“
Mfundishe mtoto wako maadili mema kwa miaka kumi na tatu, katika umri wa miaka kumi na tatu fikra za mtoto huanza kuwa na maono na utambuzi wa vitu mbalimbali na watoto katika umri huo wanao uwezo wa kuchambua dhana kadha wa kadha za kinadharia na hali kadhalika wanao uwezo wa kuchambua nadharia tata zisizokuwa na hakika na hata zile zenye hakika zisizokuwa tata, kabla hujamkabidhi kwa dunia. Ukimkabidhi mtoto wako kwa dunia kabla ya umri wa miaka kumi na tatu, kama vile kumpeleka katika shule ya bweni au kumpeleka akalelewe na watu wengine ambao si wazazi wake, yale ambayo hukumfundisha atafundishwa na ulimwengu. Mpeleke mtoto wako katika shule ya bweni au kuishi na watu wengine akiwa amefundishwa maadili mema. Kinyume cha hapo atafundishwa na shule au watu wengine kwa kudharauliwa, kuchukiwa na kuadabishwa.
”
”