Kufanikiwa Quotes

We've searched our database for all the quotes and captions related to Kufanikiwa. Here they are! All 19 of them:

β€œ
Kufanikiwa katika maisha ni kuwa tayari muda wowote kujitoa mhanga kwa ajili ya kitu unachoweza kuwa.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Kufanikiwa katika maisha lazima usimamiwe na nguvu za nuru au nguvu za giza. Kama ni nuru lazima ubobee katika nuru. Kama ni giza lazima ubobee katika giza.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Ukitaka kufanikiwa katika maisha yako kuwa tayari kuitwa mjinga au mpumbavu.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Ukitaka kufanikiwa katika maisha angalia watu wanataka nini halafu wape. Kama wanataka burudani wape. Kama wanataka elimu wape. Kama wanataka bidhaa wape. Kama wanataka huduma wape. Wape kwa msaada wa wataalamu.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
ATP hutumika katika kipindi ambapo mtu anakuwa amekata tamaa kabisa katika jambo lolote analolifanya, na yeyote anayetumia ATP ana uwezo mkubwa wa kufanikiwa katika maisha yake. Hivyo, usikate tamaa, jitahidi kwa kadiri ya uwezo wako WOTE.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Kufanikiwa katika maisha lazima kitu fulani ambacho si cha kawaida kitokee katika maisha yako, bila kujali uko upande wa Yesu au upande wa Shetani. Kufanikiwa katika maisha ni sawa na kwenda mbinguni, au kuishi mbinguni duniani. Kitu ambacho si cha kawaida kutokea katika maisha yako ni sawa na kifo. Fanya kitu ambacho hujawahi kufanya kupata kitu ambacho hujawahi kupata.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Jina langu ni Enock Maregesi na ningependa kukwambia kisa kidogo kuhusiana na bibi yangu, Martha Maregesi. Mwanamke huyu alikuwa mke mwenye upendo usiokuwa na masharti yoyote. Alikuwa mama na bibi aliyefundisha familia yake umuhimu wa kujitolea na umuhimu wa uvumilivu. Ijapokuwa hakupendelea sana kujizungumzia mwenyewe, ningependa kukusimulia kisa kidogo kuhusiana na hadithi ya maisha ya mwanamke huyu wa ajabu katika maisha yangu. Bibi yangu alizaliwa katika Kitongoji cha Butimba, Kijiji cha Kome, Kata ya Bwasi, Tarafa ya Nyanja (Majita), Wilaya ya Musoma Vijijini, Mkoa wa Mara, katika familia ya watoto kumi, mwaka 1930. Alisoma katika Shule ya Msingi ya Kome ambako alipata elimu ya awali na msingi na pia elimu ya kiroho kwani shule yao ilikuwa ya madhehebu ya Kisabato. Aliolewa na Bwana Maregesi Musyangi Sabi mwaka 1946, na kufanikiwa kupata watoto watatu; wa kiume wakiwa wawili na wa kike mmoja. Matatizo hasa ya bibi yalianza mwaka 2005, alipougua kiharusi akiwa nyumbani kwake huko Musoma. Hata hivyo alitibiwa hapo Musoma na Dar es Salaam akapona na kuwa mwenye afya ya kawaida. Lakini tarehe 19/10/2014 alipatwa tena na kiharusi na kulazwa tena katika Hospitali ya Mkoa ya Musoma, ila akajisikia nafuu na kuruhusiwa kurudi nyumbani – lakini kwa maagizo ya daktari ya kuendelea na dawa akiwa nje ya hospitali. Tarehe 29/10/2014 alirudi tena Hospitali ya Mkoa ya Musoma kwa tiba zaidi, lakini tarehe 4/11/2014 saa 7:55 usiku akafariki dunia; akiwa amezungukwa na familia yake. Dunia ina watu wachache sana wenye matumaini na misimamo ya kutegemea mazuri, na wachache zaidi ambao wako tayari kugawa matumaini na misimamo hiyo kwa watu wengine. Nitajisikia furaha siku zote kwamba miongoni mwa watu hao wachache, hata bibi yangu alikuwemo. Msalaba uliwekwa wakfu na Mwenyezi Mungu baada ya mwili wa Yesu Kristo kuning’inizwa juu yake. Kwa kuwa bibi yangu ametanguliwa na msalaba, msalaba utamwongoza mahali pa kwenda.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Kuna siri nyingi za ndani zinazofanya mtu aendelee kufanikiwa, na kuna siri nyingi za nje zinazofanya mtu aendelee kuficha siri ya mafanikio yake. Siri za ndani ni siri za kweli, ilhali siri za nje ni siri za uongo, zenye lengo la kuficha ukweli. Hata hivyo, siri ya mafanikio ni kufanya kazi kwa bidii na maarifa, pamoja na siri.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Ukitaka kuishi usiogope kufa. Kwa maneno mengine, ukitaka kufanikiwa katika maisha yako, usiogope kufa.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Kwa mfano, uko kwenye mashindano ya mbio za mita 100. Utakapofika kwenye kamba, mwisho wa hizo mita 100, utakuwa umechoka sana. Lakini kocha anakuhimiza uendelee mbele mita nyingine 50! Unaweza kufika ukiwa mzima au unaweza kufika ukiwa umezimia. Lakini usijali. Ukiendelea mita nyingine 50 utakuwa umetumia uwezo wako wote uliopewa na Mwenyezi Mungu. Ukitumia kanuni hiyo katika maisha yako ya kawaida utaweza kufanikiwa.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Ukitaka kufanikiwa wasaidie wengine kufanikiwa.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Ukipata shida itakupa akili ya kufanikiwa, kwani shida ni kipimo cha akili.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Unataka kufanikiwa lakini hutaki watu wakuone. Kama una kipaji kionyeshe kwa watu.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Mambo mawili ya kuchagua kwa binadamu anayejitambua,Katika maisha ya kawaida kuna KUFA au KUFANIKIWA
”
”
Chrisper Malamsha
β€œ
Wakati mwingine tukitaka kufanikiwa lazima tujifunze kutunza siri.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Kufanikiwa lazima umshinde Shetani.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Kufanikiwa lazima ushindikane.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Yeyote anayekosoa kwa kutafuta makosa ya mipango yako bila kujua mipango yako ilivyojijenga ni mwaribifu. Mtu yeyote anayevunja itifaki za uongozi hawezi kufanikiwa maisha. Mungu huinua wenye unyenyekevu
”
”
Kennedy Mmbando
β€œ
*Wazee wanasema, "Usijaribu kupaa kabla ya mabawa yako kuota." Ni hatari hata kwa kifaranga au ndege anayejitutumua na kuanza kuruka kabla ya mabawa na manyoya yake kuota vizuri. Kifaranga kinapaswa kiwe na subira; kikijitutumua na kuruka, huenda kikajiumiza au kuzama na kufa majini. Kila jambo na wakati wake. Tusitamani utajiri, cheo, au mamlaka kwa haraka haraka bila hata ya kupata uzoefu. Mungu aliweka matawi ya chini kwa ajili ya wale wasioweza kuruka vizuri ili hata wakianguka, wasipate kuumia sana. Na hata baada ya kufanikiwa kuruka, tambua kwamba hata ukifanikiwa kuruka juu kiasi gani, lazima utarudi chini tu kwa ajili ya kutafuta chakula.* mkia ukikatika ng'ombe hawezi kuazima kufukuzia nzi, linda heshima yako ukiipoteza hutaweza kuazima heshima ya mtu mwingine kujiheshimisha. Mchana mwema.
”
”
©️Pd. PK