Kiongozi Quotes

We've searched our database for all the quotes and captions related to Kiongozi. Here they are! All 25 of them:

β€œ
Nafasi yako peponi itapotea iwapo utamruhusu Pluto (kiongozi wa ahera) akukaribishe bazarai (makao makuu ya ahera) kwa kuchukua maisha yako mwenyewe. Kujiua ni kujipenda zaidi kuliko unaowapenda. Anayejiua hujifikiria zaidi yeye kuliko wengine.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Mandela alikuwa hodari ndiyo maana akapelekwa jela. Alikuwa mvumilivu ndiyo maana akakaa jela kwa miaka ishirini na saba. Alivyotoka akawa kiongozi bora wa Afrika Kusini. Utu ukafanya awasamehe binadamu wenzake. Urithi wa Nelson Mandela kwetu ni uhodari, uvumilivu, uongozi bora, utu na msamaha kwa binadamu wenzetu. Mandela alikuwa baba kwa familia yake. Kwa Afrika Kusini alikuwa mlezi wa ndoto, ya amani na uhuru.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Lakini damu na maji vina maana kubwa katika maisha yetu. Biblia inaeleza kuwa wakati Yesu Kristo akiwa msalabani alichomwa ubavu wake kwa mkuki, ikatoka damu na maji, ndipo zilipozaliwa sakramenti za kanisa. Aidha, tukio la askari wa Kirumi kumchoma Yesu na damu na maji kutoka lina maana nyingine kubwa katika maisha yetu. Hapo ndipo Ukristo ulipozaliwa; na ni kwa sababu hiyo mwanamke anapojifungua hutoa damu na maji kutokana na kupasuka kwa utando wa mfuko wa uzazi. Kutokana na hayo, Wakristo wanapoabudu msalaba wanaeleza umuhimu wa matukio na mafundisho waliyopata kupitia mateso aliyopata kiongozi wao na kuwa, msalaba ni chombo cha ukombozi.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Mpelelezi wa Tume ya Dunia kutoka Israeli Daniel Yehuda Ben-Asher Ebenezer, Mhebrania aliyeishi Givat Ram, Jerusalem, na mke wake mrembo Hadara na mtoto wake mzuri Navah Ebenezer, alikuwa Ukanda wa Gaza siku alipopigiwa simu na Kiongozi wa Kanda ya Asia-Australia ya Tume ya Dunia U Nanda – kutoka Copenhagen kuhusiana na wito wa haraka wa kuonana na Rais wa Tume ya Dunia. Yehuda aliondoka usiku kwenda Yangon, Myama, ambapo alionana na U Nanda na kupewa maelekezo yote ya kikazi aliyotakiwa kuyafuata. Mbali na maelekezo yote ya kikazi aliyotakiwa kuyafuata, Nanda alimkabidhi Yehuda kachero wa Kolonia Santita Mandi Dickson Santana (bila kujua kama Mandi ni kachero wa Kolonia Santita) ili amsindikize mpaka stendi ya mabasi ya Maubin, nje ya Yangon. Baada ya hapo Yehuda alisafiri mpaka Copenhagen ambapo yeye na wenzake walikabidhiwa Operation Devil Cross, ya kung’oa mizizi ya Kolonia Santita duniani kote. Yehuda alifanya kosa kubwa kuonana na kachero wa Kolonia Santita Mandi Santana! Kwa sababu hiyo, sauti na picha ya Yehuda vilichukuliwa, watu wengi walikufa katika miji ya Copenhagen na Mexico City.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Meja Jenerali U Nanda, 60, Kiongozi wa Kanda ya Asia-Australia ya Tume ya Dunia ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya, alizaliwa Jumamosi ya tarehe 19/03/1932 kandokando ya mto huko Maubin nchini Bama. Yeye na familia yake ni waumini wa dini ya Ubuda. Mke wake, Daw Aung Phyu, ana miaka 57. Alizaliwa Jumapili ya tarehe 20/10/1935. Nanda na Aung Phyu wana watoto watatu. Ko Mahn Thiri (wa kiume na wa kwanza kuzaliwa) ana miaka 37. Alizaliwa Alhamisi ya tarehe 08/12/1955. Yeye na familia yake wanakaa nchini Tailandi. Ma Nang Nyi ni mtoto wa pili wa familia ya Nanda na Aung Phyu. Alikufa kwa madawa ya kulevya Jumamosi ya tarehe 12/05/1980 akiwa na miaka 23. Alizaliwa Jumamosi ya tarehe 06/04/1957. Miaka miwili baadaye mpenzi wake wa kiume, Ko San Pe, alikufa kwa madawa ya kulevya pia Jumatano ya tarehe 21/07/1982 akiwa na miaka 25. Alizaliwa Jumanne ya tarehe 29/01/1957. Ma Thida Wai Aung ni wa mwisho kuzaliwa. Ana miaka 34. Alizaliwa Jumatano ya tarehe 23/07/1958. Anakaa Rangoon na mume wake wa miaka sita na watoto wawili, wa kike na wa kiume. Saw Saya (Mkurugenzi wa Sekretarieti ya Kanda ya Asia-Australia ya Tume ya Dunia ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya, kutoka katika kabila la Karen) ndiye aliyempa taarifa U Nanda za kikao cha dharura cha Tume ya Dunia. Ana miaka 54. Alizaliwa Jumanne ya tarehe 01/03/1938.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Biblia pamoja na historia vinatwambia kuwa mitume kumi na wawili wa Yesu Kristo waliamua kufa kinyama kama mfalme wao alivyokufa, kwa sababu walikataa kukana imani yao juu ya Yesu Kristo. Mathayo alikufa kwa ajili ya Ukristo nchini Ethiopia kwa jeraha lililotokana na kisu kikali, Marko akavutwa na farasi katika mitaa ya Alexandria nchini Misri mpaka akafa, kwa sababu alikataa kukana jina la Yesu Kristo. Luka alinyongwa nchini Ugiriki kwa sababu ya kuhubiri Injili ya Yesu Kristo katika nchi ambapo watu hawakumtambua Yesu. Yohana alichemshwa katika pipa la mafuta ya moto katika kipindi cha mateso makubwa ya Wakristo nchini Roma, lakini kimiujiza akaponea chupuchupu, kabla ya kufungwa katika gereza la kisiwa cha Patmo (Ugiriki) ambapo ndipo alipoandika kitabu cha Ufunuo. Mtume Yohana baadaye aliachiwa huru na kurudi Uturuki, ambapo alimtumikia Bwana kama Askofu wa Edessa. Alikufa kwa uzee, akiwa mtume pekee aliyekufa kwa amani. Petro alisulubiwa kichwa chini miguu juu katika msalaba wa umbo la X kulingana na desturi za kikanisa za kipindi hicho, kwa sababu aliwaambia maadui zake ya kuwa alijisikia vibaya kufa kama alivyokufa mfalme wake Yesu Kristo. Yakobo ndugu yake na Yesu (Yakobo Mkubwa), kiongozi wa kanisa mjini Yerusalemu, alirushwa kutoka juu ya mnara wa kusini-mashariki wa hekalu aliloliongoza la Hekalu Takatifu (zaidi ya futi mia moja kwenda chini) na baadaye kupigwa kwa virungu mpaka akafa, alipokataa kukana imani yake juu ya Yesu Kristo. Yakobo mwana wa Zebedayo (Yakobo Mdogo) alikuwa mvuvi kabla Yesu Kristo hajamwita kuwa mchungaji wa Injili yake. Kama kiongozi wa kanisa hatimaye, Yakobo aliuwawa kwa kukatwa kichwa mjini Yerusalemu. Afisa wa Kirumi aliyemlinda Yakobo alishangaa sana jinsi Yakobo alivyolinda imani yake siku kesi yake iliposomwa. Baadaye afisa huyo alimsogelea Yakobo katika eneo la mauti. Nafsi yake ilipomsuta, alijitoa hatiani mbele ya hakimu kwa kumkubali Yesu Kristo kama kiongozi wa maisha yake; halafu akapiga magoti pembeni kwa Yakobo, ili na yeye akatwe kichwa kama mfuasi wa Yesu Kristo. Bartholomayo, ambaye pia alijulikana kama Nathanali, alikuwa mmisionari huko Asia. Alimshuhudia Yesu mfalme wa wafalme katika Uturuki ya leo. Bartholomayo aliteswa kwa sababu ya mahubiri yake huko Armenia, ambako inasemekana aliuwawa kwa kuchapwa bakora mbele ya halaiki ya watu iliyomdhihaki. Andrea alisulubiwa katika msalaba wa X huko Patras nchini Ugiriki. Baada ya kuchapwa bakora kinyama na walinzi saba, alifungwa mwili mzima kwenye msalaba ili ateseke zaidi. Wafuasi wake waliokuwepo katika eneo la tukio waliripoti ya kuwa, alipokuwa akipelekwa msalabani, Andrea aliusalimia msalaba huo kwa maneno yafuatayo: "Nimekuwa nikitamani sana na nimekuwa nikiitegemea sana saa hii ya furaha. Msalaba uliwekwa wakfu na Mwenyezi Mungu baada ya mwili wa Yesu Kristo kuning’inizwa juu yake." Aliendelea kuwahubiria maadui zake kwa siku mbili zaidi, akiwa msalabani, mpaka akaishiwa na nguvu na kuaga dunia. Tomaso alichomwa mkuki nchini India katika mojawapo ya safari zake za kimisionari akiwa na lengo la kuanzisha kanisa la Yesu Kristo katika bara la India. Mathiya alichaguliwa na mitume kuchukua nafasi ya Yuda Iskarioti, baada ya kifo cha Yuda katika dimbwi la damu nchini India. Taarifa kuhusiana na maisha na kifo cha Mathiya zinachanganya na hazijulikani sawasawa. Lakini ipo imani kwamba Mathiya alipigwa mawe na Wayahudi huko Yerusalemu, kisha akauwawa kwa kukatwa kichwa. Yuda Tadei, ndugu yake na Yesu, aliuwawa kwa mishale alipokataa kukana imani yake juu ya Yesu Kristo. Mitume walikuwa na imani kubwa kwa sababu walishuhudia ufufuo wa Yesu Kristo, na miujiza mingine. Biblia ni kiwanda cha imani. Tunapaswa kuiamini Biblia kama mitume walivyomwamini Yesu Kristo, kwa sababu Biblia iliandikwa na mitume.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Komandoo Nicolas Kahima Kankiriho ('Kahima the Warrior') alizaliwa katika Wilaya ya Bushenyi, Ankole, kusini-magharibi mwa Uganda, Julai 24, 1954, mtoto wa tano kuzaliwa, katika familia ya watoto sita ya Nicodemas Kankiriho; mzee wa heshima wa Wabaima, aliyekuwa akisifika sana kwa uchungaji (wa mifugo) na msisitizo mkali wa ukiristo kwa watoto wake wote; hasa Kahima na Yebare, binti yake wa pekee, aliyekuwa wa mwisho kuzaliwa. Kahima (futi 6 inchi 3 aliyekuwa akiongea Kinyankole, Kiswahili, Kiingereza na Kihispania kwa ufasaha), baada ya kutoka Uganda – kwa mafunzo ya mwanzo ya ukomandoo ya Kiisraeli – alikwenda Urusi na Korea ya Kaskazini ambako aliongeza ujuzi hadi kiwango cha juu kabisa; kabla ya kwenda Amerika ya Kusini, kama askari wa msituni wa vyama vya kisiasa visivyo rasmi vya magorila wa Kolombia. Akiwa Kolombia, Kahima alikutana na Eduardo Chapa de Christopher (kiongozi wa zamani wa Kateli ya Diablos de Amazonas, Mashetani wa Amazoni, iliyokuwa ikivilinda vyama vya kisiasa vya magorila vya Americas) ambaye alimwajiri kama mlinzi binafsi na baadaye kama mlinzi binafsi wa Carlos Pulecio AlcΓ‘ntara – kiongozi wa kwanza wa Kateli ya Kolonia Santita. AlcΓ‘ntara alipouwawa, Kahima alihamia kwa Panthera Tigrisi – Kiongozi Mkuu wa Kolonia Santita.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Kiongozi kwa sababu ya haki akibarikiwa na Mungu, hata watu anaowaongoza watabarikiwa na Mungu pia. Lakini kama kiongozi amelaaniwa na Mungu kwa sababu ya uovu, hata watu anaowaongoza watalaaniwa pia.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Wakati Yuda ikiongozwa na kiongozi mzuri na mwenye haki kama Yosia, taifa lilistawi. Lakini ilipokuwa chini ya mwovu Manase, taifa lilisambaratika. Katika karne hii, Uingereza ilipata msukosuko mkubwa mwaka 1936 juu ya uamuzi wa Edward VIII kuoa mwanamke wa Kimarekani aliyekuwa mtalaka Wallis Simpson. Uamuzi huo ulisababisha matatizo makubwa ya kikatiba, na nusura serikali ya Uingereza ijiuzuru. Hata hivyo, kaka yake mdogo, George VI, kwa mapenzi makubwa na nchi yake, huku akikataa katakata kuondoka London wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia, aliliongoza taifa hilo katika kipindi kigumu zaidi kuliko vyote katika historia ya Uingereza. Kanuni hii ya uongozi ina ukweli katika jambo lolote kubwa na hata dogo la ujasiri.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Katika maisha, kila mtu ni kiongozi na ni mfuasi pia kutegemeana na hali. Kiongozi hatakiwi kuwa na kiburi, wala hatakiwi kuwa na roho yenye kutakabari, roho ya jeuri na kuona wengine si kitu, kwa sababu kiburi na roho yenye kutakabari huleta maangamizi na maanguko makubwa katika jamii. Viongozi wa mataifa wana jukumu kubwa kwa sababu kama wataruhusu maadili yaanguke, nguvu zao zote za kijeshi na kiteknolojia hazitawasaidia. Sifa ya kwanza ya kiongozi ni kuwa na maadili mema.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Hatumtaki kiongozi anayeishi katika mifuko ya mafisadi, tunamtaka kiongozi anayeishi katika ibara za katiba ya nchi. Kitambi bila Yesu ni jipu.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Kuna nguzo saba ambazo hazina budi kuzingatiwa kama unataka kuheshimiwa na kuwaheshimu wengine. Kwanza kabisa jitambue: wewe ni nani na unafanya nini hapa duniani. Halafu, kabla ya kusema jambo lolote kwa mtu yoyote fikiria kwanza maana au madhara ya hilo unalotaka kulisema. Kisha jifunze tamaduni mbalimbali na watendee wengine kama vile unavyotaka kutendewa au kama vile wanavyotaka kutendewa. Jifunze kusamehe na kusuluhisha migogoro katika jamii unamoishi huku ukidumisha heshima na utu kwa binadamu wenzako. Jijengee imani kwa watu, punguza upendeleo, fanya kazi kama timu kwani hakuna β€˜mimi’ katika umoja ila kuna β€˜sisi’, na jitahidi kwa kadiri ya uwezo wako WOTE kwa manufaa ya wote. Kuwa kiongozi katika kila jambo unalofanya na katika kila kitu unachofanya. Jitahidi kufanya jambo au kitu kwa usahihi kwa kadiri utakavyoweza.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Kuna tofauti kati ya haki na utawala wa mabavu. Haki ni jambo ambalo mtu anastahili au kitu anachostahiki kuwa nacho. Utawala wa mabavu ni utawala wa kidikteta. Ukitenda haki lazima kuna watu watafaidi. Lazima kuna watu wataumia. Fidel Castro alikuwa kiongozi msahili. Alikuwa kiongozi aliyewezesha kutendeka kwa mambo. Kwa sababu hiyo, wachache walimpenda, wengi walimchukia. Lakini ili ufanye mazuri lazima upambane na mabaya. Shetani mwenyewe hatakuruhusu ufanye mazuri bila kukuletea mabaya.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Kura ni haki yako ya msingi kabisa kwa ajili ya maendeleo yako na ya nchi yako. Ongea na nchi yako. Yaani, chagua kiongozi atakayeweza kukuletea maendeleo. Kama hujachagua mtu, usimlalamikie yule aliyechaguliwa.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Kuna watoto wa Mungu na kuna watoto watakatifu wa Mungu. Watoto wa Mungu ni wale waliobatizwa na kumkaribisha Kristo kama kiongozi wa maisha yao, na hata wale ambao hawajabatizwa na kumkaribisha Yesu kama kiongozi wa maisha yao kwa maana ya uumbaji, wakati watoto watakatifu wa Mungu ni mitume na manabii wa kweli.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Kiongozi wa kanda ya Afrika ya Kusini ya Tume ya Dunia Kamishna Profesa Justin Mafuru, alijitolea maisha yake kufanya vitu viwili vya msingi kwa ajili ya dunia: Kukomesha madawa haramu ya kulevya nchini Tanzania na duniani kwa jumla, kupitia Tume ya Dunia, na kutafuta kupitia maabara za CERN ('Conseil EuropΓ©en pour la Recherche NuclΓ©aire') chembe ndogo ya 'higgs' ('Higgs Boson') inayosemekana kuhusika na uzito ('mass') wa chembe ndogo kumi na sita za atomu kasoro chembe ya mwanga; iliyopotea mara tu baada ya mlipuko wa ulimwengu wa 'Big Bang', miaka bilioni kumi na tatu nukta saba iliyopita kwa faida ya uanadamu.
”
”
Enock Maregesi (Kolonia Santita)
β€œ
Muda haututoshi. Tunajua mizigo hiyo ni ya nani. Tunajua nani aliua maafisa wetu wa polisi na maafisa wa polisi wa Meksiko na Marekani na wapita njia na kwa nini alifanya hivyo. Hatujui kwa hakika imefichwa wapi. Kuwakamata wahusika ni kazi nzito, ndugu wajumbe. Inahitaji ujasiri wa kupindukia … na kujitoa mhanga. Kuzuia mizigo ya CS-14, na kumkamata kiongozi wake, lazima tupigane kufa na kupona. Kwa siku kumi shehena zikamatwe na kuharibiwa, na viongozi wa Santita (wote) wakamatwe na kuwekwa chini ya sheria.
”
”
Enock Maregesi (Kolonia Santita)
β€œ
John Murphy alifika Moscow tarehe 1/11/1992 saa 11 alfajiri akitokea Cairo, Misri. Wakati huo Moscow kulikuwa na baridi sana. Teksi yake ilipofika Teatralny Proezd, upande wa kusini wa Hoteli ya Metropol – karibu na mojawapo ya minara ya mwanzo ya Kitay-gorod, kitovu kikuu cha biashara cha Moscow ya kale – kwa matatizo ya injini; magaidi wanne, waliokuwa wakimfuatilia kwa gari aina ya Bentley Continental S nyeusi – iliyokuwa na namba za kitemi za B 001 BB 77 RUS mali ya Kiongozi wa CS-Moscow Dmitri Olegushka – toka Uwanja wa Ndege wa Sheremetyevo II wa kaskazini-magharibi mwa jiji la Moscow, waliendelea mbele na kusimama mkabala na Jumba la Maonyesho ya Tamthilia la Bolshoy; kisha wawili kati yao wakashuka na kuingia ndani ya kioski, wawili wakibaki ndani ya gari kuhakikisha John Murphy hawapotei. Magaidi hao wa CS-Moscow, Tawi la Kolonia Santita la Urusi na nchi zote za Ulaya ya Mashariki na baadhi ya nchi za Ulaya ya Kusini, walijua Murphy alishawahisi.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Ndege ya Kolonia Santita, Grumman Gulfstream III, tofauti na ndege alizokuwa akitumia Panthera Tigrisi na makompade wake wa karibu, ilifanya kazi kubwa katika mgogoro wa Kolonia Santita na Tume ya Dunia. Dar es Salaam Grumman ilipomchukua kachero Giovanna Garcia wa Kolonia Santita, baada ya ndege hiyo kutumwa na makamanda wa Kolonia Santita wa Copenhagen, ilimpeleka Paris nchini Ufaransa kuhudhuria kikao cha siri cha CS-Paris. Katika kikao hicho yeye na wenzake wakapanga mauaji ya Kamanda John Murphy Ambilikile, kwa kusuka mbinu kamambe za kumteketeza, kabla ndege yake haijafika Copenhagen. Giovanna akashiriki pia kupeleka taarifa za Murphy duniani kote katika matawi yote ya Kolonia Santita, Urusi ikiwemo, ambapo Murphy alitekwa nyara na CS-Moscow. Baada ya 'mauaji' ya Murphy, Grumman iliwapeleka baadhi ya maadui waliohusika na mauaji hayo Mexico City katika makao makuu ya Kolonia Santita; kisha ikarudi Copenhagen kumchukua kiongozi wa CS-Copenhagen, Regner Steiner Valkendorff, na Kachero wa Kolonia Santita Delfina Moore.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Dikteta ni kiongozi anayetawala nchi kwa amri yake peke yake bila ya kushauriwa na mtu, hasa yule aliyeingia madarakani kwa mtutu wa bunduki. Dikteta uchwara si dikteta, ni dikteta nusu.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Kama George Bush angekuwa na amani ndani ya moyo wake na Saddam Hussein angekuwa na amani ndani ya moyo wake Vita ya Ghuba isingetokea. Vilevile, katika kitabu cha β€˜Kolonia Santita’, kama Rais wa Tume ya Dunia angekuwa na amani ndani ya moyo wake na kiongozi wa Kolonia Santita angekuwa na amani ndani ya moyo wake Kolonia Santita isingepigana na Umoja wa Mataifa. Taifa lisingepigana na taifa, na mataifa yasingepigana na magaidi.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Kiongozi wa wananchi au wa serikali hapaswi kuchaguliwa au kuteuliwa kwa ajili ya kupata sifa ya madaraka na hivyo kunyanyasa na kudharau watu kwa sababu ya madaraka yake, anapaswa kuchaguliwa au kuteuliwa kwa ajili ya kuleta mabadiliko katika nchi kama kiongozi wa dhima aliyokabidhiwa kwa unyenyekevu na heshima kwa wananchi wenzake.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Stress za mwanamke kuingia kwenye ndoa ni kubwa kuliko mwanaume ndo sababu hata Vitabu vinaonesha mwanaume ni kiongozi lakini mjini kiongozi ni hela
”
”
Chrisper Malamsha
β€œ
Tupo watu takriban bilioni saba katika dunia hii. Kila mtu ni wa kipekee. Mathalani, wewe ni tofauti na baba yako au mama yako au mtu mwingine yoyote yule. Kila mtu aliumbwa kivyake na Mwenyezi Mungu. Kila mtu ana nafasi ya kwake mwenyewe aliyopangiwa na Mungu hapa duniani. Haijalishi wewe ni mwanamke au mwanamume, mweupe au mweusi, mfupi au mrefu, mzuri au mbaya, una nafasi katika nchi na dunia hii. Unachotakiwa kufanya ni kuamka, kufumbua macho na kuujua ukweli. Tafuta maarifa katika Biblia kama wewe ni Mkristo. Tafuta maarifa katika Kurani kama wewe ni Mwislamu. Tafuta maarifa katika Yoga kama wewe haumwamini Mungu. Ukishaamka na kuujua ukweli, ukishapata nafasi katika nchi yako, kuwa kiongozi na mkarimu kwa wenzako. Jifunze kutoka kwa wengine ndani na nje ya tasnia yako. Usiwe mchoyo wa maarifa. Kuwa mwadilifu. Ukifanya hivyo utafanikiwa zaidi, utaipa heshima tasnia yako, na utaacha alama katika dunia baada ya kuondoka. Kuacha alama katika dunia si lazima upate nafasi katika dunia. Kuacha alama katika dunia acha alama katika nchi yako.
”
”
Enock Maregesi
β€œ
Tafuta kitu cha kufanya katika maisha yako unachokiamini zaidi kuliko pesa, kutoa sauti kwa ajili ya watu wasioweza kusikika kwa mfano, na ukishakipata kuwa kiongozi na mkarimu kwa wengine. Kutoa sauti kwa ajili ya watu wasioweza kusikika inaweza kuwa ndiyo nafasi yako uliyopangiwa na Mungu uitumie kwa manufaa ya wengine, si kwa manufaa yako, nafasi za wengine zitatumika kwa manufaa yako. Kuna vitu vingi ambavyo mtu anaweza kufanya; chagua kimoja kinacholeta maana zaidi katika maisha yako na ukifanye hicho, kwa nguvu zako zote.
”
”
Enock Maregesi