kutukanwa, kupigwa, kushtakiwa au kulazimishwa kubeba mzigo mzito usio wa kwako kinaweza kusababisha mafutu mabaya kabisa katika asili ya binadamu. Yaani, chuki, hasira, ukatili na hata vurugu. Lakini pale wale waliobarikiwa kuwa na hekima wanapojikuta katika majaribu makubwa kama hayo tabia yao haitakiwi kuwa ya shari, inda au ya kulipiza kisasi. Bali inatakiwa kuwa ya kusaidia, kuwa na ridhaa ya kutenda mambo mema, na kuwa mwema kwa wengine siku zote.
Enock Maregesi
Hata kama umetajirika kiasi gani mpe Mungu kipaumbele cha kwanza katika kila jambo unalofanya. Toa zaka na sadaka na jitolee katika mambo yote yanayompendeza Mungu.
Enock Maregesi
Mzazi wako akikutuma kufanya jambo jema ukakubali umemheshimu. Akikutuma kufanya jambo jema ukakataa umemdharau. Lakini, mzazi wako akikutuma kufanya jambo baya ukakubali umemdharau. Akikutuma kufanya jambo baya ukakataa umemheshimu. Hivyo, mheshimu mzazi wako katika mambo mema na katika mambo mabaya.
Enock Maregesi