Kifo Quotes

We've searched our database for all the quotes and captions related to Kifo. Here they are! All 31 of them:

Kushirikiana na maadui wa nchi yetu ni hatia ya kosa la uhaini. Adhabu yake ni kifo, au kifungo cha maisha.
Enock Maregesi
Unaweza kusaliti nchi kwa sababu za kiitikadi, kisiasa, matatizo ya akili, au pesa. Ukifanya hivyo na ukabainika; utawajibika kwa adhabu ya kifo, au maisha.
Enock Maregesi
Mahatma Gandhi alipigwa risasi na kufariki dunia baada ya maisha yake kumfelisha. Lakini kifo chake kiliipatia India uhuru kutoka Uingereza. Hivyo, akafanikiwa.
Enock Maregesi
Yesu wakati anakufa msalabani hakufikiria kifo. Alifikiria maisha.
Enock Maregesi
Adam Kuambiana umerudi nyumbani ulikotoka, ukiongozwa na imani na mwanga wa wale uliowapenda na kuwapoteza. Hatuwezi kukumbuka kwamba umetutoka bila kukumbuka kwamba uliishi, na kwamba maisha yako yalitupa kumbukumbu nzuri tusizoweza kuzisahau haraka. Jumanne, siku ya kuuaga mwili uliokuwa ukitumiwa na wewe, wengine watasema Kwa heri lakini mimi nitasema Asante! Asante kwa sababu ya kipaji chako. Asante kwa sababu ya kujitahidi kwa kadiri ya uwezo wako wote, kutoa sauti kwa wale wote waliokuwa hawawezi kusikika. Asante kwa sababu ya kuacha dunia katika hali nzuri kuliko ulivyoikuta wakati ukiingia, na Asante kwa sababu ya maisha yako. Tukiendelea kuomboleza kifo cha Adam Kuambiana hapa duniani, wengine wanasherehekea kukutana naye huko mbinguni. Mchungaji wa uhai wa wote Mungu wa mbinguni ailaze roho yake mahali pema peponi: Yeye ni mwandishi wa hadithi ya maisha yetu na ndiye aliyeandika ukurasa wa mwisho wa hadithi ya Adam.
Enock Maregesi
Sabato ilianzishwa na Mungu siku ya saba ya uumbaji wake. Siku ya Sabato ni siku takatifu, iliyoko katika Amri Kumi za Mungu, ambayo hatuna budi kuitunza na kuiheshimu. Sheria ya Siku ya Sabato haikufa baada ya kifo cha Yesu Kristo msalabani kama Wakolosai wanavyodai. Wakolosai walifuata falsafa za kipagani, na walizileta falsafa hizo ndani ya mwili wa Kristo ambalo ni kanisa. ‘Usiiamini’ Wakolosai 2:17. Iamini Wakolosai 2:20-23, ambapo Paulo anafundisha Mataifa jinsi ya kuitunza Sabato, na 1 Wakorintho 12:27 ambayo inatoa maana halisi ya Wakolosai 2:17. ‘Mwili wako ni wa Kristo’ ni tofauti na ‘mwili wa Kristo’ na ni tofauti na kanisa. Ukiamini kama mwili wako ni wa Kristo na ni kanisa, utaitunza Sabato.
Enock Maregesi
Kufanikiwa katika maisha lazima kitu fulani ambacho si cha kawaida kitokee katika maisha yako, bila kujali uko upande wa Yesu au upande wa Shetani. Kufanikiwa katika maisha ni sawa na kwenda mbinguni, au kuishi mbinguni duniani. Kitu ambacho si cha kawaida kutokea katika maisha yako ni sawa na kifo. Fanya kitu ambacho hujawahi kufanya kupata kitu ambacho hujawahi kupata.
Enock Maregesi
Hakuna shaka yoyote (kwa mfano) kwamba mboga za majani na matunda vina vitamini nyingi mwilini na madini na vitu vyote vizuri katika mwili wa binadamu, na kwamba kadhalika vina kirutubisho cha ufumwele ambacho huzuia kufunga choo na matatizo mengine ya mfumo wa usagaji chakula. Kirutubisho hiki kikizidi mwilini utapata matatizo makubwa yatakayoweza hata kukusababishia kifo!
Enock Maregesi
Taabini hii ni ngumu sana kwangu kuandika pamoja na kwamba ni miaka mitatu kamili toka giza liingie. Mwaka 2014, Novemba 4, nilimpoteza bibi yangu mpendwa, Martha Maregesi, aliyefariki dunia kutokana na ukongo wa kiharusi, na tutamkumbuka daima. Alikuwa na roho ya kipekee; na kifo chake kiliwagusa wengi, pamoja na kwamba aliishi maisha kamili, zaidi ya siku 25550, siku 5110 zaidi, ambazo ndizo tulizopangiwa na Mungu. Mapenzi ya mtu kwa bibi yake ni mapenzi ya kipekee. Nadhani Mungu aliwapa mabibi wote uwezo maalumu wa kuwapenda wajukuu zao, na kufanya maisha yao yatimie, kuwafanya wawe binadamu wazuri na wenye maadili mema. Alichangia pakubwa katika malezi yangu ya utotoni; na aghalabu naweza kukumbuka nikiwa naye jikoni akipika, huku mimi nikifanya kazi nyingine, lakini wakati huohuo akinifundisha mambo kadha wa kadha ya kunikomaza kimaisha. Bibi hakuwa tu bibi. Alikuwa mlezi, rafiki na mtu aliyenihamasisha sana katika maisha. Kifo kinaleta huzuni lakini kinaleta tumaini. Naamini bibi yangu atakwenda mbinguni, kwa sababu naamini alitubu dhambi zake akisaidiwa na wachungaji. Wachungaji hao walimtembelea kila siku, nyumbani au hospitalini, akiwa kitandani kwake akiugua. Bibi yangu alitimiza wajibu wake. Alizaliwa, aliishi, na alikufa katika toba. Siku nitakapokufa ningependa kuzikwa jirani na alipozikwa bibi yangu, ili Yesu atakaporudi tufufuke pamoja.
Enock Maregesi
Biblia pamoja na historia vinatwambia kuwa mitume kumi na wawili wa Yesu Kristo waliamua kufa kinyama kama mfalme wao alivyokufa, kwa sababu walikataa kukana imani yao juu ya Yesu Kristo. Mathayo alikufa kwa ajili ya Ukristo nchini Ethiopia kwa jeraha lililotokana na kisu kikali, Marko akavutwa na farasi katika mitaa ya Alexandria nchini Misri mpaka akafa, kwa sababu alikataa kukana jina la Yesu Kristo. Luka alinyongwa nchini Ugiriki kwa sababu ya kuhubiri Injili ya Yesu Kristo katika nchi ambapo watu hawakumtambua Yesu. Yohana alichemshwa katika pipa la mafuta ya moto katika kipindi cha mateso makubwa ya Wakristo nchini Roma, lakini kimiujiza akaponea chupuchupu, kabla ya kufungwa katika gereza la kisiwa cha Patmo (Ugiriki) ambapo ndipo alipoandika kitabu cha Ufunuo. Mtume Yohana baadaye aliachiwa huru na kurudi Uturuki, ambapo alimtumikia Bwana kama Askofu wa Edessa. Alikufa kwa uzee, akiwa mtume pekee aliyekufa kwa amani. Petro alisulubiwa kichwa chini miguu juu katika msalaba wa umbo la X kulingana na desturi za kikanisa za kipindi hicho, kwa sababu aliwaambia maadui zake ya kuwa alijisikia vibaya kufa kama alivyokufa mfalme wake Yesu Kristo. Yakobo ndugu yake na Yesu (Yakobo Mkubwa), kiongozi wa kanisa mjini Yerusalemu, alirushwa kutoka juu ya mnara wa kusini-mashariki wa hekalu aliloliongoza la Hekalu Takatifu (zaidi ya futi mia moja kwenda chini) na baadaye kupigwa kwa virungu mpaka akafa, alipokataa kukana imani yake juu ya Yesu Kristo. Yakobo mwana wa Zebedayo (Yakobo Mdogo) alikuwa mvuvi kabla Yesu Kristo hajamwita kuwa mchungaji wa Injili yake. Kama kiongozi wa kanisa hatimaye, Yakobo aliuwawa kwa kukatwa kichwa mjini Yerusalemu. Afisa wa Kirumi aliyemlinda Yakobo alishangaa sana jinsi Yakobo alivyolinda imani yake siku kesi yake iliposomwa. Baadaye afisa huyo alimsogelea Yakobo katika eneo la mauti. Nafsi yake ilipomsuta, alijitoa hatiani mbele ya hakimu kwa kumkubali Yesu Kristo kama kiongozi wa maisha yake; halafu akapiga magoti pembeni kwa Yakobo, ili na yeye akatwe kichwa kama mfuasi wa Yesu Kristo. Bartholomayo, ambaye pia alijulikana kama Nathanali, alikuwa mmisionari huko Asia. Alimshuhudia Yesu mfalme wa wafalme katika Uturuki ya leo. Bartholomayo aliteswa kwa sababu ya mahubiri yake huko Armenia, ambako inasemekana aliuwawa kwa kuchapwa bakora mbele ya halaiki ya watu iliyomdhihaki. Andrea alisulubiwa katika msalaba wa X huko Patras nchini Ugiriki. Baada ya kuchapwa bakora kinyama na walinzi saba, alifungwa mwili mzima kwenye msalaba ili ateseke zaidi. Wafuasi wake waliokuwepo katika eneo la tukio waliripoti ya kuwa, alipokuwa akipelekwa msalabani, Andrea aliusalimia msalaba huo kwa maneno yafuatayo: "Nimekuwa nikitamani sana na nimekuwa nikiitegemea sana saa hii ya furaha. Msalaba uliwekwa wakfu na Mwenyezi Mungu baada ya mwili wa Yesu Kristo kuning’inizwa juu yake." Aliendelea kuwahubiria maadui zake kwa siku mbili zaidi, akiwa msalabani, mpaka akaishiwa na nguvu na kuaga dunia. Tomaso alichomwa mkuki nchini India katika mojawapo ya safari zake za kimisionari akiwa na lengo la kuanzisha kanisa la Yesu Kristo katika bara la India. Mathiya alichaguliwa na mitume kuchukua nafasi ya Yuda Iskarioti, baada ya kifo cha Yuda katika dimbwi la damu nchini India. Taarifa kuhusiana na maisha na kifo cha Mathiya zinachanganya na hazijulikani sawasawa. Lakini ipo imani kwamba Mathiya alipigwa mawe na Wayahudi huko Yerusalemu, kisha akauwawa kwa kukatwa kichwa. Yuda Tadei, ndugu yake na Yesu, aliuwawa kwa mishale alipokataa kukana imani yake juu ya Yesu Kristo. Mitume walikuwa na imani kubwa kwa sababu walishuhudia ufufuo wa Yesu Kristo, na miujiza mingine. Biblia ni kiwanda cha imani. Tunapaswa kuiamini Biblia kama mitume walivyomwamini Yesu Kristo, kwa sababu Biblia iliandikwa na mitume.
Enock Maregesi
WWPP ('WODEA Witness Protection Programme') ni Programu Maalumu ya Ushahidi ya Tume ya Dunia ya kuwakinga mashahidi wa kihalifu kwa kuwapa makazi mapya, majina mapya, kazi mpya, historia mpya ya maisha, na sura mpya, kuwakinga na Sheria ya Kitalifa ya Kolonia Santita. Ukivunja Sheria ya Kitalifa ya Kiapo cha Swastika cha Kolonia Santita utauwawa, tena utauwawa kinyama, wewe na familia yako.
Enock Maregesi
Kofia za chuma au sandarusi zenye uwezo wa kukwepesha risasi za wadunguzi na kuzuia mpaka risasi tatu za AK-47, ijapokuwa zimetengenezwa kuzuia risasi moja tu, ni miongoni mwa vitu 17 vilivyobebwa na makomandoo wa Tume ya Dunia; wakati wakitekeleza Operesheni ya Kifo au Ushindi Kamili (operesheni ndogo ya Operation Devil Cross ya Tume ya Dunia) katika Msitu wa Benson Bennett, Salina Cruz, Oaxaca, nchini Meksiko. Thamani ya vitu vya komandoo mmoja wa EAC ('Executive Action Corps') akiwa vitani ni zaidi ya dola za Kimarekani 65,000; ikiwa ni pamoja na magwanda ya jeshi ('Ghillie Suits'), kofia za chuma, miwani ya kuonea usiku (yenye uwezo wa kubinuka chini na juu), redio na mitambo ya mawasiliano migongoni mwao juu ya vizibao vya kuzuia risasi, vitibegi vya msalaba mwekundu ('Blowout kits' – katika mapaja ya miguu yao ya kulia, ndani yake kukiwa na pisto na madawa ya huduma ya kwanza), vitibegi vya kujiokolea ('Evasion Kits' – katika mapaja ya miguu yao ya kushoto, ndani yake kukiwa na visu na pesa na ramani ya Meksiko) na bunduki za masafa marefu.
Enock Maregesi
Kikwazo kikubwa cha kwenda mbinguni ni kifo. Kikwazo kikubwa cha kwenda ahera ni uzima wa milele. Kikwazo kikubwa cha kwenda mbinguni ni Shetani. Kikwazo kikubwa cha kwenda ahera ni Yesu Kristo. Yesu Kristo ni njia iliyo huru ya kwenda mbinguni. Shetani ni njia iliyo huru ya kwenda ahera.
Enock Maregesi
Kitalifa ni utiifu kamili, woga, umbali (kwa maana ya kuwa mbali na biashara ya mamafia wengine mpaka kwa makubaliano maalumu) na nidhamu ya kutoshirikiana na mamlaka zote za serikali. Ukishtakiwa kwa kosa la madawa au ujambazi ambalo hukufanya, utatumikia kifungo mpaka mwisho bila kushirikiana na polisi (kwa maana ya kutaja aliyehusika au waliohusika na uhalifu huo) hata kama aliyehusika au waliohusika hana au hawana uhusiano wowote na Kolonia Santita. Falsafa ya Kitalifa ni Sheria ya Kitalifa ya Kiapo cha Swastika cha Kolonia Santita. Na adhabu ya kuvunja sheria hiyo ni kifo.
Enock Maregesi
Kikwazo kikubwa cha kwenda mbinguni ni kifo!
Enock Maregesi
Kula sana ni kujichimbia kaburi kwa meno yako mwenyewe.
Enock Maregesi
Kula sana kunaweza kusababisha virutubisho kuzidi mwilini zaidi ya kiwango kinachohitajika na mwili, ambavyo baadaye vinaweza kusababisha madhara ya papo kwa hapo kama tumbo kuuma au tumbo kujaa gesi! Baada ya muda mrefu wingi wa virutubisho hivi unaweza kuingiliana na ufyonzaji wa madini kama fosforasi, kalisi, magnesi, chuma, na zinki, hali inayoweza kusababisha upungufu mkubwa wa virutubisho, unaoweza kusababisha kifo.
Enock Maregesi
Yeyote anayekufa chini ya miaka 70 ameuwawa.
Enock Maregesi
Dhambi ya Adamu ilileta mauti duniani (kwa viumbe vyote, si tu kwa binadamu). Hiyo ni kwa mujibu wa Biblia. Kisayansi si kweli; kwa sababu mauti yalikuwepo kabla Adamu na Hawa hawajaumbwa! Lakini haya ndiyo mawazo yangu: Dhambi iliathiri uumbaji wote ikiwemo mimea, wanyama, wadudu na kila kitu kilichoumbwa na Mwenyezi Mungu; ambavyo huteseka kwa sababu ya laana ya dunia. Kama wanyama na mimea visingekuwa vinakufa, binadamu wasingepata mahali pa kuishi. Hata hivyo, kifo cha Yesu msalabani kitafufua kila kitu – kitafufua uumbaji wote.
Enock Maregesi
Siku moja, jambo baya litatokea. Labda babu yako au mnyama wako kipenzi atafariki au shangazi yako atagundulika na kansa. Labda utafukuzwa kazi au utaachika kwa mumeo au mkeo mliyependana sana. Labda rafiki yako kipenzi atapata ajali mbaya ya gari na utatakiwa kupeleka taarifa kwa ndugu na marafiki zake. Kutoa taarifa ya jambo baya kwa mtu ni kazi ngumu sawa na kupokea taarifa ya jambo baya kutoka kwa mtu. Kama umeteuliwa kupeleka taarifa ya kifo au ya jambo lolote baya kwa mtu fanya hivyo kwa makini. Toa taarifa ya msiba au ya jambo lolote baya kwa hekima na busara kama Ibrahimu alivyofanya kwa Sara kuhusiana na kafara ya Isaka, si kama Mbenyamini alivyofanya kwa Eli kuhusiana na kutwaliwa kwa sanduku la agano na kuuwawa kwa watoto wake wawili. Jidhibiti kwanza wewe mwenyewe kama umeteuliwa kupeleka taarifa ya kifo au ya jambo lolote baya. Angalia kama wewe ni mtu sahihi wa kupeleka taarifa hiyo. Pangilia mawazo ya kile unachotaka kwenda kukisema au unachotaka kwenda kukiandika. Mwangalie machoni, si usoni, yule unayempelekea taarifa kisha mwambie kwa sauti ya upole nini kimetokea.
Enock Maregesi
Hakimu na Kuhani Mkuu wa Shilo Eli alipata matatizo makubwa wakati wa mgogoro wa Waisraeli na Wafilisti, kati ya mwaka 2871 na 2870 Kabla ya Kristo. Mara tu baada ya kupewa taarifa ya kifo cha watoto wake wawili, Hofni na Finehasi, na kutwaliwa kwa Sanduku la Agano la Bwana wa Majeshi lililohifadhi Amri Kumi za Mungu, Eli alianguka kutoka katika kiti chake na kufariki papo hapo akiwa na umri wa miaka 98. Aidha, mkwe wa Eli, mke wa Finehasi, alijifungua ghafla na kufariki alipopata taarifa ya kifo cha mkwewe na taarifa ya kuuwawa kwa mumewe na ya kutekwa nyara kwa Sanduku la Agano. Mwanajeshi kutoka Benyamini falaula angetumia hekima na busara kutoa taarifa ya kifo na ya kutwaliwa kwa Sanduku la Agano huenda Eli asingefariki, na huenda mkwewe asingejifungua mtoto njiti na huenda asingekufa siku hiyo. Kwani Sanduku la Agano lilirejeshwa nchini Israeli, na Wafilisti wenyewe, baada ya miezi saba tangu litwaliwe, na kifo cha watoto wa Eli yalikuwa mapenzi ya Mungu. Hivyo Eli asingeweza kuzuia kifo cha watoto wake, na Wafilisti wasingeweza kukaa na Sanduku la Agano milele. Lakini katika kafara ya Isaka ambapo Isaka aliamua kujitoa kafara mwenyewe kumfurahisha Mungu na baba yake kama Yesu alivyoamua kujitoa kafara mwenyewe kumfurahisha Mungu na baba yake wa mbinguni, Sara angekufa kama Ibrahimu hangetumia hekima alipomwambia anakwenda kumtolea Bwana kafara ya mwanakondoo wakati akijua anakwenda kumtoa Isaka mtoto wa pekee wa Sara. Hekima inatoka moyoni, busara inatoka mdomoni. Kwa vile suala la kutoa taarifa mbaya kwa mtu ni gumu kwa yule anayetoa na kwa yule anayepokea, hekima na busara havina budi kutumika.
Enock Maregesi
Mungu ni mkubwa kuliko jumla ya matatizo yote na vitu vyote alivyoviumba na ana uwezo wa kufanya kila kitu alichosema atafanya bila kupunguza au kuongeza chochote. Usidanganywe na matatizo. Amka, kabla kifo hakijakufika.
Enock Maregesi
Yesu Kristo hakufa siku ya Ijumaa jioni na kufufuka siku ya Jumapili asubuhi. Alikufa siku ya Jumatano jioni na kukufuka siku ya Jumamosi jioni. Wakati kifo kinamkumba, hakuwa na umri wa miaka 33, alikuwa na umri wa miaka 31. Kama Yesu Kristo alikufa siku ya Ijumaa jioni, na kufufuka siku ya Jumapili asubuhi, hatuna Mwokozi!
Enock Maregesi
Mungu asingekuwepo matajiri wangehonga kifo ili waishi milele.
Enock Maregesi
Kilio kikuu cha Yesu, “Eloi, Eloi, lama sabakthani?”, yaani, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?”, na “Imekwisha”, vilitabiriwa katika Zaburi 22 ili watu waliompinga Kristo waamini kama Yesu alikuwa Masihi. Zaburi 22 ulikuwa wimbo maarufu katika kipindi cha karne ya kwanza, kipindi ambacho Yesu alizaliwa na kufa, uliotungwa na mfalme Daudi, ulioitwa ‘zaburi ya mateso na matumaini ya mwadilifu’. Kwa hiyo Yesu aliposema maneno hayo yaliwaingia watu akilini, na kuanzia hapo imani hasa ya Ukristo ikachukua kasi hadi leo hii. Zaburi 22 inaanza na “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?” na inaisha na “Imekwisha”, miongoni mwa maneno saba aliyoyasema Yesu pale msalabani Golgotha. Kwa hiyo, Zaburi 22 ni utabiri wa kifo cha Yesu.
Enock Maregesi
Kuna sababu za msingi na za kinabii za damu na maji vilivyotoka katika mbavu za Yesu Kristo msalabani. Ubavu wake uliochomwa na mkuki ulithibitisha kifo chake cha kibinadamu, huku vingine vyote vikitimiza unabii wake uliotajwa na Yohana.
Enock Maregesi
Askari wa Kirumi alimchoma Yesu mkuki ili andiko litimie. Askari huyo ambaye Biblia haikumtaja jina kwa sababu zilizoko nje ya uwezo wetu, alivyoona kweli amepona na ameona alishuhudia, na ushuhuda wake ulitoka moyoni, ili nasi tupate kusadiki. Wauaji wa Kirumi walipoona kwamba wale wezi waliosulubiwa pamoja na Yesu walikuwa bado hawajakata roho, waliwavunja miguu ili washindwe kupumua na hivyo kuharakisha kifo chao. Kwa upande wa Yesu, waliona alishapoteza fahamu na labda alishafariki. Kuthibitisha hilo askari wa Kirumi alirusha mkuki, nao ukatoboa utando unaozunguka moyo wa Yesu na mapafu ya Yesu, na damu na maji kutoka. Lakini yote hayo yalishatabiriwa miaka mingi kabla ya Yesu: ‘Hakuna hata mfupa wake mmoja utakaovunjwa’ na ‘Nao watamtazama yeye ambaye walimchoma’.
Enock Maregesi
Kuna mambo yanatokea hapa ulimwenguni ambayo yanafanya nikiri uwepo wa Mungu kwa asilimia kubwa. Wanasayansi wanasema ulimwengu ulianzishwa na mlipuko wa ‘Big Bang’, uliotokea takribani miaka bilioni 14 iliyopita, kutoka katika kitu kidogo zaidi kuliko ncha ya sindano, lakini hawatuambii nini kilisababisha mlipuko huo utokee au hicho kitu kidogo kuliko ncha ya sindano kilitoka au kilikuwa wapi. Wanaendelea kusema kuwa baada ya ‘Big Bang’ kutakuwepo na ‘Big Crunch’, ambapo ulimwengu utarudia hali yake ya awali ya udogo kuliko ncha ya sindano, na kila kitu kinachoonekana leo ulimwenguni hakitaonekana tena. Hapo sasa ndipo utata unapokuja. Mlipuko wa ‘Big Bang’ ulipotokea ulimwengu ulilipuka na kusambaa pande zote nne za ulimwengu kwa mwendokasi wa zaidi ya kilometa milioni 2 kwa saa, mpaka hivi leo unavyoonekana na bado unaendelea kusambaa. Kutokana na dhana ya ‘Big Crunch’, wanasayansi wanaamini ulimwengu utapanuka ila baadaye utapungua mwendo na utarudi mwanzo kabisa mahali ulipolipukia. Lakini mwaka 1995 wanasayansi hao hao waligundua kitu. Ulimwengu – badala ya kupungua mwendo wa kupanuka kama wanasayansi walivyokuwa wakitabiri – sasa unaongeza mwendo, tena kwa mwendokasi ambao haujawahi kutokea. Hiki ni nini kinachosababisha ulimwengu uongeze mwendokasi kiasi hicho badala ya kuupunguza? Hicho ni nini ambacho ulimwengu unapanukia? Wanasayansi hawana jibu. Wanasingizia kitu kinaitwa ‘dark matter’, maada ambayo haijawahi kuonekana, kwamba ndicho kinachosababisha ulimwengu uongeze mwendokasi kwa kiwango hicho ambacho hakijawahi kutokea; na hicho ambacho ulimwengu unapanukia wanahisi ulimwengu wetu unapanukia katika ulimwengu mwingine, kwa mujibu wa dhana nyingine kabisa iitwayo ‘multiverse’ au ‘meta-universe’. Kuna kitu kinaitwa ‘Higgs boson’ – chembe ndogo inayosemekana kuhusika na uzito (‘mass’) wa chembe ndogo 16 zilizomo ndani ya atomu, kasoro chembe ya mwanga, iliyopotea mara tu baada ya mlipuko wa ulimwengu wa ‘Big Bang’ miaka bilioni 13.7 iliyopita katika kipindi kilichoitwa ‘epoch’ – ambayo ilianza kutafutwa katika maabara za CERN, Uswisi, toka mwaka 1964, maabara ambazo kazi yake kubwa ni kutengeneza mazingira ya mwanzo kabisa ya mlipuko wa ‘Big Bang’, kusudi wanasayansi waone kama wanaweza kubahatisha kuiona na kuidhibiti hiyo bosoni. Bosoni itakapopatikana wanasayansi watajua siri ya ‘dark matter’, watajua jinsi ulimwengu unavyofanya kazi na jinsi ulivyoumbwa na jibu la kitendawili cha ‘Standard Model’ litapatikana. Hiyo ni kazi ngumu. Ndiyo maana ‘Higgs boson’ mwaka 1993 iliitwa ‘The God Particle’. Yaani, wanasayansi wanahisi kuna muujiza wa Kimungu na huenda wasiipate kabisa hiyo bosoni. Wanasema waliipata mwaka 2013. Lakini hiyo waliyoipata bado ina utata. Kutokana na kushindwa huko kwa sayansi na historia, kutokana na kushindwa kwa sayansi kutengeneza binadamu au mnyama, kutokana na miujiza iliyorekodiwa katika vitabu vitakatifu; naamini, Mungu yupo.
Enock Maregesi
Wanasayansi wana uwezo wa kupeleleza hadi kipindi cha karne ya kwanza ambapo Yesu aliishi, alikufa, alifufuka na alipaa kwenda mbinguni, na wana uwezo wa kujua mambo mengi kwa hakika yaliyofanyika katika kipindi hicho na hata katika kipindi cha kabla ya hapo. Kuna miujiza ambayo Yesu aliifanya ambayo haiko ndani ya Biblia. Kwa mfano, Biblia inasema Yesu alizaliwa ndani ya zizi la ng’ombe wakati sayansi inasema alizaliwa nje ya zizi la ng’ombe; na muujiza wa kwanza kuufanya ambao hauko ndani ya Biblia ni kutembea mara tu baada ya kuzaliwa, na watu na ndege wa angani kuganda kabla ya kuzaliwa Masihi na kabla ya wakunga kufika kumsaidia Maria Magdalena kujifungua. Akiwa na umri wa miaka sita, sayansi inasema, Yesu alikuwa akicheza na mtoto mwenzake juu ya paa la nyumba ya jirani na mara Yesu akamsukuma mwenzake kutoka juu hadi chini na mwenzake huyo akafariki papo hapo. Watu walipomsonga sana Yesu kwa kumtuhumu kuwa yeye ndiye aliyesababisha kifo cha mwenzake, na kwamba wangemfungulia mashtaka, Yesu alikataa katakata kuhusika na kifo hicho. Lakini walipozidi kumsonga, aliusogelea mwili wa rafiki yake kisha akamwita na kumwambia asimame. Yule mtoto alisimama! Huo ukawa muujiza mkubwa wa kwanza wa Yesu Kristo, kufufua mtu nje ya maandiko matakatifu. Kuna mifano mingi inayodhihirisha uwepo wa Mungu ambayo wanasayansi hawawezi hata kuipatia majibu. Tukio la Yoshua kusimamisha jua limewashangaza wanasayansi hadi nyakati za leo. Mwanzoni mwa miaka ya 70 wanasayansi walijaribu kurudisha muda nyuma kwa kompyuta kuona kama kweli wangekuta takribani siku moja imepotea kama ilivyorekodiwa katika Biblia. Cha kushangaza, cha kushangaza mno, walikuta saa 23 na dakika 20 zimepotea katika mazingira ambayo hawakuweza na hawataweza kuyaelewa. Walipochunguza vizuri walikuta ni kipindi cha miaka ya 1500 KK (Jumanne tarehe 22 Julai) ambacho ndicho tukio la Yoshua la kusimamisha jua na kusogeza mwezi nyuma digrii 10, ambazo ni sawa na mzunguko wa dakika 40, lilipotokea. Kwa kutumia elimu ya wendo, elimu ya kupanga miaka na matukio ya Kibiblia, dunia iliumbwa Jumapili tarehe 22 Septemba mwaka 4000 KK. Hata hivyo, mahesabu ya kalenda yanaonyesha kuwa Septemba 22 ilikuwa Jumatatu (si Jumapili) na kwamba kosa hilo labda lilisababishwa na siku ya Yoshua iliyopotea. Hayo yote ni kwa mujibu wa Profesa C. A. Totten, wa Chuo Kikuu cha Yale, katika kitabu chake cha ‘Joshua’s Long Day and the Dial of Ahaz: A Scientific Vindication and a Midnight Cry’ kilichochapishwa mwaka 1890. Kama hakuna Mungu iliwezekanaje Yoshua aombe jua lisimame na jua likasimama kweli? Iliwezekanaje Yesu aseme atakufa, atafufuka na atapaa kwenda mbinguni na kweli ikatokea kama alivyosema? Ndani ya Biblia kuna tabiri 333 zilizotabiri maisha yote ya Yesu Kristo hapa duniani na zote zilitimia – bila kupungua hata moja. Utasemaje hapo hakuna Mungu? Mungu yupo, naamini, sijui. Tukio la Yesu kufa, kufufuka na kupaa kwenda mbinguni si la vitabu vitakatifu pekee, hata sayansi inakubaliana na hilo.
Enock Maregesi
Wapo watu ukitaka kuwaua wambie wasome vitabu. Hata ukiwambia someni kitabu fulani kujikinga na kifo wako tayari kufa kuliko kusoma.
Enock Maregesi
Maisha ni Dunia. Lakini Dunia ni basi. Sisi ni wasafiri. Mtu anapokufa amefika mwisho wa safari yake, huku Dunia ikiendelea.
Enock Maregesi